FINALY: Tanzania signs proposal for EAC political federation

Du Habari nzuri, lazima tulinde maslahi yetu.Hongera sana mh. Samwel Sita na Team yako.
 
Kwa hili Mh. Sita anastahili pongezi! Hongera sana Mkuu. Umetetea maslahi ya taifa.

Mkuu mimi sikubaliani nawewe kwasababu inaonekana Waziri Sitta na maafisa wetu walikua busy na mambo mengine binafsi badala ya kufanya kazi wanayopaswa kutufanyia. Matokea dakika za mwisho wanakurupuka eti wanagoma kusaini. Uzembe tunaoshuhudia katika Idara na Taasisi za Serikali sasa umekomaa tunavuka mipaka ya nchi.
 
Well done Sitta! Keep it up! Tunapenda viongozi makini na wanaoweka mbele maslahi ya taifa letu.
 
Angekuwa Yule Mwapachu angetumaliza, Huyu Sitta ingawa haileweki lakini wakati mwengine anakuwa na msimamo
patty.gif

Juma Mwapachu ni comprador hachezi mbali na chenji ndio maana siku hizi anawapigia debe Barrick Gold na Exin bank!!
 
Wangekuwa wanakomaa hivi kwenye mikataba ya madini tungekuwa mbali sana.

Hata kama mikataba yetu ingekuwa inapitishwa na bunge, kwa design tuliooshwa na wabunge wetu kwenye muswaada wa katiba kila kila jambo litakaloletwa na serikali ya CCM lazima walipitishe especially kama CDM wanamatatizo nalo. Hayo unayoyasema ni wishful thinking....................!!
 
Mkuu mimi sikubaliani nawewe kwasababu inaonekana Waziri Sitta na maafisa wetu walikua busy na mambo mengine binafsi badala ya kufanya kazi wanayopaswa kutufanyia. Matokea dakika za mwisho wanakurupuka eti wanagoma kusaini. Uzembe tunaoshuhudia katika Idara na Taasisi za Serikali sasa umekomaa tunavuka mipaka ya nchi.
Unatakiwa uwe na ufahamu wa kilichokuwa kinaendelea kabla ya kuanza kuhukumu. Nina hakika yeyote anayefuatilia hatua kwa hatua mchakato wa EAF anakushangaa unachosema maana inaonesha huelewi hata nafasi na majukumu ya mawaziri wa africa mashariki. Walau kwa kifupi ujue tu kuwa riport ile haiandaliwi na wanasiasa bali na watendaji wenye utaalam, kazi ya waziri ni kuipitia na kuamua kama asign au la.

Kwahiyo wale watendaji (secretariat) ndio ambao waliingiza vitu ambavyo Tanzania ilishasema haivitaki; suala la umiliki wa ardhi na suala ulinzi na usalama. Kuhusu usalama ktk mkataba Tanzania inapinga kipengele kinacho sema mwanachama akiingia vitani basi wanachama ni lazima waingilie kumsaidia, Tanzania inasema hicho kipengele hakina mantiki maana kuna wakati mwanachama anakuwa ndo mkorofi kwahiyo itakuwa shida sana kwa nchi kama yetu ambayo ni mwanachama pia wa SADC na kuna protocol tulisaini pia kule Lusaka kama sikosei ilikuwa 2009, ina maana Rwanda ikiishambulia DRC sie tutawezaje kutekeleza kipengele kama hicho wakati DRC ni member pia wa SADC? Kwahiyo Tanzania imesema suala la kusaidiwa ibaki kuwa ni makubaliano kati ya nchi na nchi ndani ya EAC.

Wanachama wengine kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi usalama wao unayumba na majeshi yao yako bize kwa sasa ndo maana walitaka hilo lifanyike haraka, ukiangalia sana sie ndo tungeingia hasara.
 
Wakenya wamechokoza vita na Al Shabab, wanashindwa sasa wanategemea Tanzania iwasaidie, pumbafuuu zao
 
Kweli Samuel Sitta ni jembe la ki-ukweli jaama. Ingalikua wengine hao wenzetu wangejimwa tu wino hivo hivo bila hata ya kujua yaliomo.

Viva Samuel Sitta katika hili; umeonyesha ni mtu makini sana na kwamba moyoni mwako utaifa mbeeele kama tai!!!

Hatimae Tanzania imetia saini mkataba wa East Africa community ambao waziri Samwel Sitta alikataa kusaini mpaka vipengele viwili vya ardhi na usalama kupitiwa upya..wamekubaliana hakuna swala la ardhi na ulinzi kutokuwepo!

Source: Daily National
 
Hii habari safi sana. Ningekuwa nakunywa pombe au kuvuta bangi leo ningechanganya vyote kwa mkupuo kama ishara ya kushereheka. Leo wakenya wana usongo!
 
Good work by someone.

But I'm curios to figure out where the EAC is heading, say in 20yrs!
 
Unachokisema ni kweli kabisa;

jumuia hii niionavyo mimi kama mali binafsi ya viongozi wa nchi vile - watu wa kawaida labda mpaka Samuel Sitta aje aone namna ya kutufanya tuwe at the epi-centre ya mambo ya chombo hicho ili kiweze kuleta maana kwetu.

Good work by someone.

But I'm curios to figure out where the EAC is heading, say in 20yrs!
 
Mh Sitta ukiamua unaweza.
i salute you!
Thank you kwa kuthamini raslimali za nchi yetu.
 
Sio maamuzi ya Sitta ni ya baraza la mawaziri wa Kikwete. Mbona wanapokosea lawama anapelekewa Kikwete? Basi wanapofanya vizuri pia pongezi apelekewe Kikwete.
Hongera Rais Kikwete kwa kujali maslahi ya watanzania.
 
Kibona,

Unasema secretariat ndiyo imeingiza vitu ambavyo sisi tulikwisha kataa. Katika secretariat hiyo hapakuwemo maafisa toka Tanzania? Haya majadiliano yameendelea muda mrefu, inakuwaje yanapofikia kusainiwa sisi ndiyo tunajua kwamba kuna mambo ambayo siyo sawa? Husipende kutetea watu wetu,nchi yetu imejaa uzembe.

Tunavyofanya uzembe hapa nyumbani ndiyo hivyo uzembe wetu sasa umeanza kuvuka mipaka ya nchi.
 
Mpaka sasa mie sielewi kinachoendelea na kwakuwa maisha magumu na hatujapata mshahara alafu ninashida ya 50,000
 
Back
Top Bottom