Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,073
- 34,844
Hizi ni bendi mbili tofauti zinazopiga muziki wa dansi hapa nchini, ambazo kwa kiasi kikubwa zimejizolea umaarufu kutokana na umahiri wa tungo zao kiasi cha kuwapa wakati mgumu mashabiki kuamua nani mkali kuliko mwenzake katika tasnia ya burudani ya muziki wa dansi hapa nchini... Miongoni mwa masongi ambayo yameimbwa na Bendi hizi na kufanikiwa kuwateka mashabiki vilivyo, ni pamoja na Dunia kigeugeu wa Fm Academia a.k.a 'Wazee wa Ngwasuma' na Sifa kwa mwanamke, wimbo ulioipaisha sana bendi hiyo.
Kwa upande wa Akundo Impact a.k.a 'Wazee wa Masauti', wao wana nyimbo kama Yako wapi mapenzi , Mama Vanessa na Safari Siyo Kifo, huku wakitarajia kuachia albamu yao mpya iliyobatizwa jina la History no Change na ndani yake kukiwa na ngoma kama pongezi kwa wenye ndoa na Ubinafsi
Dondosha kura yako utuambie nani yuko juu zaidi kati ya bendi hizi mbili.