Fixed account za benki na utajiri wa haraka haraka

Wana JF plan yangu ni kufungua deposit fixed account kiasi Kama cha 20m kwa mwaka mmoja, ni bank gani inatoa faida nzuri kwa asilimia ngapi?!
 
Ni rahisi kwenda kwenye benki mbalimbali na kupata viwango vyao vya faida. Mara nyingi pia huwa wanaviandika magazetini.
 
Wana JF plan yangu ni kufungua deposit fixed account kiasi Kama cha 20m kwa mwaka mmoja, ni bank gani inatoa faida nzuri kwa asilimia ngapi?!

seriously?! baada ya kuzungusha hio hela mwaka mzima unaenda kuweka mwaka mzima upate ka-interest tu?
 
Habari wana Jf
Naombeni kujuzwa juu ya utaratibu unaotumika katika kumpa faida mtu aliye fungua fixed account bank,Kwa maneno mengine kanuni inayotumika mfano mtu anayeweka laki tatu kila mwezi

Nawasilisha hoja
 
Inategemea ulipofungua hiyo fixed account ulikubali kulibwa interest rate asilimia ngapi na utaweka hela kwa mda gani.

Kwa mfano kama interest ni 8.5% na account yenye 100,000 ukaweka laki 3 kila mwezi mwisho wa mwaka utakuwa na 3,738,185.47 kwenye account. So faida ni kama 138,000 minus fees.

Unaweza kutumia hii calculator kukokotoa, jaza shilingi tu sio tatizo.
http://www.bankrate.com/calculators/savings/simple-savings-calculator.aspx?MSA=&MSA=&MSA=&MSA=&MSA=&MSA=
 
Naona CRDB wanatoa 6% interest kwa mwaka, na inflation Tanzania ni kama 6% so mwisho wa mwaka unakua kama umetoa draw tu.
 
Mi naombeni mnisaidie benki gani inatoa interest kubwa. So far najua i&m ndo inatoa 11% kwa mwaka
 
Ao I&M wanatoa iyo riba ya 11% kwa kianzio cha sh. Ngapi na kwa muda gan??kama ata ukiweka laki tano unapewa 11% itakuwa ni uongo
 
Mi nimeshaweka hapo i&m minimum amount ni laki moja na hiyo 11% ni per annum, miezi 6 ni 10% kama sijasahau
 
Umuofika kwenu wadau wa JF

Ninadunduliza vijisent vyangu ili ninunue kausafiri (Kaswift tu) mwaka huu mwishoni. Nimejaribu kutunza kwenye akaunt yangu, najikuta nalazimika kutoa kutoa kidogokidogo na kuzitumia pale nipatapo matatizo, hali mabayo inahatarisha uwezekano wa kufikia malengo yangu. Nafikiria kuzihifadhi mahali salama ambapo sitaweza kuzitoa lakini pia ziwe zinazalisha kafaida hata kama ni kidogo.

Nawaombeni mnijulishe ni benki gani ambayo nikitunza vipesa vyangu (havizidi 4milion) kwenye fixed account kwa muda wa miezi mitatu nitapata ka--riba kakubwa ukilinganisha na benk nyingine.

Natanguliza shukrani..
 
Kwa amount hyo....hutaona tofauti...benk nying zinatoa 7 au zaid% but kwa amount kubwa kubwa say angalau 10 mil kwenda mbele huko....mie nadhan kulinda thamani ya hela yako...nenda benki....( kwa maoni yangu crdb ni better) fungua akaunt ya mtoto ya usd ....then badilisha hela zako kuwa dola...nenda kaziweke mule kwenye account. Hii italinda thamani ya hela.yako....lakin pia siku unaitaka utauza dola zako kwa bei nzuri...ambayo itakuwa above faida ya riba ambayo ungepata
 
Back
Top Bottom