Foleni ya Mabatini Mwanza ni uzembe tu!

Foleni ya Mabatini Mwanza ni uzembe tu!

Hata pale Nyerere road kuanzia mnara ulioko Stanbic kuelekea jengo la CCM inatakiwa kupanuliwa. Kumbuka ni barabara ya upana wa mwaka tangu 1954! Leo kuna foleni ya kutisha.

Hapa solution pekee ni kubomoa hizo nyumba za wahidi na kuipanua Nyerere road. Vinginevyo, msidhani foleni ni huko tu wakati wa kuingia Mwanza, wakati kumbe hata katikati ya jiji ni uchuro.

Hebu ona ile barabara ya sokoni inayounganika na Pamba Road. Utapitaje pale na gari. Urefu wa mita 400 lakini ukiingia ni kama adhabu.

Tufikirieni yote haya.

asivunje, wapanue mji na shughuli kuu zitawaywe ktk viungo vya mji
 
ule mpango wa kuondoa hiace na kutumia mabasi kama coaster uliishia wapi? au Kabwe kaondoka nao?
 
Halmashauri ya Jiji bado iko usingizini, watalu wa miaka ya 2000 wanabuni na kutengeneza barabara za miaka ya 1900! Barabara za Mwanza ni nyembamba sana, hazikidhi mahitaji ya matumizi ya barabara za karne hii. Zilijengwa wakati hakukuwa na pikipiki nyingi, hivyo walizingatia magari pekee.

Siku hizi pikipiki zimeongezeka sana hivyo one lane should accommodate motorcycle or Bajaji and one Vehicle, yaani zote ziende sambamba na kuwe na nafasi kidogo ya steering play.

Ningeona wataalamu wetu wana akili kama wangeweka viwango vipya vya barabara za Barabara kuu zinazoingia mijini, yaani ziwe zinapitisha magari manne na pikipiki mbili zinazokwenda sambamba na kutoka nje ya miji vivyo hivyo! Zile za mitaani ziwe na uwezo wa kupitisha gari na bajaji kila upande wa uelekeo na mita zingine nne nne kwa ajili ya parking. Makampuni ya Parking yajenge parking kila mtaa. Lakini kwa vile wataalamu wetu ni watu wa kukalili, ubongo umefika mwisho barabara ni nyembamba sana na hazina side parking.

Halmashauri ya Jiji la Mwanza sijui wana mkataba gani na Nyanza Road, wanawapa tenda zakujenga barabara za lami wakati hawana utaalamu huo. Angalia barabara ya Kona ya Bwiru via Kiseke-Buzuruga, ni nyembamba na imeanza kubomoka hata mwaka haijamaliza. Kama sikosei Nyanza Road walijenga barabara ya Mwaloni, Pamba, Lumumba na sasa Karuta. Zilijengwa lakini sasa hivi ni uchafu mtupu ukiondoa Karuta ambayo nayo haita maliza mwaka!

Nyanza Road ni wazuri kwa barabara za vumbi na si za lami. Jiji amkeni tokeni kwenye usingizi bora muwape wachina hizo za mjini. Mitaro nayo ijengewe mifuniko, siyo mjini mitaro mipana ina achwa wazi utafikiri ya highway, inaharibu mandhali ya Jiji.
 
Back
Top Bottom