Fitness and wellness

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
10,637
21,050
Salam,

Kama title inavyojieleza huu uzi utakuwa wa kuelimishana na kushauriana juu ya fitness and healthy living. I'll put my two cents in naamini wadau wataendeleza ili watu wenye goals tofauti tofauti waweze kupata kitu.

Goal kuu la watu walio wengi ni kupunguza uzito (weight loss) lakini pia wapo wanaotaka kujenga mwili (bodybuilding), wapo wanaotaka kupunguza kitambi tu (burning bellyfat) nk. Wote wataguswa katika uzi huu

Aidha tutajadili meal plans, supplements, mazoezi, apps & gadgets za kukusaidia katika safari ya healthy living.

Kwa ufupi formula mama ya healthy lifestyle ni Eat clean train dirty.

Kupunguza uzito (weight loss)

Cardio exercises kama running, jogging, swimming, biking, soccer ni mazoezi mazuri sana katika kusaidia kupunguza uzito na kuondoa kitambi. Aidha weightlifting ni bora zaidi kwa weight loss kuliko hata cardio. Mtu afanyae weightlifting zaidi na cardio kidogo atakuwa in good shape haraka kuliko yule anaefanya cardio pekee. Kwa wale wanaoweza kwenda gym ningeshauri katika saa moja unalotumia gym fanya weightlifting for 45mins na dakika 15 za mwisho fanya cardio. Kwa wale wasioenda gym ni sawa pia unaweza kufanya mazoezi nyumbani kama push ups, pull ups na kukimbia nje kidogo.

Kama goal lako ni kupunguza uzito inabidi uzingatie vitu unavyokula. Vyakula vyenye mafuta na sukari kama chips, soda inabidi upunguze sana. Binafsi sio muumini wa "usile kabisa chips" ila inabidi upunguze sana na vyakula vingine vyote vyenye sukari na mafuta bila kusahau maziwa. Maziwa yana fat kubwa inabidi kuyaacha au kunywa maziwa yenye less fat kama 2% milk au alternatives za maziwa kama almond milk, soy milk, cashew milk. Veggies na matunda inabidi viongezeke katika diet yako huku kiasi cha chakula kikipungua ili uweze kufikia goal lako. Usisahau kunywa maji ya kutosha

Bodybuilding

Bodybuilding is life. Weightlifting ni dawa mujarabu ya kuongeza au kupunguza mwili inategemeana na goal lako. Ninaposema bodybuilding siongelei wale watu wakubwa naongelea watu wa kawaida tu wanaofanya bodybuilding kujiweka sawa mfano mzuri msanii Dayamondi.

Kwa kufanya weightlifting unaweza ku-target part ya mwili na kuifanya iwe defined zaidi kama biceps, triceps, back, shoulders, chest, calves, quads, booty etc. Weightlifting ina burn more calories hivyo kwa mtu ambaye anataka kupungua basi hii ndiyo njia bora na kwa yule anayetaka kuongezeka na kuwa in shape basi itabidi ale zaidi ila vyakula vyenye kujenga mwili.

Mazoezi kama kitu kingine chochote yanahitaji nidhamu na uvumilivu wa hali ya juu siyo kwamba utabadilika overnight. Nigeshauri mtu afanye mazoezi at least siku 4 za week na kama ukiweza kufanya 5 basi more power to you ila isiwe siku zote saba sababu mwili unahitaji muda wa kurecover. Speed ya maendeleo yako itategemea na juhudi zako ila kwahakika yataka uvumilivu. Faida za mazoezi kila mtu anazijua sihitaji kuzijadili ukiachilia mbali ile ya kuonekana sexy mbele ya kioo :)

Supplements

Binafsi naamini katika supplements tatu tu; whey protein, fish oil na multivitamins. Haijalishi goli lako ni nini unahitaji protein ya kutosha kila siku, ni vyema kama utakula vyakula vyenye protein ya kutosha kila siku kama mayai, kuku, nyama, samaki, maziwa(bodybuilders) nk. Kama hupati protein ya kutosha basi protein supp inaweza kuwa ya msaada kwako zaidi whey protein ina amino acids kwa kiwango kikubwa ambazo zinahitajika sana katika recovering process. Fish oil ni mafuta ya samaki nayo ni muhimu sana kama unadhani huli sea foods kwa kiwango cha kutosha basi si mbaya ukatumia, pia fish oil huboresha ngozi na nywele. Multivitamins ni mchanganyiko wa vitamins mbali mbali ambazo zote zipo katika vyakula ila hizi ni extra push kwa wale ambao hawapati za kutosha kwenye mlo wa kila siku. Kama unakula vizuri veggies, matunda, samaki, nyama, kuku, mayai nk sio lazima kutumia supplements. Usisahau kunywa maji ya kutosha kila siku

Apps&gadgets

Ni ulimwengu wa technology sio basi kuna gadgets zipo ili kukusaidia katika safari yako ya fitness and wellness. Pedometer ni kifaa kinachohesabu steps zako pindi ukimbiapo na kukujulisha umekimbia umbali gani kwa muga gani na heart rate. Kumekuwepo na malalamiko kuhusu accuracy ya pedometer nyingi

App kama Fitness Buddy unaweza ipata bure play store inatoa muongozo wa jinsi ya kufanya mazoezi mbali mbali. Ni nzuri na rahisi sana kutumia

Pages

Kuna hizi pages Instagram za trainers na watu wengine wa kawaida tu ila wanatoa motisha na kuonyesha jinsi yakufanya mazoezi mbali mbali si mbaya kama ukazipitia pia; DoviesFitness Worldwide (@doviesfitness) • Instagram photos and videos ,
TanzaniaStreetsWorkouts (@tanzaniastreetsworkouts) • Instagram photos and videos ,
Marco Online Fitness Coach (@runandlift) • Instagram photos and videos ,
@workoutroutine • Instagram photos and videos ,
FitnessBunnie (@sbahle_mpisane) • Instagram photos and videos

Nakaribisha nyongeza, ushauri, maswali. Good luck

12080672_838772892910065_199355106_n.jpg
14240690_1755968737990104_1449095845_n.jpg
CFW+496+-+Version+2-1813262764-O.jpg
Charter-Fitness.jpg
12080672_838772892910065_199355106_n.jpg
 
na bia je natakiwa kuiacha?
Kuwa na mwili kama wa huyo mwanadada wengi wao huwa na nidhamu ya hali ya juu linapokuja suala la nini kiingie tumboni...Si ajabu ukaambiwa ni vegan..
Ni bora kama ukiacha kabisa,ama ukapunguza kwa kiwango kikubwa..
 
Kuwa na mwili kama wa huyo mwanadada wengi wao huwa na nidhamu ya hali ya juu linapokuja suala la nini kiingie tumboni...Si ajabu ukaambiwa ni vegan..
Ni bora kama ukiacha kabisa,ama ukapunguza kwa kiwango kikubwa..
siyo mnywaji kivile....na vichupa viwili vya Heineken ama nikizidisha vitatu.....au wine glass moja basi.
 
This is what's up.

For some of us, physical fitness is our lifestyle.

To say I'm a gym denizen is an understatement.

Workout warrior is my alter ego.

I love everything about working out.

I also think I'm a glutton for pain because I do enjoy the DOMS that ensues after a serious workout.

Those biceps curls, them bench presses, shoulder shrugs, lat pull-downs, squats, etc., I love them all.

Great thread. I plan to be a regular.
 
Mimi nina 175cm nina kg 76 natamani sana kupungua nifike 70 ila inashindikana, nakula mara moja kwa siku mchana na usiku nakula matunda au greens, sinywi bia huwa natumia pombe kali ila mara moja moja, inshort kwenye kula nina nidhamu, kukimbia nashindwa sababu nakosa company, mwili wangu ni mwepesi yaani sijaludhikana nyama wala sina tumbo mpaka sometimes nawaza labda ni u-giant maana baba yangu na mama wote ni warefu. Msaada tafadhali.
 
Mimi nina 175cm nina kg 76 natamani sana kupungua nifike 70 ila inashindikana,

Nasadiki wewe ni mdada, sio?

Kwa urefu wako huo wa 5'7 na hizo kilo zako, bila ya kukuona na kujua genetic body type yako, naweza kuhisi huenda uko overweight kidogo.

Nadhani kilo 68-70 ndo ideal weight yako

nakula mara moja kwa siku mchana na usiku nakula matunda au greens, sinywi bia huwa natumia pombe kali ila mara moja moja, inshort kwenye kula nina nidhamu,

Unakula vyakula gani hasa? Kiti moto, chipsi, mishikaki?

Soda na juisi unakunywa?

Caloric output na input yako ikoje? Unai-monitor?

Unazijua calories unazokula kila siku?

kukimbia nashindwa sababu nakosa company, mwili wangu ni mwepesi yaani sijaludhikana nyama wala sina tumbo mpaka sometimes nawaza labda ni u-giant maana baba yangu na mama wote ni warefu. Msaada tafadhali.

Naona huna self-motivation. Kwa watu wengi hili ndo tatizo kubwa ambalo huwa naliona.

Kwa sie wengine self-motivation si ishu kabisa.

Kwako naona hiyo ndo inaweza kuwa changamoto iliyo kikwazo cha wewe kufikia uzito unaotaka kuufikia.

Unaweza kubadilika kwenye hilo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom