Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,184
- 44,015
Kama vile samaki anavyohitaji maji ili aishi vivyo hivyo fisadi huitaji
ufisadi ili aishi na kufanikiwa. Kumtoa fisadi kutoka ufisadi ni sawa na
kumtoa samaki kwenye maji ukidhania unamuokoa. Lakini samaki huvuliwa ili kugeuzwa mlo na siyo mapambo!
Wapo wengine hufanya uvuvi kama mchezo; wenyewe wanaita sport fishing ambapo samaki hutolewa kwenye maji, anaachwa anatapatapa halafu anarudishwa majini kuendelea kuishi. Ukiniuliza mimi hivi ndivyo ninavyoona mchezo wa CCM na ufisadi - Sport Corruption.. ambapo mafisadi huchezewa chezewa, hupewa chambo, hunaswa na kutolewa majini na watu wanashangilia. Lakini kabla hawajafa kwa kukosa oksijeni hurudishwa majini ambapo huruka ruka kwa furaha huku wananchi wakisubiri waone nani mwingine atavuliwa.
Kumbe hatuhitaji wavuvi wa michezo tunataka wale wenye kuvua samaki ili kuwageuza kitoweo. Hawa wanafuata kanuni asili ya mababu kuwa "usivue samaki ambaye hutaki kumla" (msiniulize mababu walisema lini hilo).
Tunahitaji viongozi wapya ambao hawatakuwa na muda wa mchezo na mafisadi bali watawakaanga na kuwageuza geuza katika jungu kuu la sheria huku mafuta ya ushahidi yakizidi kumiminwa juu yao.

Mkuu hii ya samaki ina mantiki kali sana na nadhani unahitaji kuipa sura zaidi maanake kila napotazama TV kipindi cha sports fishing hucheka sana wanapoibua bonge la samaki wakapiga picha nalo, wakaonyesha meno yake na rangi zake kisha jinsi ndoana ilivyoweza kushika (TAKUKURU) na kadhalika.
Lakini maajabu ya Mungu samaki huyo hurudishwa majini! halafu wao wakapongezana sana kwa jinsi kazi ilivyokuwa kubwa kumvua samaki huyo!.
Hapo hapo majuzi tu nimeona kisha cha Nyangumi mmoja akirukia mashua na kuipindua majini, ikawa habari kubwa na kkutangaza jinsi samaki huyo anavyoweza kuwa hatari. Na hakika sijawahi kuona wavuvi wa sports fishing wakivua Nyangumi kwa mchezo huo huo maanake ni hatari kwa usalama wao... ooooh! nimekosea sio usalama wao ila ni Usalama wa mashua (Taifa).
Tunakushukuru wewe kwani pasipo mawazo ya mtazamo wa samaki sisi wengine tungeelea kununua sokoni na vijiweni wale waliokwisha kaangwa na kutiwa chunvi na ndimu. Nafikiri hapo pia umenipata..Aisee nimecheka saaana hujui tu.. yaani na hilo ulilolisema itabidi niiendeleze kidogo sikuwa nimeifikiria sana lakini mawazo yenu hapa yamenipa mwanga zaidi.. thanks!