Finally mpenzi wangu kaniacha lakini bado nampenda

toto zuli

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
265
278
Ilikuwa kwenye mida ya saa 2 usiku alinipigia simu akaniambia nina maongezi na wewe ukiwa free kwenye saa nne ni beep Nina maongezi na wewe

Muda ulipowadia nilimbeep akanipigia tuliongea takribani dakika 20 kuhusu maisha na mahusiano ila finally alikuja kunitamkia hahitaji kuwa na mm katika mahusiano kwa sababu ameona

1. Mimi ni mtu nisieleweka

2. Pili alinipa muda mambo yangu niyaweke sawa Akaona sieleweki

3. Alishanipa muda nibadilike akaona sielweki niko vile vile

4. Amejitahidi kunipenda toka moyoni lakini moyo wake umekufa ganzi

Mwisho akaniambia tuachane Lakini pia akanisisitia ndugu zangu niwambiea Kama tumeachana nisipo sema watanitanga
 
pole sana mkuu, sio kila mahusiano huwa yanazaa ndoa,karibu kwa ulimwengu mwingine wenye furaha na amani , likuepukalo lina heri ndani yake boss wangu.
 
Kila kitu Ni kwa muda tu, huyo alishakuacha moyoni mwake sikunyingi tu.
Mapenzi hayashauriki wapo wataokwambia achana naye, wengine wataokwambia mtafute muongee lakini yote kwa yote
Jua mwenzio ajakuacha hapo tu kwasababu mmeongea, alikuacha long time hata ukimrudia hatokupenda Sana.
 
Kubaliana na hali, Kama kakwambia moyo wake umekufa ganzi basi jipe muda utapata anayekupenda.
 
Ni kosa kubwa sana kwa mwanaume kuzikubali stress za mapenzi kumtawala.

Chuja mawazo yako. Una mambo mengi ya kufanya kwa ajili ya Taifa, achana naye.
 
Ilikuwa kwenye mida ya saa 2 usiku alinipigia simu akaniambia nina maongezi na wewe ukiwa free kwenye saa nne ni beep Nina maongezi na wewe

Muda ulipowadia nilimbeep akanipigia tuliongea takribani dakika 20 kuhusu maisha na mahusiano ila finally alikuja kunitamkia hahitaji kuwa na mm katika mahusiano kwa sababu ameona

1. Mimi ni mtu nisieleweka

2. Pili alinipa muda mambo yangu niyaweke sawa Akaona sieleweki

3. Alishanipa muda nibadilike akaona sielweki niko vile vile

4. Amejitahidi kunipenda toka moyoni lakini moyo wake umekufa ganzi

Mwisho akaniambia tuachane Lakini pia akanisisitia ndugu zangu niwambiea Kama tumeachana nisipo sema watanitanga
Nadhani huyo jamaa alihitaji ubadilike uwe mtu mwingine. Afadhali hukubadilika maana ungeishi Maisha fake
yaani usingekuwa wewe bali huyo mtu mwingine ambye jamaa alitaka uwe. Jamaa alimpenda Zaidi huyo kimbe aliyekuwa kichwani mwake
na siyo wewe ndiyo maana moyo wake ukafa ganzi baada ya wewe kugoma kubadilika.
 
Shukuru snaa na songa mbele kila jambo huwa na sababu hutaelewa kwa sasa ila hapo baadae utaelewa uliepushwa na nn. Mshukuru sana Mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom