Flaviana Matata wewe si msaada kwa wanawake

Flaviana Matata wewe si msaada kwa wanawake

MIGUGO

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
2,137
Reaction score
3,942
Jana amezindua taulo za kike Hotel Hyatt Dar es salaam. Bei yake alitangaza ni shilingi 3, 000 ambayo binti masikini hawezi kugharamia.

Kama walivyo wanawake wengi maarufu wakijifanya kuwa mstari wa mbele kwenye kutetea jinsia ya kike. 3,000 ni kubwa sana maana mtaani kuna pedi (taulo za kike) ambazo wadogo zetu, wanetu, dada na ndugu wengine wananunua kwa 2,000 hata hii 2k bado ni kubwa kwao.

Atapewa tuzo "Sheroes" wakati hawana msaada kwa mtoto wa kike (girl child).

Feminism si kutweet kiharakati tu.

Hawa wanawake maarufu wanajifanya feminists wakati wao Misandrists tu ikichukia jinsia ya kiume.
Screenshot_20200714-162216_Instagram~2.jpeg
 
Ni kweli kaka, angeweza kuja na ped za 500 au 1000 walau! Hii 3000 ni kubwa sana kwa mabinti zetu, hivi ndoa yake iliishia wapi? Maana nasikia kulikua na mtafaruku mkubwa sana
 
Mkuu wewe mwambie demu wako anunue za bei anayomudu, mbona kuna condom za 65,000 kwa pakti moja na kuna za buku jero so the choice is yours usitake mtu afanye biashara ambayo haitampa faida.
 
Ni kweli kaka,angeweza kuja na ped za 500 au 1000 walau! Hii 3000 ni kubwa sana kwa mabinti zetu,hivi ndoa yake iliishia wapi? Maana nasikia kulikua na mtafaruku mkubwa sana

Utanipatia mrejesho.
 
Una uhakika kuwa hizi nyingine za hazina ubora kwa kulinganisha?
Nimeuliza maswali mawili,hujatoa jibu zaidi ya wewe kuniuliza swali. Uzi wako umeenda moja kwa moja katika kutoa lawama na kudhihaki juhudi alizofanya(kana kwamba unauhakikika pasi na shaka ya uzalishaji wa bidhaa hiyo)
 
Nimeweka mada hii kwa sababu yeye amekuwa mstari wa mbele kudai haki na kumsaidia mtoto wa kike.

Taulo za bure ni moja kati msaada mkubwa kwa wanawake kipindi chote chao cha ujana mpaka pale menopause. Kwa hiyo nilidhani ataqoute "bei rafiki" walau chini ya ile iliyozoeleka mtaani.
mkuu wewe mwambie demu wako anunue za bei anayomudu, mbona kuna condom za 65,000 kwa pakti moja na kuna za buku jero so the choice is yours usitake mtu afanye biashara ambayo haitampa faida.
 
Ni kweli kaka,angeweza kuja na ped za 500 au 1000 walau! Hii 3000 ni kubwa sana kwa mabinti zetu,hivi ndoa yake iliishia wapi? Maana nasikia kulikua na mtafaruku mkubwa sana
Mchangieni hela auze kwa hiyo bei 500 au 1000
 
Unataka nikujibu jibu unalolitegemea wewe lakini nimekujibu hivyo.
Nimeuliza maswali mawili,hujatoa jibu zaidi ya wewe kuniuliza swali. Uzi wako umeenda moja kwa moja katika kutoa lawama na kudhihaki juhudi alizofanya(kana kwamba unauhakikika pasi na shaka ya uzalishaji wa bidhaa hiyo)
 
Unataka nikujibu jibu unalolitegemea wewe lakini nimekujibu hivyo.
Swali ni jepesi.....''Unafahamu gharama aliyozalisha bidhaa mpaka kuingia sokoni?'' Ulitaka iuzwe chini ya sh.2000,kana kwamba unuhakika Unit cost ni chini ya hapo.

Bidhaa ndio kwanza imeingia sokoni,hata mrejesho wa ubora kujustify bei ni kubwa ama ni stahiki huna. Sitetei wala kupinga hiyo bei, lakini walau tunapotoa lawama ama kudhihaki juhudi za watu tuwe na hoja zenye mshiko.
 
Back
Top Bottom