Filamu ya Royal Tour yaongeza watalii nchini

Filamu ya Royal Tour yaongeza watalii nchini

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,447
Reaction score
2,094
Wakati Rais Dkt. Samia Suluhu anaingia madarakani mwaka 2021 sekta ya utalii ilikuwa inapitia katika mazingira magumu kutokana sababu mbalimbali ikiwemo athari ya UVIKO 19

Mapato ya utalii yalipungua sana, ajira nyingi zikashuka, wanufaika wa sekta hii wakaathirika kiuchumi.

Hata hivyo, ujio wa Rais Samia mwaka 2021 ulibadilisha taswira ya sekta hii kwa kiasi kikubwa, hii ni baada ya kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kuandaa mkakati maalum wa kutangaza vivutio vyetu katika maeneo mbalimbali ya Dunia

Soma pia:

Tukio kubwa lililovutia hisia za wengi na baadae kuzaa matunda ni lile la yeye kushiriki kucheza filamu maarufu ya Royal Tour

Filamu hii iliyokidhi vigezo vya kimataifa ilisaidia sana kuwavutia watalii hasa wale kimataifa kuja nchini.

Katika kipindi kifupi idadi ya watalii ya kimataifa iliongezeka kutoka 922,692 mwaka 2021 hadi kufikia 2,141,895 mwaka 2024, ongezeko la asilimia 132.1 huku watalii wa ndani wakiongezeka, kutoka 788,933 mwaka 2021 hadi kufikia 3,218,352 mwaka 2024

Ongezeko hili la watalii limepelekea kuongeza ajira kwa watu milioni 1.5. Licha ya mafanikio haya katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake katika sekta hii, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kupitia ilani ya uchaguzi wa CCM kuongeza ajira kutoka milioni 1.5 mwaka 2025 hadi milioni 3 mwaka 2030 sambamba na kuongeza idadi ya watalii hadi milioni 8 mwaka 2030

1754910780325.png

Chanzo: ITV DIGITAL
 
Ni kweli utalii umeongezeka kwa kasi, lakini data za CCM always ni ngumu kuziamini
 
Back
Top Bottom