Paedocypris: huyu ni samaki mkubwa tu katika jamii yao, wala sio dagaa. Anashikilia rekodi ya samaki mdogo duniani. Kwenye picha hiyo; huyo kakomaa kabisa kuendeleza kizazi chao
Katika pande mbili za mazingira ya bahari ; Kutisha na kuvutia. Hili ni eneo samaki wengi wasio tishio kwa samaki wengine na kwa binadamu ndio makazi yao. Hapa kauli mbiu yao ni AMANI ITAWALE KWA WOTE
View attachment 2101794
Viumbe unicorn pekee waliobaki katika ukanda wa bahari. Wanakaa deep water huko na kipindi barafu zinapo yeyoka kuko south pole wanaenda mapumzikoni huko
Paedocypris: huyu ni samaki mkubwa tu katika jamii yao, wala sio dagaa. Anashikilia rekodi ya samaki mdogo duniani. Kwenye picha hiyo; huyo kakomaa kabisa kuendeleza kizazi chao View attachment 2101806
Ribbon eel; hawa ni jamii ya wale hatari ingawa hawa sio hatari na wanafugwa kwa baadhi ya watu. Mara nyingi hujifungua mdomo pale waonapo tishio ili aonekane hatari ila kiuhalisia ni tofauti.
Nguva/mermaid?? Hapana! Wenzetu walimpa jina la Dogong. Huyu ni mnyama kabisa 100% anaishi kwa kula majani yanayojiotea huko chini ya bahari. Wanyama hawa wanapatikana pia katika maji baridi mfano ziwani. Ni kati ya viumbe vilivyo katika hatari kubwa ya kupotea duniani.
Amini ya kwamba dogong ni wana kama kaundugu na wenzao wa nchi kavu, Tembo.
Kulingana na FISHBASE, mpaka mwezi wa tisa 2020; jamii za samaki waliotambulika ni takriban 34,300 huku ikihofiwa kuna idadi kubwa za jamii hazijajulikana bado.