Asante sana kwa maswali mkuu. Nitajitahidi kujibu. Frem zote mbili za biashara nimepanga karibu na kituo cha Magomeni Mapipa - Morogoro road nyingine mbali kidogo na kituo ila karibu na barabara, frem ya kwanza kodi ni laki moja kwa mwezi (1.2m kwa mwaka) na tayari nimeshalipia kodi ya mwaka hadi February 2014, ya pili ni elfu 90 kwa mwezi (1.08m kwa mwaka) nategemea ku renew mkataba ifikapo 30 April mwaka huu. Sehemu za biashara zote ni competitive areas but the market is high, kuna wateja wengi maana ni sehemu ya heka heka na muingiliano wa watu ukizingatia kuwa ni karibu na barabara kuu ya Morogoro na pia karibu na kituo cha daladala. Kiwanja kwa ajili ya bond bado hakijapimwa ila kiko kwenye process ya kupimwa na nyaraka ninazo. Maduka yote nina wafanyakazi, kila duka mfanyakazi mmoja na huwa naenda kwa zamu kusimamia mwenyewe kila siku. Nauza kwa reja reja na bidhaa zangu huwa nanunua kwenye maduka ya jumla Kariakoo. Toka nianzishe biashara hizi nimekuwa nikinunua bidhaa by cash, sijawahi kununua kwa mali kauli. Kiukweli naipenda sana biashara ya mali kauli tatizo kwenye maduka yote ya jumla ambayo nimekuwa mteja hawatoi huduma hiyo. Mkuu kama kuna sehemu unafahamu ambapo naweza pata bidhaa kwa mali kauli nitashukuru sana tukiwasiliana zaidi kwa PM maana hiyo itamaliza kabisa tatizo langu.