Fixed account za benki na utajiri wa haraka haraka

Hiyo fixed account mimi naitaka.

Nataka kufungua niweke kiasi cha pesa kila mwezi baada ya miezi 12 ndo nataka kuitoa.

Je hakuna pesa ambayo nitakatwa kama malipo ya kuwalipa kunitunzia pesa ?

Je ikitokea kuna tatizo nikahitaji kutoa pesa kwa muda usiokuwa nimeandika inakuwaje ?

Na je inawezekana nikawaambia benki husika wanikate kwenye mshahara moja kwa moja pale unapoingia uende kwenye fixed account ?

Nijibu hayo niendelee maana ninaitaka hyo fixed account.

Sent using Jamii Forums mobile app
iyo Sio fixed sasa fixed ni mara moja na inakua annual
 
Vipi wakati wa kurejesha kile kiasi ulichozidisha kukitoa kunakuwa na Riba?
Kiasi ulicho utilise/tumia kinakatwa riba kila mwezi mpaka utakapo reqularies account. Hii ni nzuri kwa suppliers/ contractors ambao hawana daily au monthly sales.

The good, the bad and the ugly.
 
Mara nyingi hii ni kwa ajili ya wafanyabishara wakubwa mfano Mo au Bakhressa pia kampuni na co kwa customers wa kawaida
Shukrani mkuu

Kiasi ulicho utilise/tumia kinakatwa riba kila mwezi mpaka utakapo reqularies account. Hii ni nzuri kwa suppliers/ contractors ambao hawana daily au monthly sales.

The good, the bad and the ugly.
Ahsante sana chief hapa sasa umenijibu vyema
 
Hiyo fixed account mimi naitaka.

Nataka kufungua niweke kiasi cha pesa kila mwezi baada ya miezi 12 ndo nataka kuitoa.

Je hakuna pesa ambayo nitakatwa kama malipo ya kuwalipa kunitunzia pesa ?

Je ikitokea kuna tatizo nikahitaji kutoa pesa kwa muda usiokuwa nimeandika inakuwaje ?

Na je inawezekana nikawaambia benki husika wanikate kwenye mshahara moja kwa moja pale unapoingia uende kwenye fixed account ?

Nijibu hayo niendelee maana ninaitaka hyo fixed account.

Sent using Jamii Forums mobile app
Utaratibu huo haupo kwenye fixed account, unachokitaka wewe kinawezekana WADU, tena kule unaweza kuwa unadeposit moja kwa moja kwa kukatwa toka kwenye mshahara. Nenda bank ya Posta utapewa ufafanuzi na kufunguliwa account.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nataka niweke milioni 2 fixed deposit. Faida sh ngapi
Kwa benki zilizoimarika miezi mitatu 3% mwaka 6%to 11%.....Kwa benki zenye ukwasi mdogo sometimes hadi 15% per annum for 3 years eg.kuna mda access waliweka 13-15 kama sikumbuki vizuri

Kama huna matumizi ya maendeleo au uzalishaji Kwa hiyo hela ,weka.....kama unauzalishaji ingiza huko ,maaana unaweza pata 15-20% per annum above market rate ya fixed deposit accounts..

Kuanzia mil 100 ,bil 1 na zaidi hela ndio unaiona .

Kwa mil 2 sizani kama Kwa mwaka itazidi riba ya faida tsh . 200,000 ,says laki mbili.
 
Vipi wakati wa kurejesha kile kiasi ulichozidisha kukitoa kunakuwa na Riba?
Kinakuwa na riba ambayo unatozwa tu Kwa muda uliokaa na hela na kiasi ulichotumia let's say 30 day,utachajiwa riba ya mda huo ......tofauti na term loan ambayl riba ni fixed per year na marejesho unapangiwa kila mwez
 
Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’

Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki

‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi

‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika

Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini

Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie

Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali

Signed

Oedipus
naona umetoka kusoma kitabu chako cha bool keeping cha form 2 eeeh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo fixed account mimi naitaka.

Nataka kufungua niweke kiasi cha pesa kila mwezi baada ya miezi 12 ndo nataka kuitoa.

Je hakuna pesa ambayo nitakatwa kama malipo ya kuwalipa kunitunzia pesa ?

Je ikitokea kuna tatizo nikahitaji kutoa pesa kwa muda usiokuwa nimeandika inakuwaje ?

Na je inawezekana nikawaambia benki husika wanikate kwenye mshahara moja kwa moja pale unapoingia uende kwenye fixed account ?

Nijibu hayo niendelee maana ninaitaka hyo fixed account.

Sent using Jamii Forums mobile app
Najua kiasi cha kuvuna ni makubaliano baina ya benki na customer, je kwa uzoefu wako tu ukiweka fixed Tshs 500k ni kiasi gn unaweza kuvuna kwa muda wa miezi mi3?
Elfu Moja miatano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Riba inayotolewa na mabank kwenye mikopo ni kubwa sana kuliko wanaotoa wao kwenye fixed deposits na mwisho wa siku faida unayopata inakatwa kodi....hio ni hasara kwako.

The good, the bad and the ugly.
Ndugu, kwenye masuala yote kodi zinakatwa, iwe ni hisa, dhamana za serikali, fixed account nk, wanakata 10% ya added value.

Kama ongezeko lao ni 1000 basi wataondoka na shilingi 100.

Hili swala lipo kila sehemu hata ukinunua vitu kwenye mnada wa TRA
 
Vipi wakati wa kurejesha kile kiasi ulichozidisha kukitoa kunakuwa na Riba?
Inategemea na masharti ya benki, mara nyingine ni ukizidisha ule muda ambao ilipaswa urudishe ndio huwa unaweka na cha juu.
 
Back
Top Bottom