Fix za town

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,549
Mpo poa masela ?
Ziro Matamaa ni mshikaji wetu anayekaa mtaa wa Uchafu, ni mtaa unaopatikana pande za mabondeni.

Jamaa ni msela mwenye mbwembwe na mikogo kibao. Huwa anakuja kupiga stori kwenye kijiwe chetu cha mabishoo.Baada ya kutuzoea watoto wa kishua akaanza kuazima pamba zetu za kibishoo ili iwe nahisi kuwapata mashori wa kijanja, basi Ziro akawa kila akipata demu mkali anamdanganya kwao na kumleta kwenye magneto yetu ya kijanja.

Mwaka juzi baada ya msela Ziro kuchemsha mtihani wa kumaliza O level akaamua kutimkia bondeni kwa mzee Madiba(Sauzi) kisha tukawa tunasikia tu stories zake kitaa kwamba jamaa mambo safi. Baada ya miezi 7 alarejea Joto City(Bongo) akiwa na vikorokoro kibao, pamba kali,simu kubwa kama site mirror ya Fuso ,kuvaa cheni kubwa kama mnyororo wa mbwa pia alitoga sikio na kuvaa hereni, hakuishia hapo tu bali alisuka na nywele!

Ujio wa Ziro ulifanya kijiwe chetu kisiwe na amani kabisa! Jamaa akaanza dharau akawa kila akipita kitaa anasalimia"mambo zenu watoto wa mama?" Duh tulimkoma jamaa kwani aliamua kutuchapia hadi mademu zetu!! Tukawa wapole tu.Baada ya miezi 3 Ziro Matamaa akarudi bondeni na kufanya kijiwe chetu kiwe fresh.

Sasa mwaka jana mwishoni Ziro karudi tena Joto City, jamaa ka
fulia kinoma na kuanza kutupiga mizinga na kutuomba pamba zetu ili apige tunampotezea tu.tukimuuliza utarudi lini Sauzi anatupiga kamba eti bado kuna machafuko! Kibaya zaidi kakuta kibanda chao (nyumba) imepigwa X na vijana wa Mzee Hapa Kazi Tu!!! Na huku kitaa siku hizi tunamchapia tu mademu zake hahahahaaaaa......

***Turn on ur swagga !***

Superstar wa kitaa
The Bitoz
 
wewe ni boya tena kiazi hilo ni tatizo la jf ngoja wakirekebisha utaona like zio ngapi Invisible naomba urekebishe hizo like naona huku huyu dogo analeta dharau
Heri mimi boya kuliko ww andazi na lodilofa...wakirekebisha kwa wote hizo likes bado utaburuza mkia tu ...kalale
Hahahaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom