First Half Bunge Maalumu la Katiba: CCM 2, UKAWA 0.

First Half Bunge Maalumu la Katiba: CCM 2, UKAWA 0.

Unaelemea CCM hata katika maelezo yako. Bado hata UKAWA wakiamua kutoka nje sasa na milele bado katiba mpya itakuja tena hili ndiyo litachochea wananchi waitake katiba mpya iliyo bora kuliko UKAWA wakirudi na baadaye washindwe kwa kura za CCM kulazimisha muundo mbovu wa sasa wa serikali 2
Ungenisoma taratibu ungegundua wazi kwamba there's no way CCM wanaweza kuwashinda UKAWA kwa kura unless, kama ambavyo nimesema kabla, CUF wawasaliti CHADEMA na NCCR... Rasimu haiwezi kupita bila theluthi mbili kutoka Bara na Theluthi mbili kutoka Zanzibar! Ni lazima CUF waunge mkono Rasimu ndipo rasimu inaweza kupita coz' CCM peke yao hawafikishi two third!! By the way, kama ungetaka niegemee UKAWA, ulitarajia niseme nini? Kwamba UKAWA waendelee tu kukaza na CCM wenyewe watalegeza, au? Kama ndivyo, tayari nimeshasema... CCM wanaweza kulegeza kisha wanaikataa rasimu na yeye (CCM) kuendelea kuwa mshindi coz' katiba ya zamani itaendelea kutumika!
 
Wala cjachanganya mambo... mimi nilichotaja ni yale ambayo nayaona matatizo ya msingi yanayolikabili taifa hili... manung'uniko hayawezi kuwa matatizo ya msingi kv sidhani kama patatokea muundo ambao hautakuwa na manung'uniko. Kusini, kwa maana ya Lindi na Mtwara na Kaskazini kwa maana ya Arusha na Kilimanjaro, zote zipo Tanganyika lakini bado kusini hawajaacha kunung'unika kwamba serikali inaelekeza shughuli za maendeleo kwa upendeleo... manung'uniko ni silika ya mwanadamu, labda jambo la kuangalia ni endapo manung'uniko yenyewe yana msingi na kweli yana athari kwa jamii husika na si tu kwamba ni manung'uniko ya watu wachache wenye sauti lakini kutokana na sauti zao yanabadilika kuwa ni manung'uniko ya wengi ambayo kimsingi athari ama chanzo cha manung'uniko hayo ni ya hao wachache. Mathalani, watu wanaoongoza kwa manung'uniko ni Zanzibar... hususani wafuasi wa CUF. Ni wananchi ndio wananung'unika lakini ukiangalia kwa makini ni manung'uniko yenye maslahi kwa viongozi na wala sio watu wa kawaida unless wawe ni wale wenye mwamko wa utaifa!

Kwamba tatizo la muungano ni manung'uniko ambayo yanasababisha hata kufunika matatizo ya msingi, hapa naomba nisikubaliane na wewe! Sidhani kama mwananchi wa kawaida ana shida sana na muundo wa muungano kuliko kushughulikwa matatizo yake ya msingi. Mimi binafsi, wala sioni kama kuna kitu chochote ninakikosa kwavile tu tupo kwenye mfumo wa serikali mbili lakini kuna mengi nayakosa kwa sababu tu watu hawataki kuwajibika, kuna uzembe kila mahali, kuna ufisadi na wizi wa hovyo n.k.... haya yote wala hayasababishwi na muundo wa muungano otherwise kwenye mataifa ambako suala la muundo si tatizo, haya yasingekuwepo!!!!
Nadhani mtazamo wako ni mtazamo wa sehemu ya jamii, na kwasababu hizo mtazamo huo unatupa nguvu za kutoa elimu zaidi kuliko kukaa kimya.

Kwanza, manung'uniko ni sehemu ya maisha yetu,hilo nakubaliana nawe. Manung'uniko yanapofikia kuathiri shughuli za kijamii si jambo la kupuuzwa tena.
Mpasuko katika BMLK ni kiashirio kizuri kuwa lipo tatizo na si manung'uniko.

Mfano, Zanzibar wameamua kutoitambua katiba ya JMT, je hilo ni jambo dogo? Ukiwa na sehemu ya nchi isiyotambua utaratibu unaoongoza jamii yetu suala kama hilo unaweza kulipuuza tu.

Pili, unaposema baadhi ya wazanzibar, si kweli.
Waliokaa katika BLW na kupitisha sheria za kuvunja katiba ni wajumbe wanaowakuilisha wananchi wa znz.

Aliyesaini sheria hiyo ni Rais wa Zanzibar.
Waliotaka wajumbe sawa katika tume ni wazanzibar.
Wanaotaka nafasi asilimia 21 ni wazanzibar.
Walioweka sheria ya kuwazuia Watanganyika wasitumie fursa za zanzibar kama ajira na ardhi ni wazanzibar. Na kila walilofanya ni wazanzibar.
Unawezaje kusema ni baadhi ili hali athari za matendo yao zipo kwa ujumla wao?

Tatu,Manung'uniko ya wananchi wa Mtwara au Lindi dhidi ya sehemu nyingine ni juu ya serikali yao. Hayajafikia kiwango cha kuvunja katiba, kuleta ubaguzi na uhasimu.

Hatujasikia mtu kachomwa moto Mtwara au kanyimwa fursa yoyote Kilimanjaro au Kigoma. Huwezi kuweka katika mizani na mambo wanayofanya wazanzibar dhidi ya Watanganyika. Wametunga sheria za kumbagua Mtanganyika na wala si Mtaliano au mtu wa Oman. Hivyo mfano wako haujakidhi haja ya ufannanisho hata kwa 1/10

Nne,ni kweli kuwa wananchi wengi kama ulivyo hawaoni athari za muundo wa muungano kwa maisha yao. Kutoona hakuna maana hazipoathari.

Zipo athari kubwa kinachozuia kutoona ni kiwango cha uelewa.
Na hilo ndilo la kufanyia kazi.
Mfano,
(a) (i)Mwananchi wa Tanganyika angefahamu kuwa kodi anayolipa ni kwa maendeleo yake na mtoto wake, basi asingekaa kimya mtoto wake anyimwe haki ya mkopo wa chuo kwasababu tu wazanzibar wanaotakiwa kupewa kipaumbele.

(ii) Mwananchi angefahamu mwanawe anapaswa kurudisha mkopo na yule wa zanzibar anasoma bure kwa kodi yake nadhani wangejua athari.

(iii)Mwananchi wa kawaida angetambua kuwa hana haki yoyote zanzibar ili hali mzanzibar ana haki hata ya kuwa kiongozi wake, angeiona athari.

(iv)Mwananchi angetambua kuwa nafasi za elimu zinatolewa kwa kuzingatia upendeleo, kwamba Watanganyika wagombee nafasi ndani ya nchi yao ili hali wenzao hata wasio na sifa wanakuja kwa kigezo cha uzanzibar, angeona athari

(v)Mwananchi angetambua kuwa sehemu ya kodi yake inatumika kuhudumia nchi jirani ya znz katika kufidia bajeti, angeona athari za muungano

(vi)Mwananchi angetambua kuwa yeye anawajibika kulipa asilimia 88 ya deni la znz kwasababu amechukua dhamana hiyo, asingekaa kimya

(vii)Mwananchi angetambua kuwa, mipango yake ya maendeleo lazima iende ikaidhinishwe nchi jirani ya zanzibar, angeona athari.

Angetambua kuwa hawezi kupata wodi ya wazazi au shule hadi wazanzibar waidhinishe tena wakiwa 50 tu, angeona athari zake.

vii)Mwananchi angetambua kuwa umeme anaolipa sehemu ya bei yake ni kumfidia raia wa nchi ya zanzibar asiyelipa, angetambua athari zake.

(viii)Mwananchi angetambua kuwa kodi yake inakwenda kulipa mishahara ya wafanyakazi wa nchi jirani ya zanzibar, angetambua athari zake

IX)Mwananchi angetambua kuwa kodi zake zinahudumia mashirika ambayo kazi zake huko znz haziongezi tija kwa Tanganyika, angetambua athari zake.

Orodha ni ndefu, ninachoweza kusema kwa ufupi ni kuwa wazanzibar wanahitaji muungano pale wanapoona kuna masilahi.
Masilahi ni wewe Mtanganyika kumtengenezea mambo yake yaende vizuri.

Kinyume chake mchango wao katika huu muungano hakuna. Lakini basi kama hakuna ingekuwa haijambo, wangekaa kimya, leo wanachota tu.

Kuna sababu gani za wao kupata 4.5% ya pato la taifa? Mchango wa znz katika pato hilo ni kiasi gani?

Mkoa gani unapata kiasi hicho na kwanini iwe wazanzibar kama sisi ni taifa moja.

Kwanini sisi tulipe mzigo wa kuendesha muungano, madeni ya ndani na nje? Je, mwananchi haoni kuwa hapo anamenyeka bila kujijua?

Mwaka huu wa fedha wamepewa bilioni 15 kutokana na kodi za wafanyakazi wa muungano. Hizo kazi za muungano nyingi haziwahusu.

Pamoja na upendeleo wa elimu ikiwa ni pamoja na kusoma bure na kupewa nafasi asilimia 21, ajira n.k. bado kodi yako inatumika kuwapongeza wazanzibar kwa kuwapa upendeleo.

Bilioni 15 ni za nini ikiwa tunapunguza unemployement kwao kwa gharama za watu wetu?

Mwaka 2013/14 zilipelekwa bilioni 32 kwa SMZ bila maelezo.
Kiasi hicho kinatoka wapi kama si kodi za Mtanganyika.
Ipo hoja kuwa ni misaada na mikopo, je znz wanalipa nini katika hiyo mikopo?

Huwezi kujua kuwa Mtanganyika anahudumia wizara ya ulinzi, mambo ya ndani na mambo ya nje. Hii ni pamoja na wizara zingine za muungano.

Gharama hizo hazipo katika bajeti ya znz. Leo pesa zao wanaelekeza katika huduma, pesa za Mtanganyika zinaelekezwa katika kubeba mzigo usiowahusu.
Mwananchi angetambua, angeliona athari

Lakini basi kama wao wana fiscal autonomy yao, huyu Mtanganyika yake ipo wapi?
Kutokana na kukosa fiscal autonomy, Mtanganyika anajikuta akihudumia kila kitu kinachomhusu na kisichomhusu. Hawezi kupanga mipango yake hadi iridhiwe na watu 50. NazDaz haoni athari tu.



 
Mkuu Nguruvi3,
Nikipata fursa nitajibu hoja zako manake hukunitendea haki kurundika hoja nyingi kiasi hicho sehemu moja vinginevyo nitalazimika niache kila kitu. Hata hivyo, wakati nikitafuta fursa ya kujibu hoja moja moja, labda nikuulize suala moja. Nchi kama Uganda, Kenya, Burundi n.k hakuna matatizo yote hayo uliyotaja kwavile ni taifa moja lenye serikali moja na hakuna upande ambao unamnyonya mwenzake kwa mujibu wa katiba! Are they much better than us only because kwa upande wetu kuna huku Tanganyika yenye koti la muungano na kule kuna Zanzibar mnyonyaji?? Na kwa maelezo yako, ni kwamba Zanzibar anainyonya Tangannyika... katika hali kama hiyo basi ungetarajia Wazanzibar waupigie chapuo muundo wa sasa unaowawezesha kuwanyonya Watanganyika... badala yake, nao wanasema ndio wanaonyonywa...! Kama ndivyo, ina maana mmoja wapo ana baseless claims otherwise the system will remain in equilibrium. Sasa ikiwa mmoja wapo ana baseless claims na bado wanasema wananyonywa; nini basi tafsiri yake kama si kwamba haya si malalamiko ya wananchi bali ni ya watu fulani fulani?! Lakini kubwa kuliko yote, hayo yote uliyoyaorodhesha hayana guarantee ya kutokuwapo tena ikiwa tutakuwa na serikali tatu. Kwani, leo hii hapa tukawa na serikali ya Tanganyika, ndo itafuta uwezekano wa wanafunzi wa kizanzibari kupata upendeleo? Leo hii tukiwa na serikali ya tanganyika, ndo itafuta uwezekano wa znz kupata mgao wa 4.5% kila mwaka? Ikiwa serikali yako ya Tanzania kila mwaka, inakomba % kadhaa kutoka mataifa ya nje kwa ajili ya bajeti, seuze Zanzibar kuendelea kukomba >4.5% kutoka Tanganyika kwa ajili ya bajeti yake??!!!LIkewise, kwa mfano hayo ambayo umeyaorodhesha mwanzoni... hivi chanzo cha hayo ni muundo wa serikali mbili zisizo na Tanganyika ndani yake au ni mfumo ambao wameuweka wenyewe?!

Mkuu Nguruvi3, we're grown up... don't beat around the bush... just hit the target coz' you're at close range. Hoja zako zote ulizotaja zitakuwa na maana if and only if you don't agree with union thing!! Kama hutaki muungano, kuwa wazi... usiwe kama watu wa CUF wanaosema wao hawapingi muungano lakini ukichambua wayatakayo, net result ni kwamba hakuna muungano. Kwanini mnakosa ujasiri wa kueleza hisia zenu?! Nitakuunga mkono kwa hoja zako zote kama main objective ni kuachana na muungano... si dhambi kuwa na maono kama hayo! Kwa mfano, ingawaje watu wanaweza kudhani mie napigia chapuo muundo wa serikali mbili, hapa nimeshapata kusema tangu zamani kwamba, ikiwa muundo wenyewe wa serikali mbili ni huu wa sasa, basi ni bora kuwa na serikali tatu kuliko mbili. Lakini mkuu wangu, pamoja na kuona unanyonywa kiasi hicho bado unataka kunipiga changa la macho kwamba unataka muungano uendelee ili hali unafahamu fika yote uliyotaja yanaweza ku-exist ndani ya muundo serikali tatu!!!!
 
Tuache yote,tujipange kuwapa watanzania katiba mpya!kila aliye mzalendo hiki ndio kipimo cha uzalendo wake,ukikwamisha mchakato hauthamini umma ingawa unajiita mtetezi wa umma!
 
Back
Top Bottom