SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,803
- 25,442
Hellow! Natumai mko poa ndugu na mnaendelea kujikinga dhidi ya Corona. Na mimi katika nafasi yangu, naendelea kuwaletea mambo kadha wa kadha kuhusu filamu kama moja ya njia ha kuhamasishana kukaa nyumbani ili kupunguza mizunguko isiyo na ulazima.
Basi leo, tofauti na siku zingine ambazo huwa natuma post ya chambuzi za filamu lukuki, nitaongelea filamu moja tu kwasababu maalum. Kwa zile post zingine tukutane siku kadhaa mbele ntaendelea na session 04.
Naomba fuatana nami mdogomdogo hapa ...
Tunaishi katika ulimwengu gani haswa? Au unaonaje ulimwengu huu? Hili (haya) ni (ma)swali ambalo kila mtu ukimuuliza atakupatia jibu kutokana na aonavyo yeye, na majibu hayo tofauti yanachochewa na imani, malezi na elimu ya mhusika. Kama ilivyo vidole vya mkononi, hatufanani.
Ndo’ maana kuna mmoja aliwahi sema kwa ‘kimombo’, ‘we may look at the same spot but have different vision’ – akimaanisha (kwa utafsiri uso’ sahihi) – tunaweza wote tukatazama eneo moja lakini miono yetu ikawa tofauti.
Mfano, yani mimi na wewe tukamtazma mtu mmoja, lakini mwisho wa siku kila mmoja ataondoka na lake kumhusu mtu huyo. Kuna mwingine atasema la haula! Ni mrembo si kifani, ingali mwingine akisema kama mtu huyu angelilinganisha rangi ya nguo yake na mkoba basi ndo’ angelikuwa ‘bomba’ zaidi.
Nakumbuka siku moja ambayo haina jina kutokana na usahaulifu wangu, mama na baba yangu walikuwa wameketi sebuleni kutazama taarifa ya habari. Ingali wakiwa wanafanya hivyo, walikuwa makini haswa kumtazama mwanamke anayetangaza habari, lakini kama nilivyosema huko awali, wote walikuwa wanatazama kitu kimoja lakini wakiwa na picha ama miono tofauti.
Nililitambua hilo upesi baada ya mama yangu kusema kauli ya kulaumu kwamba kwanini mtangazaji yule alikuwa amerudia kuvaa hereni moja mara mbili? Yani aliivaa hiyohiyo jana yake na pia siku hiyo.
Japo katika siku zote hizo, mama alipata kutazama taarifa ya habari na baba, lakini yeye aliona kitu ambacho baba hakuona. Kwanini? Kwasababu kila mtu alimtazama mtangazaji yule lakini kwa MWONO tofauti. Mwingine akiweka zaidi mazingatio kwenye kitokacho mdomoni, ingali mwinginewe akiweka juu ya kile kinachoonekana.
Si unaona?
Na basi ndivyo inavyokuwa kwenye kila sehemu ya maisha na ndo’ maana katika kila jambo huwa hakuna jibu moja tu linaloonekana ndilo sahihi kupita yote. Mwingine anaweza kuelezea hili kwa namna ile, aonavyo yeye ni sahihi, na mwingine pia akaeleza kwa namna nyingine, aonavyo ni bora. Kwanini? Kwasababu hatufanani kwenye vingi vinavyofanya MIONO yetu pia iwe vivyo hivyo.
Basi juzi, nikiwa katika mapumziko yangu nikapata bahati ya kutazama moja ya filamu mpya ya mwaka huu yenye mahadhi ya kispanyola, kwa jina El Hoyo (The Platform), Filamu hii ikiwa ni chapa ya NETFLIX na imeongozwa na bwana Galder Urrutia. Filamu hii ni nzuri mno, lakini pia kama vile tutofautianavyo miono, kuna watu walioitazama mwanzo mpaka kikomo chake na kuona haifai.
Cha kufahamu ni kwamba, katika utazamaji wowote wa filamu huwa kuna mambo mawili; moja, kuna picha ya nje ya filamu, hii ndo huwa bayana kwa kila mtu atazamaye hata kama ni mtoto, kwani huwa inahusisha yale tu yanayoonekana na macho mawili na kutambuliwa na milango yetu ya fahamu iliyozoeleka.
Pili, kuna picha ya ndani ya filamu, ambapo hapa sasa si kila mmoja wetu huwa anapata kung’amua maana yake. Hapa ndo’ kwenye tatizo. Na kwanini hili hutokea? Mosi, kwasababu tunapuuzia alama na ishara zinazoonyeshwa ndani ya filamu kwa kutozipa mazingatio yanayotakiwa. Pili, hatuchukui muda wetu kujiandaa na kuitazama filamu husika kama vile kufanya ‘kaudadisi’ kidogo.
Naelewa kwanini hili linatokea … watu wanataka kutazama filamu wapate burudani bana si mateso. Au sio? Hawa ndo’ huwa wanaishia kwenye ile picha ya kwanza na kama ikitokea mambo hayaja-flow kama maji ya mto (yani ‘steringi’ ajulikane toka mwanzoni, apate hasira na apambane kumuua adui), hukengeuka na kuishutumu filamu haileweki.
Si kwa ubaya, lakini kuna muda sasa tunakosa ujumbe muhimu sana ambao ulikuwa umelengwa tuupate. Na filamu ni kama fasihi zingine, si kila jambo litaachwa uchi, bali ni juu yako wewe kuzama kwenye uchambuzi ujue nini msanii alilenga., usikute ni ujumbe wa siri! Hahaha (joking).
Sasa tuzame kwenye kitu chenyewe …
EL HOYO (THE PLATFORM) ya 2020.
Mwanzoni mwa filamu hii, tunaona watu wakiwa wanaandaa chakula kwa ustadi mkubwa sana. Kuna mkaguzi, mwanaume mzee (ikimaanisha uzoefu) akipita kukagua hapa na pale kuanzia ladha mpaka harufu kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Na pale jambo linapokuwa halipo vile linavyotakiwa, basi mkaguzi huyu hung’aka kwa msisitizo.
Yote tuyaonayo hapo hayana sauti. Ni kimya tu lakini matendo yakionekana dhalili. Chakula hiki ambacho huandaliwa kwa ustadi, na ni cha daraja la juu kabisa, kinawekwa kwenye meza ngumu, pana na nzito, ambayo hushuka chini. Meza hiyo ndo ‘the platform’ yenyewe.
Huko chini sasa ndo’ kuna tafrani ya nyani shambani. Ni shimo kubwa ambalo limejengwa kushuka chini ambapo ni mbali mno, na katika kila ‘floor’ kuna wafungwa wawili wawili, yani maana yake kuanzia floor namba moja mpaka huko chini kabisa ambapo kuna floor ya mia tatu na kitu hivi! ‘Imagine’ zipo floor mia tatu na ushenzi!
Hivyo ‘the platform’ iliyobeba chakula kile kingi na cha hadhi ya juu inapita katikati ya shimo kubwa kwa mtindo wa kuelea. Inapita kwenye kila floor ambapo inasimama kwa dakika mbili tu, ambapo mtu atakula kile kilichomo hapo, baada ya dakika hizo mbili, the platform inaondoka zake kwenda kwenye floor za chini na chini mpaka mwisho wake.
Sasa shida inakuja wapi? Ni pale ambapo chakula kile kinachowekwa kwenye ‘the platform’ hakifiki chini hivyo kupelekea watu waliopo chini kukaa kwa njaa kiasi kwamba wakilazimika hata kuuana na kulana wenyewe ili wapate kuishi!
Na ipo hivi, yule aliyepo kwenye floor ya juu kabisa, kama vile namba moja, mbili na tatu mpaka sita hivi, wao watakula vinono na vizuri maana bado vitakuwa vimebakia mezani, shida inaanzia hizo floor za chini ambapo wale waliopo katikati kama vile floor namba kumi na kitu na ishirini na kitu hivi, hukuta tu makombo, mikojo na hata vinyesi toka kwa watu waliopo kwenye floor za juu. Lakini nao, sababu ya njaa, hawana budi kula kile kilichopo.
Shida zaidi inakuja kwa wale waliopo floor za kuanzia mia moja huko mpaka huko chini. Wao wanakuwa hawapati kitu kabisa. Wanaishi maisha magumu kupita kiasi ambayo yanawalazimu wafanye chochote kile ili wapate kuishi.
Na utaratibu upo hivi ndani ya shimo hilo, kila mtu hukaa kwenye floor yake kwa muda wa mwezi mmoja tu. Baada ya hapo dawa inapuliziwa, unapokuja kuamka unajikuta katika floor nyingine kabisa. Sasa ni bora uombe ujikute kwenye floor ya juu maana unazidi kukisogelea chakula kuliko ujikute kwenye floor ya chini huko kwenye mapambano na mauaji!
Utaratibu mwingine ni kwamba, huwezi chukua chakula ukahifadhi kwa ajili ya baadae. Endapo ukifanya hivyo, basi joto ama baridi litaongezeka kupita kifani kwenye floor yenu mpaka pale mtakaposalimu amri! … kwahiyo wewe ni kula na uache kila kitu kwenye platform tu!
Na utaratibu wa nyongeza, humo ndani ya shimo watu wanaingia na chochote kile walichopendekeza waingie nacho. Hivyo kuna watu humo ndani wana wanyama kama vile mbwa, wengine wana silaha kama visu, wengine kamba na kadhalika. Kuna jamaa mmoja yeye aliomba kuingia humo na kitabu. Ni uchaguzi wako.
Sasa je ni kwamba chakula hakitoshi ndani ya shimo hilo kiasi cha watu kuuana na mpaka kulana wenyewe? Jibu ni hapana. Ukiwa unaingia katika shimo hili, mlengwa huwa anaulizwa mpaka aina ya chakula apendacho ili kipate kuwekwa jikoni. Na chakula kinachowekwa kwenye ‘The Platform’ ni kingi sana kiasi cha kutosha wote ndani ya shimo, lakini shida inakuja wapi? – tamaa, ubinafsi ulafi, kutojali wengine, roho mbaya na chuki.
Kama kila mmoja angekuwa anakula kile tu anachotakiwa kula na kisha kubakizia wengine, chakula kingemtosha kila mtu lakini haipo hivyo. Wale wenye nafasi ya kula, yani wale waliopo kwenye zile floors za juu, hawawajali kabisa waliopo chini yao. Wanakula kupita kiasi, na mpaka wengine wanatoa haja zao kwenye meza ya chakula ama kupanda kabisa kwenye meza na kukanyagakanyaga chakula ambacho wenzao huko chini wanakingoja kwa hamu!
Wale waliojuu huwatusi walio chini.
Huwaona ni mbwa tu sababu wao wamepata nafasi ya kuwa karibu na chakula. Hula kupita vile wanavyovihitaji na basi hupelekea wengine kufa na njaa, kuingia kwenye vita ya kugombania chakula mpaka kulana wenyewe kwa wenyewe.
Hiyo ndo’ maana halisi ya ubepari (Capitalism), ambapo filamu hii inatuonyesha ni namna gani ulimwengu wa kibepari ulivyo. Namna gani ambavyo kunakuwa na matabaka na yule aliyejuu anapojilimbikiza mpaka asivyovihitaji ingali kuna wengine chini yake wakiwa wanalia na kusaga meno angalau wapate mlo.
Tazama mtu anayemiliki kiwanda, yeye ni bwanyeye mwenye pesa zake ambapo anakula atakavyo, anavaa atakacho na familia yake inapata mahitaji yake kwa raha, lakini wafanyakazi wake wale wanaovuja jasho kiwandani wakishindia kwa siku ujira wa shilingi alfu tatu ama tano pasipo kujali ana familia yenye mahitaji lukuki. Na basi anapojaribu kusema jambo akma kupambana, wanaishia kuonekana wahuni tu na wavivu na wale waliopo juu.
Filamu hii yaonyesha ni namna gani ambavyo rasilimali za dunia zinatosheleza kabisa mahitaji ya binadamu wote. Kila mtu akapata chakula, maji na huduma za kijamii, lakini bado inashindikana, kwanini? sababu ya ubinafsi wa wale walipo juu. Wanataka kula kila kitu, na hata wanaposhiba, wanakanyaganyaga kile kiendacho kwa wale walio chini.
Na kwa sababu wale walipo chini wanapata kidogo mno au kukosa kabisa, hapo ndo’ inapotokea ‘survival of the fittest’ (kudumu kwa mwenye nguvu). Ambapo hiko kidogo kinapiganiwa. Na ikikosekana, wanakulana mpaka wenyewe (a dog-eat-dog society).
Pasipo kujua, Jambo hili linatengeneza chuki ya mduara. Hivyo pale inapokuja kutokea wale walio chini wakija kupanda juu, na wao hawajali tena kuwa wa chini walipitia shida na mateso. Wanatumia fursa hiyo kuwatesa wengine waliopo chini kwa kufanya vilevile kama njia ya malipizi!
Sasa wafanye nini?
Katika filamu hii kuna jamaa aitwaye Goreng ambaye aliingia katika hili shimo na kitabu (hii huonyesha uelewa wake wa mambo). Kwa namna fulani jamaa huyu anataka kubadili mambo ndani ya shimo hili (ambalo ndo huwakilisha jamii yenyewe sasa) kwa kuhamasisha watu waishi kwa ushirikiano na kuwe na ubinadamu (yani sasa ndo’ Ujamaa), lakini mambo yanakuwa magumu sana kwani watu wameshazoea kuishi kwa ukatili na ubinafsi mno!
Jamaa huyu mwenyewe anajikuta kila anapozidi kuishi humu ndani, anaanza kubadilika kuendana na wengine ilia pate ku-survive! Mwishowe anakutana na mtu mwenye angalau mawazo yanayowiana na yeye, jamaa ‘black’, kwa jina Baharat. Jamaa huyo ana hamu sana ya kupanda juu lakini aliishia kushushiwa kinyesi usoni na wale waliopo juu pale alipojaribu kuomba msaada!
Hatimaye anaamua sasa kushirikiana na Goreng, wakitokea kwenye floor yao namba sita, wawe wanasimamia chakula ndani ya shimo kwa kuhakikisha kila mtu awe anakula chakula kinachotakiwa ili na wengine wote wapate.
Mzee, haikuwa kazi rahisi hata kidogo! Kwani majamaa hawa kila walipokuwa wanashuka chini na ‘the platform’ walikuwa wanakumbana na chagamoto za wafungwa wengine wabinafsi wenye njaa kali wasiojali wengine hivyo wakawa wanapambana na kupambana! Na hata kufikiwa kuwaua wale wazandiki (hapa ndo tunaona picha ya Ujamaa na namna gani inavyokumbana na changamoto za mauaji pale inapotumika. Sharia zake ni kali sana zenye kutaka kujitoa).
Na majamaa hawa wawili, Goreng na Baharat, lengo ni chakula kibaki ili kikirudi juu kiwe ni ujumbe kwa walio juu kwamba wafungwa hawa wameshastaarabika!
Je ujamaa wao utafanikiwa? Na kama chakula hiko kisipobaki kama walivyopanga, watatuma ujumbe gani kwa wale walio juu kuonyesha ustaarabu wao? Ukitazama utaone vema… ni filamu nzuri mno isiyoisha hamu.
Lakini zaidi ikituonyesha uhalisia wa dunia yetu tunayoishi juu ya namna gani pale tupatapo nafasi ya kuwa juu ya wengine, tunavyotumia nafasi zetu hizo kutapanya, kufuja na kujilimbikiza pasipo kujali tunaumiza wangapi walio chini yetu na pasipo kujali kabisa (ama kusahau) ya kwamba maisha yanaweza kubadilika muda wowote ule kwa yule juu kuwa chini, na wa chini kuwa juu yetu!
Nakusihi ipe muda filamu hii.
Pengine unaweza kupata mwono wa zaidi.
Enjoy!
IMEANDALIWA na,
Steve BM,
A Freelance Journalist &
A Literary and Movie critic.
0685 758 123 (Whatsapp tu).
Sent using Jamii Forums mobile app