Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Kusini Nyanda za Juu kumeibua wanasiasa wengi wenye umaarufu ndani ya chama tawala na upinzani. Mmoja ambaye amefanikiwa kutikisa anga la Tanzania kisiasa ni Mtikila ambaye ni mzaliwa wa wilaya ya Ludewa ambayo ni jimbo la uchaguzi la Mbunge Filikunjombe. Ikumbukwe kwamba mara moja Mtikila alishawahi kugombea ubunge kule Ludewa na kurudi kwa aibu bila hata kuambulia theluthi moja ya kura.
Filikunjombe alipoenda kugombea kule hakuwa na umaarufu wa kujulikana kisiasa kitaifa kama ilivyo kwa mchungaji Mtikila, lakini kwa kipindi kifupi tu amejizoelea umaarufu mkubwa jimboni mwake na hata kitaifa kwa msimamo wake kujali utaifa na kutetea haki za wengi na pengine hata kudiriki kuinyoshea kidole serikali bila woga.
Mtikila pamoja na kuwa mwanasiasa aliyediriki kuanzisha chama cha siasa ambacho hakionyeshi kukua ameonekana kutopokeleka kwao kwa vile ni mtu wa blabala za mdomoni licha ya kujenga hoja za msingi. Lakini je, ili kupokeleka kwa wananchi ni kufungua kesi mahakamani na kuishtaki seirkali tu bila kuwasogelea karibu wananchi? Sina mazoea ya kuona Mtikila akifanya mkutano ya hadhara ila mikuano yake ni mahakamani mahakimu na wanasheria.
Wote wawili ni maarufu, lakini mmoja anaonekana kutambulika zaidi kwa wananchi si kwa maneno bali kwa matengo kinyume na mwingine yupo zaidi kwa kauli na mara anaingia mitini, atakaporudi huko sijua atakuna na lipi.