Filikunjombe: Mkulo, Maghembe wajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filikunjombe: Mkulo, Maghembe wajiuzulu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Feb 11, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, amewataka mawaziri wa Fedha, Mustapha Mkulo na wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe kujiuzulu nyadhifa zao kwa kushindwa kutimiza ahadi ya Rais ya kununua mahindi kwa wakulima wa jimboni mwake.
  Kauli hiyo aliitoa jana bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo alitaka kujua utekelezaji wa ahadi hiyo.

  Filikunjombe pia alitaka kujua ni hatua gani ambazo serikali imechukua kwa ajili ya kununua mazao ya wakulima hao ambao walitekeleza mpango wa wake wa kilimo kwanza na kupata mazao mengi lakini iliwazuia kuuza mahindi hayo nje ya nchi kwa madai kuwa serikali ingenunua mazao hayo jambo ambalo halikutekelezwa.

  Akijibu swali hilo, Magembe alisema Serikali haijapuuza agizo hilo bali inajipanga kutafuta fedha ili kuhakikisha inanunua mahindi hayo kwa wakulima katika kipindi kifupi kijacho. Alisisitiza kuwa Serikali haijazuia kuuza chakula katika masoko mengine isipokuwa iliweka tahadhari kwani wanunuzi wengi walikuwa wakinunua mazao ya wakulima kwa kutumia njia za panya.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  haya maswali huwa hayana nguvu, kwani yanaulizwa siku za nyuma sana...hata kama kweli anatakiwa ajiuzulu...mpaka swali linakuja kuulizwa anakuwa ameishafanya jambo fulani la kuridhisha

  usanii tu huu
   
 3. A

  Ahakiz Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hivi hamujagundua tu au mpaka waje wazungu wizara zote zimeoza mpaka mtu akujue ndio akufanyie unachotaka japokuwa ni haki yako yaani wizara ya afya imeaanza na zitafuata zingine kudhihilisha haya maneno yaani wizara inakuwa na matatizo yote haya waziri na naibu wake wapo
   
 4. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Circus
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Jibu lilitolewa na waziri bungeni ni jibu la kisanii na ametoa jibu linalopingana lenyewe. Kwamba serikali haikuzuia uuzwaji wa mazao nchi za nje bali ilikuwa tahadhari. Wananchi waliambiwa wasiuze mazao nje ya nchi na kwamba serikali ndiyo itakayo yanunua. Leo anajibu kwamba serikali ilitahadharisha wakati ilikataza kuuzwa mazao nje. Wananchi ndio wameathirika kutokana na mazao yao kuuzwa na hivyo maghala yangali na mazao ya mwakajana wakati mazao mapya yameanza kuvunwa.
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Serikali yetu full mzuka kila kukicha. Inawezakana kutetea kwamba serikali haikuzuia kuuza mazao nje ya nchi wakati nakumbuka walitangaza kwamba hakuna kuuza mazao nje? Mbona kauli zinapingana na hawana kumbukumbu nini walisema hapo awali na leo kuja na kauti tata inayopingana na tamko la awali?
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa nini tusibadilishe kipengere kwenye katiba mpya ijayo kwamba mawaziri si lazima watokane na wabunge kwa sababu mawaziri wote tulio nao ni wanasiasa na wanafanya shughuli za serikali kisiasa zaidi na hata kuwavuruga makatibu wakuu na wakurugenzi kwa itikadi za kisiasa.
   
 8. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu hapo
   
 9. N

  Njele JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kinachonishangaza huyu jamaa Filikunjombe hana woga kama ******* wenzake wanavyoogopana na kulindana. Haogopi tindikali au yaliyowapata akina Mwakiembe?
   
 10. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ''CIRCUS'' hili neno AG(mwanasheria wa serikali-Werema) alisema juzi mjengoni kwamba kwenye maneno ya Kiindereza halipo. mi nadhani anaitaji msaada kidogo.
   
Loading...