kacnia

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
3,893
15,247
Ni hisia ya pekee sana pale unapo tambua kuwa umependa kwa mara ya kwanza, wengine hupenda ukubwani na wengine katika kipindi cha makuzi yao hasa wanapo balehe. Niwapongeze wote mlio fanikisha kuwapata wapenzi wenu wa kwanza kabisa mlio wapenda, kwa upande wangu mimi haya ndio yaliyonikuta kwa msichana niliye mpenda wa kwanza kabisa katika maisha yangu.

Ni miaka mingi iliyopita siku ya jumamosi, niliamka asubuhi nikajiandaa kwenda kanisani, nyumbani hapakuwa mbali na kanisa hivyo sikuona haja ya kwenda mapema, nilitumia muda wa asubuhi kunywa chai, kuoga na kuvaa nguo nilizokuwa nazipenda zaidi (nguo za kanisani) kutokana na upekee wa siku ile - sabato ambayo makanisa yoye ya mjini yalisalia katika kanisa moja, ibada ilifanyikia nje.

Muda ulipofika nikachukua kiti changu na kuanza kujongea kuelekea kwenye umati ambao umekusanyika pamoja kwa lengo la ibada, kwa sababu nilikuwa nimechelewa kidogo ilinilazimu kukaa nyuma chini ya kivuli cha mti ambapo pia tulikaa wachelewaji wengi kila ibada ya pamoja inapo fanyika. marafiki zangu wakajiunga na mimi ili tuwe tunajadili mawili matatu pale inapo tulazimu maana penye wengi pana mengi.

Macho yakaniponza
Militupa macho upande wa pembeni kidogo ndipo nilipokutana na sura ya msichana mrembo sana. moyo ulishtuka, mwili ukakosa nguvu na akili ikaacha kufanya kazi yake kwa ufanisi, nikawa kama nimepigwa na shoti ya umeme, hapo ndipo nilipo gundua kuwa nimependa tena kwa kasi ya ajabu, kikichonivuruga zaidi ni pale nilipokuwa nageuka kumuangalia nakuta na yeye ananiangalia (sijui yeye aliwaza nini kichwani mwake ila kwangu ilikuwa ni faraja kubwa sana). baada ya ibada, yule binti alitoweka kwenye umati wa watu nisijue pa kumpata, chakula cha mchana siku hiyo hakikupanda kabisa mwili ulikuwa na hisia mchanganyiko mithili ya mwanafunzi ambaye hajasoma na yupo chumba cha mtihani akiwa na shauku ya kufaulu.

Safari ya matumaini
Niliondoka sebuleni kwenda chumbani, kwani sikufurahia chakula kabisa, jirani na nyumba yetu ilikiwepo nyumba ya mchungaji, uani alipanda miti ya machungwa, nilipo chungulia dirishani moyo ulijawa na furaha ya ajabu kwani nilimuona yule binti akiwa mama yake na mdogo wake mmoja wamekaa chini ya mti mmoja wapo wakipata chakula cha pamoja, hapo nikapanga sasa namna ya kuzungumza nae maana tayari nilisha pata uhakika kwamba atakuepo katika vipindi vya mchana mpaka kufunga sabato, kwani washiriki wanapo beba chakula kutoka nyumbani huwa na lengo la kurudi nyumbani baada ya vipindi vya jioni kabisa.

Mama yake alipo maliza kula alienda kuongea na marafiki zake, akawa amemuachia jukumu la kupeleka vyombo kwenye gari yao akimaliza kula, hapo ndipo nilipo pata nafasi ya kuongea na msichana huyu mrembo aliye iteka akili yangu kwa muda mfupi sana tangu nimuone.

Alinyanyuka na kuanza kwenda uelekeo wa gari, nilitoka nje fasta nikamsogelea na kusema ''samahani naweza kuongea na wewe'' akageuka na kusimama, nikamuuliza jina akaniambia, baada ya hapo maneno yote niliyo panga kuzungumza nae yakafutika, nikaanza kupata kigugumizi na kuuliza maswali ambayo sikutarajia kama ningeuliza kama vile, unasomea wapi, mchepuo,mbona umefunga kitambaa mkononi nk. basi nikaaga huku moyo ukiwa mzito sana akaendelea na safari yake, niliumia sana na kuilaumu akili kwa usaliti wake kwangu katika tukio muhimu sana kama lile, huku nikiwa mwenye uchungu sana kwa kushindwa kuitumia fursa vyema.

Baada ya muda kupita nilipata mawasiliano ya yule msichana kupitia dada yangu ambaye alikua ni rafiki wa mama yake, alipojua kuwa nampenda aliahidi kuniletea namba, basi nilimpigia na kujitambulisha, alipojua ni mimi alicheka sana, kisha akanipa nafasi ya kujieleza kwa mara ya pili kwa kusema ''enhe leo una maswali gani?''

Nikafunguka mwanaume na kuweka wazi nia yangu ya kuanzisha naye mahusiano, akadai kuwa yeye hana mpango wa kuingia kwenye mahusiano kwani bado mdogo na ana malengo mengine tofauti na mapenzi, niliendelea kusisitiza nia yangu kwake kwa miaka mingi, mada ikabadikika na kuwa umbali utakua kikwazo cha mahusiano yetu kwani walihamia mkoa.mwingine na kwamba amefuatilia na kujua kuwa nina mahusiano na wasichana wengi hivyo hana imani kama kweli nampenda au namtamani tu.

Hatimaye kukata tamaa
baada ya kufanya jitihada zangu nyingi zilizo gonga mwamba, niliamua kumpotezea na katika jitihada zote niliambulia American kiss tu,

Katika kipindi chote hicho tangu nimuone huyu binti, nimewahi kuwa kwenye mahusiano na wasichana kadhaa lakini sijawahi kujiskia kumpenda yeyote kati yao kama nilivyo mpenda huyu, aliuteka moyo wangu akaondoka nao wala hakunipa nafasi ya kufurahia mapenzi na msichana niliyetokea kumpenda kwa moyo wangu wote.

Amepelekea niwaumize wasichana wengi kwa sababu walinipenda kwa dhati na mimi moyo wangu ulikua kwa mtu mmoja tu. YEYE. mpaka sasa nipo kama roboti kwa sababu sijiskii kabisa kupenda na wala bado sijakutana na mwanamke ambaye amefanikiwa kuuteka moyo wangu.

“First love is dangerous only when it is also the last.”

images (3).jpeg
 
First love
Hii inakuwaga from the bottom chamber of heart na hapa ndio wengi huwa wanalia

Hisia ni mbaya sana inaleta maimivu plus majuto
Tatizo first love inakurubuni akili sana
 
First love
Hii inakuwaga from the bottom chamber of heart na hapa ndio wengi huwa wanalia

Hisia ni mbaya sana inaleta maimivu plus majuto
Tatizo first love inakurubuni akili sana
just true
 
Back
Top Bottom