Finally: Nimeanza rasmi kilimo cha miti ya mbao Iringa

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,177
2,000
Baada ya kuona fursa hii kupitia jukwaa hili nimeamua kuifanyia kazi.
Mwaka huu mwezi wa 8 nikasafiri kuja Iringa mji wa Mafinga nikafanya research na kugundua kweli kilimo hiki kinafanyika na mashamba yanapatikana!
Nikafanikiwa kupata Shamba ekari 5 maendeo ya Ifunda kwa 250,000@ garama za resekali ya kijiji ni 50,000. Kusafisha shamba ikanigharimu 150,000 maana lilikuwa na vichaka.
mwezi huu wa 12 nimefanikiwa kupanda ekari zote miche ya pine kwa gharama zifuatazo. Miche 2250 @sh 100(miche 450 kwa ekari 1) Gharama za wapandaji ni sh 60 kwa kila shimo moja. Mwakani Mungu akipenda Nina lengo la kupanda miche ya milingoti ambayo inawahi kuvunwa kabla ya pine.
Hii ni fursa nzuri kwa wale wenye malengo ya muda mrefu. karibuni
 
Wissman

JF-Expert Member
Dec 12, 2014
992
1,000
Mkuu kuna mkubwa mmoja serikalini kaanzisha kiwanda cha nguzo za zege. Likatolewa ze tamko kwamba wanataka wasitishe ukataji miti ya nguzo ambayo ni uharibifu wa mazingira. Ukija upande wa pili maliasili nao wanakomalia sana kukata miti. Kuwa makini mkuu
 
The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
7,911

Kuna miti ya biashara achana na hiyo ya uoto asili, miti kama pine, mikaratusi, mitiki n.k ni miti inayopandwa kwa ajili ya biashara na nikujuze tuu siyo kila mtu apandaye miti anataka kuuza nguzo, miti inatumika kutengeneza karatasi, furniture n.k acha uoga
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,177
2,000
Mkuu kuna mkubwa mmoja serikalini kaanzisha kiwanda cha nguzo za zege. Likatolewa ze tamko kwamba wanataka wasitishe ukataji miti ya nguzo ambayo ni uharibifu wa mazingira. Ukija upande wa pili maliasili nao wanakomalia sana kukata miti. Kuwa makini mkuu
Mkuu kuna mkubwa mmoja serikalini kaanzisha kiwanda cha nguzo za zege. Likatolewa ze tamko kwamba wanataka wasitishe ukataji miti ya nguzo ambayo ni uharibifu wa mazingira. Ukija upande wa pili maliasili nao wanakomalia sana kukata miti. Kuwa makini mkuu
Miti ya pine ni ya mbao mkuu sio nguzo..... pia milingoti ni mult purpose kwa ajili ya nguzo na mbao pia ...vulevile inatumika kama mirunda kwa ajili ya ujenzi
 
mtotowamamanjungu

JF-Expert Member
Oct 13, 2016
351
500

Kweli.. Japo soko la mbao ni pana zaidi.. Na gharama za nguzo za nzge ni kubwa sidhani kama tanesco wataacha kununua nguzo ya mufindi...
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,177
2,000
hiyo ni biashara nzuri sana after 10 years unaweza kuvuna ukauza kila mti kwa 15,000×2250 ni zaidi ya 337,000,000 ni bonge la uwekezaji halafu watu wanalia eti serikali serikali!ebooh kufa na tufe!
ni bonge la uwekezaji wa muda mrefu Nina mpango wa kulima ekari 40 ndani ya miaka mitatu ijayo hapo naamni kama mungu akinijalia naweza kustafu kabla ya muda na kufanya biashara nyingine
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,177
2,000
Kweli.. Japo soko la mbao ni pana zaidi.. Na gharama za nguzo za nzge ni kubwa sidhani kama tanesco wataacha kununua nguzo ya mufindi...
kilichonishangaza ni huku mufindi ndani ndani kuna hadi raia wa Kenya na Rwanda wamenunua mashamba makubwa na kupanda Miti huku watanzania tunaendelea kupiga soga kuwa hakuna ajira.
 
monaco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,184
2,000
Miti ya pine ni ya mbao mkuu sio nguzo..... pia milingoti ni mult purpose kwa ajili ya nguzo na mbao pia ...vulevile inatumika kama mirunda kwa ajili ya ujenzi
unajua miti hiyo ulioipanda itatumia miaka mingapi kuvuna? mbao?
na uko umbali gani kutoka barabarani?
 
mtotowamamanjungu

JF-Expert Member
Oct 13, 2016
351
500
kilichonishangaza ni huku mufindi ndani ndani kuna hadi raia wa Kenya na Rwanda wamenunua mashamba makubwa na kupanda Miti huku watanzania tunaendelea kupiga soga kuwa hakuna ajira.
Tanzania shamba la bibi lisilovunwa na wajukuu,
Wanavuna wazamiaji.. Tuwakilishe bro
 
lemone grass

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
291
500
Bravoooo!!!! wachache sana watakuelewa. hope tutaungana msimu ujao, pamoja na elimu itolewayo kuhusu uwekezaji wa muda mrefu watu bado wanatetemeka!! wakati mtu anaamka usingizini, atajikuta amechelewa sana. haijalishi una umri gani, time will tell.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom