Foleni ya masaa sita yawatesa wakazi wa Mbagala, watembea kwa miguu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
10d3618d67a0566579905996e0570560.jpg

Wakaazi wa mbagala na vitongoji vyake asubuhi ya leo wamepata usumbufu mkubwa wa usafiri baada ya Lori lenye namba za usajili T 143 AQE kuanguka alfari ya leo eneo la mtongani daraja la reli.

Lori hilo lililokuwa linatoka maeneo ya mbagala lilianguka baada ya kushindwa kupandisha mlima uliopo eneo hilo la mtongani hivyo basi kurudi nyuma kwa kasi hatimaye kuanguka na kuzuia barabara zote mbili za kwenda katikati ya mji hivyo kusababisha foleni kubwa sana.

Wakaazi wa mbagala na vitongoji vyake leo kuanzia saa za alfari mpaka saa tatu walilazimika kuacha vyombo vya usafiri wa umma na kuamua kutembea umbali mrefu kutoka eneo la kizuiani hadi kwa azizi ally kutafuta usafiri mwingine.
2b6fda133043df47ae1629856f48eb5f.jpg

NB. ni wakati saa umefika tunaiomba serikali haya malori yatafutiwe njia maalum ili kuondoa usumbufu kama uliojitokeza leo na siku za nyuma, kwasababu lori moja likiharibika barabara ya morogoro road au Mandela road, kilwa road basi hutatitiza mfumo wote wa usafiri kufika katikati ya mji.
13557751_723605994447974_2392986790000659169_n.jpg

Nawasilisha..!
 
...hizi barabara nyingi zinahitaji kupanuliwa,lorry kuanguka limefunga barabara yote!, km kuna mgonjwa alikuwa anahitaji kuwahishwa hospital alipitishwa wap?!, poleni!
 
Sio lazima kupanua barabara. Kinachotakiwa ni kuwa na gari za uokoaji zenye uwezo mkubwa. Ingekuwa gari dogo limepata ajali, hata kama halikuziba njia, lingechukuliwa na gari za uokoaji zinazokaa karibu na wanapokaa maaskari wa usalama barabarani. Kilichokosekana hapo ni uwezo wa mtambo wa uokoaji wa kuliondoa lori hilo barabarani haraka.
 
Mkuu kupanua barabara ni muhimu sana kwasababu hata hayo magari ya uokoaji some time yanashindwa kufika haraka eneo pale ambapo wananchi wanapoamua kupita barabara zote za eneo hilo hivyo hata wanaorudi kupata foleni tena
 
Tatizo la Kilwa road kuanzia mtongani sijui kwa aziz ally zaidi ya hio main road hakuna njia ingine ya pembeni. Ukiziba main road tu basi labda upite kongowe utokee kigamboni.
 
Sio lazima kupanua barabara. Kinachotakiwa ni kuwa na gari za uokoaji zenye uwezo mkubwa. Ingekuwa gari dogo limepata ajali, hata kama halikuziba njia, lingechukuliwa na gari za uokoaji zinazokaa karibu na wanapokaa maaskari wa usalama barabarani. Kilichokosekana hapo ni uwezo wa mtambo wa uokoaji wa kuliondoa lori hilo barabarani haraka.
Ni kweli kbs,hiyo ajali ilitokea jana saa nne usiku,lkn inavyoonyesha ucku kucha ulikosekana mtambo wa kuweza kuliondoa hilo lori,na askari walikuwepo.kwa kweli watu wameteseka sana......
 
Acha wafanye mazoezi ya kutembea....

Hapakazitu# mshaambiwa
 
Sio lazima kupanua barabara. Kinachotakiwa ni kuwa na gari za uokoaji zenye uwezo mkubwa. Ingekuwa gari dogo limepata ajali, hata kama halikuziba njia, lingechukuliwa na gari za uokoaji zinazokaa karibu na wanapokaa maaskari wa usalama barabarani. Kilichokosekana hapo ni uwezo wa mtambo wa uokoaji wa kuliondoa lori hilo barabarani haraka.
Maaskari wetu, hawapendi kujichanganya - how comes wasingetumia njia ya upande moja na shughuli ikaendelea?
 
Poleni sana. Juzi nikiwa kituo cha mwendokasi pale posta ya zamani kuna abiria alikata tiketi akaingia ndani akawa anasubiri gari ya mwendokasi ya kwenda mbagala. Mie niliondoka sasa sijui kama alipata usafiri
 
Kuna chanzo tofauti na hicho kilichoelezewa humu?
Ha ha ha JF raha sana..!

mkuu hata kama kungekuwa na chanzo kingine tofauti na kilichoelezwa humu.. issue ni foleni isiwepo inapoteza lengo.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Ha ha ha JF raha sana..!

mkuu hata kama kungekuwa na chanzo kingine tofauti na kilichoelezwa humu.. issue ni foleni isiwepo inapoteza lengo.
Tunakubali kweli lorry lilisababisha foleni, ila kuna wakati mwingine foleni hutokea kwa askari kutokuchanganya na za kwao, wamekariri tu.

Kwa mfano huwa sielewi kwanini kila ikifika saa 9/10 jioni magari ya kutoka Kilwa road yanazuiwa kuingia mjini, matokeo yake watu wanatembea kwa mguu toka Ufundi hadi posta,kariakoo au watu kutoka stesheni, kariakoo wanatembea kwa miguu hadi mivinjeni au ufundi kwa miguu ili wapande mabus ya kwenda Mbagala, Tandika, na Kigamboni?
 
Sio lazima kupanua barabara. Kinachotakiwa ni kuwa na gari za uokoaji zenye uwezo mkubwa. Ingekuwa gari dogo limepata ajali, hata kama halikuziba njia, lingechukuliwa na gari za uokoaji zinazokaa karibu na wanapokaa maaskari wa usalama barabarani. Kilichokosekana hapo ni uwezo wa mtambo wa uokoaji wa kuliondoa lori hilo barabarani haraka.

Well said
 
Tunakubali kweli lorry lilisababisha foleni, ila kuna wakati mwingine foleni hutokea kwa askari kutokuchanganya na za kwao, wamekariri tu.

Kwa mfano huwa sielewi kwanini kila ikifika saa 9/10 jioni magari ya kutoka Kilwa road yanazuiwa kuingia mjini, matokeo yake watu wanatembea kwa mguu toka Ufundi hadi posta,kariakoo au watu kutoka stesheni, kariakoo wanatembea kwa miguu hadi mivinjeni au ufundi kwa miguu ili wapande mabus ya kwenda Mbagala, Tandika, na Kigamboni?
Sio kwl ninachojua huwa magari ya kwenda kurudi mbagara huruhusiwa kwa zamu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom