KiZunguMukuti
Member
- Oct 7, 2014
- 66
- 66
Ni kwa muda mrefu sana fimbo zinatumiwa kama njia kuu ya kuwakanya wanafunzi na hata kudai kuwarekebisha pale wanapokosea!,binafsi sikumbuki kama kuna kipindi fimbo zimewahi kukatazwa mashuleni ingawa kuna baadhi ya shule hawatumii fimbo na wanafunzi wanafaulu vizuri,mfano ni mzumbe sekondari ya morogor,kule hakuna fimbo,na mpaka sisi tunahitimu pale hakukua na fimbo,na wanafunzi wanafaulu vizuri sana,lakini pia shule ya msingi Lupalama A iliyopo Iringa vijijini kuna fimbo sijawahi ona kwingine!,shule ile wameweka kigezo cha kutumia fimbo kama njia pekee ya kuwafaulisha watoto ingawa hali siyo kama inavyotegemewa na matokeo yao ni mabovu kuliko kawaida,naamini hali hii ipo hata hapo kwenu!,sasa ningependa kuwauliza watu weusi tunaoishi katika hili bara la afrika,hivi ni kwanin hali hii inaendelea?,wakoloni waliotutawala walikua hawatujali na hawatupendi ndio maana waliuanzisha huo utaratibu wa kutumia fimbo!,sasa kwanin sisi pia tunaendelea nao ili hali wao katika nchi zao hawatumii hizo fimbo ili kuwafaulisha wanafunzi au kuwakanya wanao na watoto wao wanafaulu vizuri tu?,kwanin sisi tunashindwa kutafuta njia mbadala?,hivi unapomchapa mwanafunzi ambae ni mwafrika kama wewe!,hujisikii vibaya moyoni mwako?