Filamu ya cannibal halocaust ya 1980

Filamu ya cannibal halocaust ya 1980

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,480
View attachment 1409350

IMG-20200405-WA0028.jpeg


Hii bado ni filamu ya kiitaliano ya kutisha bora sana duniani hadi sasa, inaitwa Cannibal Hallocaust iliyotoka rasmi February 7, 1980 Millan Italia chini ya muongozaji Ruggero Deotato raia wa Italia.

Uhalisia uliotumika katika matukio ya kutisha ndani ya filamu hii ulipelekea serikali ya Italia kuamini kua filamu hii ni halisi, haikuigizwa, na mauwaji yaliyofanywa humo yalikuwa ni halisi, hii ilikuwa ni siku 10 tuu baada ya filamu hii kuachiwa.

Hii ilipelekea Director Ruggero kukamatwa na Polisi kwa kosa la mauwaji, na ubaya ni kwamba kabla ya kuingia location washiriki wote walisign mikataba yenye kipengele cha kutoonekana mtaani ovyo kwa mwaka mzima tangu filamu hiyo itoke ili kuongeza uhalisia zaidi, hii ndio ilichochezea zaidi kuamini kuwa jamaa aliwauwa kweli washiriki wa filamu hii.

Director alienda jela kwa kosa la mauwaji ambayo kiuhaalisia hakuyafanya, Bali ni ufundi tuu wa kutengeneza matukio yawe halisi kwenye filamu, akawasiliana na Luca Barbareschi ili awaambie waigizaji wenzake wakatoe ushahidi kuwa wapo hai bila kuongea lolote na vyombo vya habari kwa kuhofia kuididimiza filamu hiyo sokoni.

Wanyama wote waliouliwa katika filamu hii ilikuwa kweli kabisa, hiyo haikuwa kuigiza. Baba wa muigizaji aliyecheza kama Miguel aliuwawa wakati mwanae huyo akiwa location anaandaa filamu, akaenda msibani na wakaamua waingize kipande hicho kwenye filamu, kwahivyo huzuni ya Miguel haikuwa ya kuigiza.

Filamu hii ya kutisha imepigwa marufuku kuonyeshwa katika zaidi ya nchi 50 duniani ikiwemo italia yenyewe, faida waliyoipata Ni mara 20 zaidi ya bajeti waliyoitumia.



IMG-20200405-WA0030.jpeg


@military_Genius
 

Attachments

  • IMG-20200405-WA0035.jpeg
    IMG-20200405-WA0035.jpeg
    54.7 KB · Views: 10
Back
Top Bottom