Fire Extinguisher ama Sticker ya fire!

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Wadau nomba tujuzane!
Pita yangu hivi karibuni huku kaskazini ndo nimejua kumbe baadhi ya majeshi bado yapo. Jana pale A town nilikuta jamaa wenye wenye uniform kama polisi wetu! Wakanipiga mkono nikasimama wakajitambulisha kuwa wao ni askari wa zimamoto. OK wkataka niwaonyeshe sticker ya zimamoto! Du nilichoka kwelikweli, nikawaambia fire extinguisher ninayo wakanijibu sasa ial wao wanataka hiyo sticker! Nikawauliza inasaidia nini hiyo! Wakanijibu ni kielelezo kuwa nimekaguliwa. Niauliza nani ndo huwa anakagua wakasema wao. Nikawaambia wakague wakanambia gharama ni shs 5000 kwa gari yangu. Ilibidi niwe mkali kidogo Nikawwauliza kipi cha maana kati ya sticker na extinguisher! Wakasema extinguisher, basi nikawaambia hiyo sticker siitaki maana haiwezi kuzima moto ila kitakachozima moto ni extinguisher tu basi. Wakaona nawawekea usiku wakaniruhuru kuendelea.
Leo hii saa hii nakutana na askari wa usalama barabarani anainiuliza sticker ya fire! Nikamwambia sina halafu nikafunga vioo nikaishia. Sasa nauliza maana inawezekana ndo sheria, Je ni munimu kuwa na sticker ya fire! Nawasilisha
 
hahahaaaa kwako muhimu extinguisher bse itazima moto, kwao muhimu sticker b'se wanakua wameingiza 5000, kwa hiyo inategemea nalitizama hilo swala toka upande gani
 
Huu utaratibu wameuanzisha mwaka jana hapa Arusha, kuwa lazma kwenye gari uwe na sticker ya fire na fire xtinguisher yako iwe imekaguliwa..stika ni 25,000 na ukaguzi pamoja na kurekebisha mtungi ni 15,000. Tatizo ukifanya hayo malipo zaidi ya kupewa stika ya kubandika ktk gari unapewa na risiti ambayo siyo ya serikali..risiti ya kawaida kabisa yenye muhuri wakuchonga...mimi binafsi nilienda hadi ofisini kwao wakanipa hyo risiti, nikawambia siyo ya serikali....wakaniambia niende kesho yake kuchuka nyingine..

Kifupi huu ni mradi wa watu wachache hapa Arusha....
 
Hii nchi imeoza :A S 13: Yaani kila watu wanakaa na kufikiria jinsi ya kuibia wenzao badala ya kuwatumikia!!! Sasa sticker ni ya muhimu kuliko fire extinguisher huu si uhuni na wizi tu!!!
 
Mambo mengine ni kituko,wizi na .....sijui niandikeje.
Juzi nilikuwa na rafiki yangu hapa Arusha,hakuwa na hiyo kizima moto. Alipo kamatwa akatakiwa aoneshe stika,hakuwa nayo.
Akawauliza ataipata vipi nao wakamueleza aende ofisini kwao.
Tulienda na jamaa hadi ofisini na kuomba stiker,huwezi amini, stiker tulipata lakini kizima moto hatukupata na kwakuwa tulikuwa tumeshalipia,alituambia tuendee j3 ijayo
 
Jamaa yangu aliniambia Fire extinguisher aliinunua miaka minne iliyopita, anachofanya ni kununua sticker kila mwaka, hakuna cha kukaguliwa wala nini, ni njia tu ya serikali kuongeza mapato. Kama nia ni usalama basi ukaguzi ungefanyika bureee!!!
 
hata huku Mwanza kautaratibu ni hako wa kuu! Hata kama unao huo mtungi, basi kama huna sticker trafic akikushika unalipishwa faini ya elfu 20, 000 . Jamani tutapona kweli? Mbona hawa jamaa hawana mtu?
 
mimi mwez huu nilifika babati-polisi wa pale wakanipiga notification ya elfu 20000 kisa eti sina sticker ya fire-japokuwa fire extinguisher nilikuwa nayo-nilibishana nao,but mwishoni nikalipa-cha ajabu nikazungumza na polisi mmoja nikiwa narud anipe sticker ya fire-akaniahidi atanipa kwa elfum 5-ila wakati narudi nikaona ananipa mlolongo mrefu sana-nikaona ni walewale tu-nikaachana nae
 
Jamaa yangu aliniambia Fire extinguisher aliinunua miaka minne iliyopita, anachofanya ni kununua sticker kila mwaka, hakuna cha kukaguliwa wala nini, ni njia tu ya serikali kuongeza mapato. Kama nia ni usalama basi ukaguzi ungefanyika bureee!!!

Fedha hii inafika serikalini kweli? Jamaa kasema ka mhuri kenyewe ka kuchongea barazani. Mbona ukiwa mkali wanakuachia kama kweli kuna serikali pale. Kuna jamaa akanitonya kuwa huo ni mradi wa kuwafanya waishi maana serikali nayo imewasahau sana.
 
Upuuzi mtupu, kwanini wasikague na magari ya wakubwa au wao hiyo stiker ni wanyonge tu. Wangese kuanzia rais hadi mwenykt wa kijiji
 
Back
Top Bottom