Filamu ya DONT BREATHE

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Image may contain: 2 people, people standing and indoor


Ni Rock, Alex, na Money. Wanaishi kwa kutumia wizi. Wwanavunja usiku na kuingia kwenye nyumba watayoona inafaa na kuchukua kila kinachowafaa, wanaishi hivo.

Walipopata taarifa kutoka kwa mtu anaewapa dili za nyumba za kwenda kuiba,aliwaelekeza kuhusu dola laki tatu,alizopewa mzee mmoja kama malipo baada ya mtoto wake wa kike kuuliwa, wao wakaenda kutaka kuziiba.

Walichokuwa hawakijui wakakijua,ni kuwa huyu mzee kapoteza uwezo wa kuona, na walipojua kuwa haoni, hawakujua kuwa ni mwanajeshi mstaafu.

Mtu aliepigana vita vikubwa miaka mingi iliyopita, na ni vita ndio ilimuondolea macho..wakatumia uwezo wao na vifaa kuingia ndani,lakini hawakutumia akili baada ya kufika ndani.

Mlango uliohifadhiwa pesa uliposhindwa kufunguka, wakatumia bastola. Bstola haikuficha siri, ikamjulisha mzee kutoka kitandani kuwa kuna watu ndani.

Walipomuona kasimama mbele yao na hawaoni, kumbe mzee huyu ana kitu kikubwa ndani ya mwili wake baada ya kupoteza macho yake. Kitu kinachomsaidia kwenye maisha yake yaliyobaki.

Pumzi ndio gulf war man anasikia pumzi za viumbe,na anajua kuwa kuna mtu au hakuna kupitia pumzi zao

Ni ndani ya nyumba yake ndipo palipotokea mshike mshike wa aina yake baina ya kipofu na wanaoona walikufa, tena kinyama kwa sababu moja tu ili uwe hai usipumue. Ukipumua unakufa kwa mikono yake, ukiacha kupumua unakufa kwa kujiua kwa kukosa pumzi, nini wafanye, nini wasifanye!..ni katika..

#DONT BREATHE..
 
Unfortunately nimeshindwa kuendana na technology ya hizi movie za siku hizi,story nzuriii but ukishaiweka kwenye kioo stim zinakata sijui labda kwa sababu napenda zaidi action zinazofanana na ukweli!huwa naona kama computer imetumika sana tukilinganisha na zile za 80s kama predator,John Rambo etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom