Five stars modern taarab wapata pigo!!

Zero One Two

JF-Expert Member
Sep 16, 2007
9,347
3,023
Ajali iliyotokea jana maeneo ya mikumi mkoani morogoro wakitokea kyela katika maonesho yao imesababisha vifo vya wasanii wa kundi mahiri la 5 stars wapatao kumi na tatu akiwamo Issa kijoti aliyeimba wimbo maarufu kama ''kanunua simu kampa demu walipoachana kampokonya''huku wengine kumi na tatu wakiwa majeruhi akiwamo bi Mwanahawa Ally wanaendea vizuri. POLENI WAPENZI WOTE
WA TAARABU.MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI .AMINA
 
Kikundi cha taarabu cha Five Stars kimepata pigo baada ya kufiwa na jumla ya wanakikundi 10,
wakiwemo waimbaji, mafundi mitambo na mkurugenzi wa bendi. Katika ajali ya gari iliyotokea usiku
wa kuamkia leo Mikumi, Mkoani Morogoro, wakitokea Kyela,Mbeya ambako walikuwa na ziara ya
kimuziki. Katika ajali hiyo, alikuwemo pia mwimbaji mkongwe Mwanahawa Ally ambaye alinusurika
baada ya kuumia vibaya, aliungana nao kama mwimbaji mwalikwa akitokea Melody ModernTaarab. Pia
mwanamuziki mwingine mahiri, Hammer Q, ambaye alikuwepo kwenye msafara, alinusurika baada ya
kubaki Iringa wakati wenzake wakiendelea na safari. . Yafutayo ni majina ya wana Five Stars waliothibitishwa kufa hadi sasa:

Issa kijoti - mwimbaji
Husna mapande-mwimbaji
nasoro madenge - mkurugenzi
Sheba juma - mpiga solo
Omari hashimu- mpiga bass
Omari tall- fundi mitambo
Hamisa mussa - mwimbaji
Rama kinyoya - mwimbaji
Tizo mgunda - mcheza shoo
Haji mzaniwa - fundi mitambo
 
Maskiniiiiii kijotiiiiiiiii!!! Mungu azilaze roho zao peponi ameeeeeeeeeeeeen!!!!
 
Madereva punguzeni usela mavi mkiwa safarini, sasa munaon mr ajali moro2.JPG a mulivyo licost Taifa na wapenzi wa muziki kwa ujumla?
Nasasa kama Dreva huyu ange sikiliza ushauri wa Abiria wake Ajali isingetokea kamwe.

moroajali moro3.JPG
 
wadau kuna picha nimeambiwa zilikuwa kwenye global publishers na leo hazipo kuna yyte aliweza kudownload atushirikishe ???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom