Foleni ya Mabatini Mwanza ni uzembe tu!

Foleni ya Mabatini Mwanza ni uzembe tu!

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,312
Wasaalam wakuu.
Naipongeza serekali kwa kujitahidi kutuwekea daraja la waenda kwa miguu mabatini_mwanza..
kutoka nata hadi mabatini foleni sasa imeisha kabla hata daraja kuzinduliwa imeisha shauri ya upana wa barabara na jitihada za trafiki.
Foleni sasa imeamia mabatini buzuruga na pale buzuruga ni uzembe tu kwani wahusika wengeweza kuhamisha kituo kimoja cha hiace wanaoenda Igoma zishushe hiace nje ya bus stand buzuruga na wanaoenda mecco washushe barinaba.
naomba mamlaka husika wachukue hatua sasa!
 
Mkuu jaribu kuwasiliana na Wenje atatue hizo kero si ndiyo mbunge wenu.
 
Jamani wakati mwingine tuwe tunatafiti kidogo mambo kabla ya kuandika,hapo buzuruga mkabala na lango la kutokea mabasi kuna kituo cha hiace kinajengwa na Nyanza Roadways
 
awamu ya pili ya upanuzi wa barabara utakaokamilisha kipande cha nata - buzuruga utamaliza tatizo la foleni ya iyo barabara ya musoma!
 
Usinganganie Wenje tu kwani Maria Hewa yeye si mbunge wa mza wa kuambiwa? Tumia akiri ya shuleni usitumie akili ya ccm.
Huyo mama Hewa kama naye anakaa Dar basi Mwanza hakuna wabunge mimi sipo hapa kutetea CCM.
 
Mimi nafikiri tofauti kabisa, foreni ya mabatini inatokana na uwepo wa njia moja inayoingia na kutoka mjini hali inayopelekea kuwapo na foleni muda wote.Anglia hata wakati wa mvua kubwa magari hulazimika kusimama kusubiria maji yakatike kutiririka barabarani.

SULUHISHO LA FOLENI:
serikali ifikirie kuifungua/kujenga barabara mbadala itokayo MABATINI kupitia NYAMBITI hadi NYASAKA to buzuruga hii itapelekea kufunguka kwa miundo mbinu mingi na foleni ya kuingia na kutoka mini kupungua kwa 90%. Lakini kinachoendelea mabatini nikama kutibu tatizo la homa kwa kutumia panado badala ya dawa mahususi kwa kutibu malaria.
 
ni kweli ila kwa serekali hii itachukua miaka 50 kutekeleza haya
 
ila wakuu kama kuna mtu anaishi mwanza atakubaliana na mimi Wenje naye ni mzembe pamba road imeshazibwa mashimo mara mbili kwa mwaka huu na sasa yale mashimo yamegeuka handaki na mbunge yupo na hasemi chochote
 
Mimi nafikiri tofauti kabisa, foreni ya mabatini inatokana na uwepo wa njia moja inayoingia na kutoka mjini hali inayopelekea kuwapo na foleni muda wote.Anglia hata wakati wa mvua kubwa magari hulazimika kusimama kusubiria maji yakatike kutiririka barabarani.

SULUHISHO LA FOLENI:
serikali ifikirie kuifungua/kujenga barabara mbadala itokayo MABATINI kupitia NYAMBITI hadi NYASAKA to buzuruga hii itapelekea kufunguka kwa miundo mbinu mingi na foleni ya kuingia na kutoka mini kupungua kwa 90%. Lakini kinachoendelea mabatini nikama kutibu tatizo la homa kwa kutumia panado badala ya dawa mahususi kwa kutibu malaria.

Barabara inayotakiwa kufunguliwa hapo ni ile ya nyakato mahina mpaka mkuyuni hapo watakua wamefanikiwa kupunguza magari kupita katikati ya mji.
 
Barabar zote kuingia mjini sasa ziwe ""double roads", asanteni

Hata pale Nyerere road kuanzia mnara ulioko Stanbic kuelekea jengo la CCM inatakiwa kupanuliwa. Kumbuka ni barabara ya upana wa mwaka tangu 1954! Leo kuna foleni ya kutisha.

Hapa solution pekee ni kubomoa hizo nyumba za wahidi na kuipanua Nyerere road. Vinginevyo, msidhani foleni ni huko tu wakati wa kuingia Mwanza, wakati kumbe hata katikati ya jiji ni uchuro.

Hebu ona ile barabara ya sokoni inayounganika na Pamba Road. Utapitaje pale na gari. Urefu wa mita 400 lakini ukiingia ni kama adhabu.

Tufikirieni yote haya.
 
Back
Top Bottom