Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Wakaazi wa mbagala na vitongoji vyake asubuhi ya leo wamepata usumbufu mkubwa wa usafiri baada ya Lori lenye namba za usajili T 143 AQE kuanguka alfari ya leo eneo la mtongani daraja la reli.
Lori hilo lililokuwa linatoka maeneo ya mbagala lilianguka baada ya kushindwa kupandisha mlima uliopo eneo hilo la mtongani hivyo basi kurudi nyuma kwa kasi hatimaye kuanguka na kuzuia barabara zote mbili za kwenda katikati ya mji hivyo kusababisha foleni kubwa sana.
Wakaazi wa mbagala na vitongoji vyake leo kuanzia saa za alfari mpaka saa tatu walilazimika kuacha vyombo vya usafiri wa umma na kuamua kutembea umbali mrefu kutoka eneo la kizuiani hadi kwa azizi ally kutafuta usafiri mwingine.
NB. ni wakati saa umefika tunaiomba serikali haya malori yatafutiwe njia maalum ili kuondoa usumbufu kama uliojitokeza leo na siku za nyuma, kwasababu lori moja likiharibika barabara ya morogoro road au Mandela road, kilwa road basi hutatitiza mfumo wote wa usafiri kufika katikati ya mji.
Nawasilisha..!