Filamu kuoneshwa tena Saudi Arabia

Filamu kuoneshwa tena Saudi Arabia

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322

_100934850__100712543_mediaitem100707982.jpg


Filamu kutoka katika kitovu cha utengenezaji filamu duniani Hollywood zimekuwa zikichujwa nchini Saudi Arabia wakati ufalme ukiruhusu urushwaji filamu baada ya miaka thelathini na tano ya marufuku.
Kuonyeshwa kwa filamu ya blockbuster, "Black Panther" ni sehemu ya majaribio ya mapitio ya filamu zinazopitia mchujo kabla ya majumba ya kuonesha filamu kuruhusiwa kuwaonesha waja, awali kila mtu alikuwa akitazama nyumbani kwake, ila kwa hadhira sasa ni rasmi tangu tarehe 18, April mwaka huu .

Maafisa wa serikali, wanadiplomasia na jamii wanatarajiwa kushiriki. Marufuku ya kuoneshwa filamu nchini humo lengo lilikuwa ni kulinda imani ya kihafidhina ya kiislamu pamoja na mila za kitamaduni za nchi hiyo.

Lakini kurudi kwa maonesho ya filamu nchini humo inaelezwa kuwa ni sehemu ya mfululizo wa mabadiliko ya kijamii yenye uhuru unaoingizwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman.


Chanzo: BBC


 
Dah hii black panther imepiga hela sana, mpaka Saudi? duh.
 
infiltration and mind programming, muda sio mrefu waarabu nao watatupa mila na desturi zao wajiunge na mkanganyiko wa kimaadili wa dunia.
 
infiltration and mind programming, muda sio mrefu waarabu nao watatupa mila na desturi zao wajiunge na mkanganyiko wa kimaadili wa dunia.
Nakuunga mkono mkuu au unaweza sema hivi part of NEW WORLD ORDER uislam unapotea saudia unakua uislam wa kinafki
 
Back
Top Bottom