Wazo muhimu na la msingi kuhusu setting ya fire extinguisher kwenye majengo na sehemu za umma

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Nina wazo la jinsi ya kufanya setting za fire extingisher kwenye majengo na sehemu za umma ambazo zinaweza kupatwa na moto au mlipuko kiasi cha kuhitaji hatua za haraka kwenye kuukabili. Nadhan taasisi au idara za Serikali na binafsi zinaweza kufanyia kazi wazo hili ili kuleta ufanisi na sio kutegemea magari ya Zimamoto tu.

Zitengenezwe system ambazo unaweza kuactivate fire extingisher hata ukiwa mbali na sio mpaka uwe karibu kama inavyofanyika sasa. Kuna wakati moto unakolea sehemu fulani iwe kwenye gorofa au chumba kiasi cha kufanya isiwezekane kuusogelea na kutumia mitungi ya fire extinguisher.

Kuwe na mfumo ambapo mtu anaweza kua ghorofa ya chini aweze kuactivate mtungi wa fire extingisher uliopo gorofa ya tano yenye moto. Mf.unavuta waya flan au unabonyeza batton fulan unaactivate fire extinguisher za gorofa ya 5.

Pia unaweza kua na mtungi mkubwa wa fire extinguisher ukawekwa nje(kama mitungi ya gas za kupikia) na zikatengenezaa pipe zikasambazwa kwenye vyumba na korido za jengo kiasi moto ukilipuka kunakua na mtu anacontrol pipe ipi iwashwe kulingana na sehemu moto uliopo na sio lazima asogelee moto unakowakia..

NB: Mimi sio mwandishi mzuri wa hoja na nimejitahidi kadri niwezavyo kufikisha ombi langu kupitia JF. Kwa wale ambao watakua hawajanielewa niwaombe radhi ila kwa wataonielewa naombeni tuchangie hoja hii. Pia wenye mamalaka kama mtaweza kufanyia kazi jambo hili itakua faida kwa taifa letu.
 
Ninachokiona sasa tutaanza kukaguliwa 'extinguishers' kwenye vibanda vyetu huku na faini kali, kama huna mtungi kaa mguu sawa.
 
Zinaitwa fire hydrants. Ni takwa la kisheria kwa Kila jengo kuwa miundombinu hiyo. Sema kikosi kimejikita kuuza Certificate za Fire .na kusahau kuhakijisha compliance
 
Zinaitwa fire hydrants. Ni takwa la kisheria kwa Kila jengo kuwa miundombinu hiyo. Sema kikosi kimejikita kuuza Certificate za Fire .na kusahau kuhakijisha compliance
Nadhan pia hakuna mkazo sana kwenye haya mambo. Ndo maana mambo yanajiendea tuu
 
Back
Top Bottom