Fisadi kaitwa shujaa kwao:Nyerere na moringe tuwaiteje

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
wanaJF nimepatwa na kizunguzungu cha kufa mtu,baada ya kuona watanzania wenye akili timamu wanampokea mtuhumiwa wa ufisadi Lowassa wakiwa na fulana zenye maandishi "karibu lowassa,shujaa wetu".Nikajiuliza huyu mtu ni shujaa kwa misingi ipi? Kwa ufisadi wa kuliingiza taifa hasara? Kwa kuwajibika kutokana na makosa ya watendaji wake,kama anavyotaka tuamini? Nikajiuliza pia,Mashujaa wetu Mwl.Nyerere,Moringe na wale wote walioliletea taifa hili heshima tuwaweke wapi? WanaJF,napatwa na wasi wasi wa matumizi ya hili neno la SHUJAA,TUSAIDIANE KWA HILI
 
AS I SAID BEFORE, HAWA WATU WALINUNULIWA NA WAPAMBE AMBAO WALIFAIDIKA WAKATI AKIWA PM JAMANI. HUU NI MCHEZO MCHAFU IN OTHER LANGUAGE, FULANA UNAZOZUNGUMZIA ZILITOLEWA FREE OF CHARGE(F.O.C) NA KIWANDA FULANI CHA NDUGU ZETU WA KI ASIA. AMBACHO PIA NASIKIA KINA JIKOMBA KWAKE PIA KUMSAIDIA EL KUMALIZIA SHULE YAKE HUKO JIMBONI PIA. HII HABARI NIMEISIKIA JUU JUU BADO NATAFUTA FACTS. KUHUSU HII SHULE KWA VILE NI WENGI WALIKUWA WANALAZIMISHWA KUPELEKA MATERIAL SITE ALIPOKUWA PM.

SAA YA UKOMBOZI NI SASA
 
..hao waliompokea kwa heshima zote ni wananchi wa Monduli. kuna uwezekano alikuwa ni mtu wa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo lake la uchaguzi.

..kwamba Lowassa ni fisadi ktk masuala ya kitaifa[richmond,dowans,...] haimaanishi kwamba hakuwa na msaada wowote ule kwa maendeleo[shule za sekondari za bweni,visima vya maji,majosho...] ya wana monduli.

..kwamba Lowassa ni fisadi ktk masuala ya kitaifa haimaanishi kwamba hakuwa mwema ndani ya nyumba yake. si mliona mkewe analia pale bungeni? pia haimaanishi kuwa hakuwa makini ktk malezi ya wanawe. si mliona binti yake amehitimu Muhimbili?

..kuna tofauti kati ya LOCAL na NATIONAL politics.

..Tanzania ni kama tuna laana vile. Ukichunguza majimbo wanakotoka viongozi waadilifu utakuta yako choka mbaya. Ukienda kwa viongozi mafisadi utakuta huko kuna ahueni. Kwanini?
 
Wamonduli kama Wamonduli wana haki kumpokea maana ni mtoto, kaka, baba nk. hilo lisitusumbue, Mwano akiua/akibaka/akiiba akitoka jera huna budi kumpokea. EL yeye amepata mwanya wa kupokelewa kabla ya kuhukumiwa na kama atahukumiwa! Hapa cha maana ni kuangalia hili la ufisadi na kama ni kweli pesa zetu zirejeshwe toka mikononi mwa mafisadi.
 
machinga walilipwa elfu kumi kumi na ishirini pale arusha wakapewa na tshirt wakaambiwa wajiunge na msafara na washangilie....uliza mjini pale watakuambia wazi wazi. Hawakurepresent watu wa monduli. Wengi Monduli wamechoka na huyu kujiita mmasai wakati siyo na amewachafulia jina sana watu wale.
 
Back
Top Bottom