Fixed account za benki na utajiri wa haraka haraka

Kinakuwa na riba ambayo unatozwa tu Kwa muda uliokaa na hela na kiasi ulichotumia let's say 30 day,utachajiwa riba ya mda huo ......tofauti na term loan ambayl riba ni fixed per year na marejesho unapangiwa kila mwez
Ahsante sana wakuu
Inategemea na masharti ya benki, mara nyingine ni ukizidisha ule muda ambao ilipaswa urudishe ndio huwa unaweka na cha juu.
 
Je makato yake(gharama) yanakuwaje kila mwisho wa mwezi au pale nitakapokuja kutoa

Mkuu nimekuelewa ni benki gani mzuri wanahiyo account ya kuweka kila mwezi tu ila kutoa mpaka muda ufike ?
Kuweka kila mwezi hip ni saving account- kuna bank wanafungua saving accounts ambazo unaweza kuweka tu kutoa mpaka muda mliowekeana. ILA

Fixed account unafanya one single deposit. Mfano unaweka 10m kwa mwaka mmoja kwa riba ambayo inaanzia 6-8% kwa mwaka. N a pia napenda kukumbusha faida unayopata unatakiwa ilipia kpdi ya 10% (ya faida)-withholding tax upon maturity/ kuiva kwa fixed deposit yako

The good, the bad and the ugly.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba current acc unaweza kutoa pesa zaidi ya uliyonayo, kivipi sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ameshindwa kuelewa, current account.

Kutoa hela kuliko kiwango ulichonacho siyo current account hii inaitwa overdraft. Ni aina ya mkopo, na kwamba hautolewi kwa kila mtu, mpaka uwe mfanyabiashara ambae umedevelop trust na benki husika. Hawatoi kwa kila mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa benki zilizoimarika miezi mitatu 3% mwaka 6%to 11%.....Kwa benki zenye ukwasi mdogo sometimes hadi 15% per annum for 3 years eg.kuna mda access waliweka 13-15 kama sikumbuki vizuri

Kama huna matumizi ya maendeleo au uzalishaji Kwa hiyo hela ,weka.....kama unauzalishaji ingiza huko ,maaana unaweza pata 15-20% per annum above market rate ya fixed deposit accounts..

Kuanzia mil 100 ,bil 1 na zaidi hela ndio unaiona .

Kwa mil 2 sizani kama Kwa mwaka itazidi riba ya faida tsh . 200,000 ,says laki mbili.
Milion 2 labda upate 60000
 
Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’

Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki

‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi

‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika

Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini

Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie

Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali

Signed

Oedipus

kwa hiyo mzee nikiwa na kama kibillion hivi siwezi kukosa faida ya mil 100 kwa mwaka eeh?
na je kuna option ya kuweza kuwa nalipwa hiyo faida on monthly basis?
 
Unaonaje kama nikichukua mkopo WA benki mahali na kiasi kukitupa huko kama biashara? Kitaaluma inakuwaje hii.
Banks walishafikiria suala hilo mkuu.

Naweka mfano kwa 'urahisi' zaidi ili ieleweke:

Assume pesa husika ni Tsh.10mil umeikopa Bank X inayo charge riba ya 17% kwa mwaka then itakua:

10mil×17%=1.7mil

Riba itakua Tsh.1.7mil so mpk Mwaka unaisha utakua umewalipa Bank X Tsh.11,700,000

Assume umekopa hio hio 10mil hapo bank X na ukaenda kuiweka kwny Fixed deposit Bank Y kwa mwaka mzima ambapo Watakupa 10% kwa mwaka,hesabu itakua:

10mil×10%(1-0.1)=Tsh 900,000

Hio 0.1% iliyotelewa hapo juu ni 10% itakayolipwa Tra(Withholding Tax)

So mwisho wa mwakaBank Y itakupa 10,000,000+900,000=Tsh.10,900,000

So kama ulikopa hio pesa bank X na ukaenda kuiweka hio hio pesa kwny fixed a/c bank Y then utapata hasara ya 11.7mil-10.9mil=Tsh.800,000 kwa mwaka.

NOTE:point ya msingi ni SIKU ZOTE Riba ya Mkopo hua ni kubwa kuliko Riba ya kwenye Fixed a/c ili ku-encourage watu wakope na wakafanyie biashara pesa hizo na sio kukopa then wakaziweke kwny fixed a/c.
 
[
Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’

Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki

‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi

‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika

Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini

Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie

Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali

Signed

Oedipus

Hapa ameshindwa kuelewa, current account.

Kutoa hela kuliko kiwango ulichonacho siyo current account hii inaitwa overdraft. Ni aina ya mkopo, na kwamba hautolewi kwa kila mtu, mpaka uwe mfanyabiashara ambae umedevelop trust na benki husika. Hawatoi kwa kila mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapana, wewe ndiyo hujamwelewa vizuri alichosema. Amesema kwamba, ukiwa na current account, unaruhusiwa kufanya overdraft, hajasema kuwa current account ni overdraft, kama unavyodai wewe hapa. Unanipa wasiwasi kama bado uko shule au chuo, unaweza kuwa una tabia ya kutunga swali lako kwenye mtihani, linaloshahibiana na swali ulilouliulizwa, lakini ambalo ni tofauti na swali uliloulizwa
 
kwa hiyo mzee nikiwa na kama kibillion hivi siwezi kukosa faida ya mil 100 kwa mwaka eeh?
na je kuna option ya kuweza kuwa nalipwa hiyo faida on monthly basis?
Hata kama ikitoa riba kwa mwezi bado wewe hautaweza kutoa hela hadi muda utimie
 
Hata kama ikitoa riba kwa mwezi bado wewe hautaweza kutoa hela hadi muda utimie

mie shida yangu sio kutoa ile hela mie nachotaka ni kuwa na uhakika wa kupata pesa kila mwezi na sio kusubiria mpaka mwisho wa mwaka ndio nipewe hiyo faida.
 
Kwamba current acc unaweza kutoa pesa zaidi ya uliyonayo, kivipi sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni kwa CRDB
2020-04-15.png
 
Wakat nko level flan ya elimu nkaanza kujifanya niwe investa. Nkaingia zangu nmb nkafngua hyo fixed nkaweka 50000(elfu hamsini) kwanza zen next time nweke mzigo mkubwa.. nlivunjika moyo coz afta 3 months ndo nkaruhusia kutoa na kkuta faida yangu 2500(elfu mbili na mia tano). Naona vijana twauliziiia hyo fixed.. cha muhm kujua n kwamba mzigo mkubwaaaaa utakupa faida ya ela ya kula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom