Five Star Hotel

Mpilipili

Member
Nov 17, 2011
28
12
Kwa mnaofahamu au pengine mna exposure katika nchi za wenzetu, hivi tunaposema Hotel hii ni ya nyota 5 maana yake ni nini? Mfano nikijenga Hotel yangu sehemu nzuri tu tuseme kwenye prime area, hotel nzuri na kubwa naweza kuibuka tu na kuita ni hotel ya nyota 5 au kuna viwango vya kuzingatia! Sielewi naomba vigezo au criteria zinazotakiwa hadi Hotel iwe na hadhi ya kuwa FIVE STAR
 
Nkamba uko sahihi bt ukimkuta mtu anaoga chooni na bafu lipo mayb yuko na stress! So far unamtoa chooni kisha humuoneshi bafu there4 akaoge wp? Muelekeze jukwaa ikibidi umtiririshie mapembuzi ya 5 star sisi wengine vwango vye2 ni kwenye "guest bubu" na zile "sisi kw sisi guest house"
 
na sio kila kitu uulize kaka,huwezi kufanya hata research on your own ukapata majibu,mbona unaonekana kama unajua kutumia internet,cant u do that!
 
Kwa mnaofahamu au pengine mna exposure katika nchi za wenzetu, hivi tunaposema Hotel hii ni ya nyota 5 maana yake ni nini? Mfano nikijenga Hotel yangu sehemu nzuri tu tuseme kwenye prime area, hotel nzuri na kubwa naweza kuibuka tu na kuita ni hotel ya nyota 5 au kuna viwango vya kuzingatia! Sielewi naomba vigezo au criteria zinazotakiwa hadi Hotel iwe na hadhi ya kuwa FIVE STAR

Mkuu

Mkuu hii yote ni kwa ajili ya kumlinda mteja na kuhakikisha kwamba mwenye hoteli hawaibii watu

Hii inatofautiana kati ya taifa na taifa hali kadhalika na makampuni, Hotel rating system iko hivi, ni vigezo ambavyo mwenye hoteli anatakiwa avifuate, kiafrica zaidi Nchi inatakiwa iwe na hotel rating agency, hizi zinatakiwa zitengeneze vigezo vitakavyotofautisha hoteli na hoteli, moja ya masharti yanaangalia hoteli imejengwa wapi,aina ya jengo, ukuwa wa mapokezi,vyumba na huduma nyingine,pia wanaangalia kama hoteli inatoa huduma kwa makundi maalumu katika jamii kama, walemavu, je mlemavu akienda anaweza fikia reception,chumbani bafu bila matatizo? pia wanaaangalia pia aina ya wafanyakazi kama wanaweza kuwasiliana kwa lugha ngapi za kimataifa,aina ya vitanda vinavyotumiwa, vijiko, sahani nk. Vigezo vipo vingi sasa Rating agency wakishapitia na kukagua kila kitu ndio wanaitangaza hoteli kama imefikia vigezo wa Five star au 4 star, 3 star nk


HALi HALISI kwa tanzania


Kwa Tanganyika hatuna Hotel Rating Agency, japo wizara ya utalii walijitahidi kutengeneza vigezo wakatembelea baadhii ya hotel, cha kusikitisha hoteli zilizoweza kufikia vigezo ni chache sana kwani nyingi zinazojiita 4 na 3 star hazina vigezo kabisa, pia wizara ilikuwa haina pesa na upungufu mkubwa wa wataalam, na hata kufanya hivyo walipata msukumo kutoka kenya na Uganda ambao wao wanazo hivi vitu miaka mingi iliyopita ( Kumbuka tuko nyuma k wa kila kitu)

HALI HALISI

Mahoteli yaliyopo sasa tanzania yanajipa hadhi yenyewe kutokana na matakwa ya mmiliki au mwendeshaji, haya ya kimataifa kama, Hiliday Inn, wao wako tofauti kidogo kwani ni chain hoteli zinazofuata set stardard hata zile amabzo zimeuza jina aliyeuziwa laima afuate stardard za mwenye jina. Hizi nyingine kwakuwa serekali imelala wanajitangazia tu ni 4 star lakini kiuhalisia huduma wanazotoa hailingani kabisa na hoteli yenye Nyoya 4


NINI cha Kufanyika


Wizara ya Maliasili na utalii inatakiwa ianzishe Hotel rating agency, waajiri, nakusomesha wataalamu ambao watatengeneza vigezo na wawezeshwe ili waweze kutembelea haya mahoteli na kutangazia umma kama ye metimiza vigezo, Hii itasaidiakuzuia wizi unaofanyika sasa kwani hoteli zinacharge garama kubwa ili hali huduma wanayotoa hailingani na pesa wanazotozwa wateja

kama hujaridhika waweza uliza zaidi
wasalaam
 
Ki ufupi kila nchi ina vigezo vya mahoteli katika nyota hizo 1 mpaka 5.ni vyema kuulizia wizara ya utalii ili upate msaada mzuri zaidi
 
Back
Top Bottom