FikraPevu: Polisi aliyefyatua bomu lililoua mwandishi akamatwa, kushitakiwa kwa mauaji

POLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu limefahamishwa.

Taarifa za kutoka Iringa zimeeleza kwamba kushitakiwa kwa askari huyo, kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao unathibitisha pasi shaka kwamba bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha mwandishi huyo wa habari.

Imethibitishwa kwamba kilichousambaza mwili wa mwandishi huyo ni bomu maalumu linalorushwa kwa kutumia bunduki kwa nia ya kusambaza watu waliokusanyika kwa nia ya kutenda uhalifu na lilirushwa kwa karibu mno kinyume cha masharti na kanuni za matumizi yake.

Bomu hilo hutakiwa kurushwa kutoka umbali wa mita kati ya60 na 80, wakati askari huyo alilirusha kwa karibu mno na akimlenga mwandishi Mwangosi.

Katika tukio hilo, bomu hilo liliusambaratisha mwili wa Mwangosi na kumjeruhi ofisa mmoja wa polisi ambaye anaelezwa kutaka kumsaidia mwandishi huyo ambaye alikua akipigwa na polisi wenzake.
Marehemu Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika kijijini cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika tukio ambalo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakifungua tawi la chama chao, huku Polisi wakitumia nguvu kubwa kuzuia uzinduzi wa tawi hilo.

Source: Fikra Pevu | Kisima cha busara!

Litakuwa aibu kweli kwa yule jamaa aliyesema marehemu alijilipua. Shame to you narrow minded CCM leader at UDSM
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.

swali la kujiuliza ni kwamba, hizo tume zitafanya kazi gani? Kama makosa yameshaonekana na muhusika amekamatwa na kushtakiwa, tume zinachunguza nini tena? Ni mpango wa kupeana hela za posho tu!
 
RPC wa iringa ni mwongo mkubwa na ametumwa na wanasiasa
pili,kama suala lipo chini ya tume mbona ccm wanawanyooshea vidole chadema?
weshatoa hukumu tume la nini sasa

awa makenge kweli
 
Jamani tuache kudanganyana. Hakuna haja ya kuwa na Tume wakati serikali inadai mikusanyiko/maandamano si halali lazima yazuiwe. Sasa kama walienda kuyazuia kwanini wanaunda tume na kupoteza rasilimali chache za Taifa.
 
halafu jambo jingine watu wanafikiri kwamba kwa kuipenda kwetu au kuishabikia cdm wanahisi tunaipenda sana kumbe hii inasababishwa na mfumo kwamba hatuna njia ingine mbadala ya kukabiliana na madaraka yao zaidi ya kuutumia utaratibu huu huu uliowekwa.lakini pointi yangu ni kwamba watanzania tuwe na utaratibu,uwezo na tabia ya kuondosha kitu ambacho tayari tumekiona hakitufai.hii inamaanisha kwamba hata kama cdm wataharibu maana na wao ni binaadamu tutakuwa tumeshajenga uwezo na uzoefu wa kubadili palipo na uozo tofauti na sasa ambapo watu wanauurunda sisi tunanung'unika kipembeni.ila yote kwa yote yana mwisho haya hata kama utakuwa mbaya iwe kwetu au kwao lazima mwisho utakuwepo tu na naamini mungu hawezi kututupa maana ni wetu sote.
Nimekuelewa mkuu... mimi nilikuwa natoa tahadhari tu hasa katika haya mabadiliko tunayoyataka kwa sababu tusijejikuta tumebadilisha majina ya watu tuu halafu kila kitu kikawa bado kiko vilevile bado hatutakuwa tumefanya kitu. Wanasiasa hutofautiana sana katika kauli lakini malengo na matendo yao huwa karibu sawa. Shida ya watanzania tuliowengi ni kubadilisha mfumo wakuendesha nchi (katiba)... uwe wa uwazi zaidi na usiwe wa kikandamizaji hapa.... kuwepo na usawa na haki katika ugawanaji ya keki ya taifa...sio mbunge analipwa milioni 10 halafu mwalimu analipwa laki3.....hatuujui mshahara wa raisi halafu tunateta kuhusu utajiri wa familia yake..hapa tutakuwa hatumtendei haki mheshimiwa... ninajua hapa ninaweza kutofautiana na wengi katika hili...
Tuanze sisi wenyewe majumbani kwetu tuwaeleze wanafamilia vipato vyetu..twende vyamani tujue mishahara ya viongozi wetu kwa uwazi kabisa kwani sisi ndiyo tunaowalipa..kisha tuingie serikalini tujue vipato vyao pia.... sisi ndiyo walipa kodi
Lakini tukisema tushinde mabarabarani kutwa tukiimba na kucheza huku tumevalia mashati ya kijani au suti za kaki bila kujua kwamba tunahitaji kujenga mfumo utakaowabana wanasiasa juu ya matumizi ya madaraka na rasilimali zetu basi haitatusaidia lolote kwani tutakuwa tunabadilisha mazimwi tu.... Tutabaki tukisema yana mwisho haya na Mungu wa kwetu wote huku tukiendelea kuzeeka.....
 
Tayari dagaa anatolewa kafara huku wakubwa walio suka mpango mzima wa kukidhoofisha CHADEMA wakiendelea kupeta maofisini akina Nape, Nchimbi, Mwema, Kamhanda na wengineo
 
Hahahaa.sasa hapo ndipo utakapojuta kujifanya kwamba wewe ndie unauchungu sana na ccm kuliko hata wenye ccm wenyewe.ukajifanya kuwa ccm ni mama yako jk ni baba yako.ukaamuwa kufanya kazi kwa kutii amri za wakubwa wako bila kuchanganya na akili zako.sasa hili ni lako mke wako, watoto wako na wazazi wako umewaacha wanateseka.walio kutuma hutawaona hili ni lako baba uliokuwa unawapiginia hawooo.jk miguu juu na riz,Mwema miguu juu na familia yake,Nchimbi miguu juu na familia yake,Nape miguu juu na familia yake.Hapo ndipoutakapo wakumbuka walimu wako walio kufundisha kuwa usifanye kazi kwa kufuata amri tu.Tumia na akili zako.
 
Wana JF je kila tume inapoundwa kuna malipo yoyote kwa watendaji wa tume husika ? Isije ikawa ni kamradi fulani ,watu wakatumia matatizo kama advantage ya kuishi?
 
POLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu limefahamishwa.

Taarifa za kutoka Iringa zimeeleza kwamba kushitakiwa kwa askari huyo, kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao unathibitisha pasi shaka kwamba bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha mwandishi huyo wa habari.

Imethibitishwa kwamba kilichousambaza mwili wa mwandishi huyo ni bomu maalumu linalorushwa kwa kutumia bunduki kwa nia ya kusambaza watu waliokusanyika kwa nia ya kutenda uhalifu na lilirushwa kwa karibu mno kinyume cha masharti na kanuni za matumizi yake.

Bomu hilo hutakiwa kurushwa kutoka umbali wa mita kati ya60 na 80, wakati askari huyo alilirusha kwa karibu mno na akimlenga mwandishi Mwangosi.

Katika tukio hilo, bomu hilo liliusambaratisha mwili wa Mwangosi na kumjeruhi ofisa mmoja wa polisi ambaye anaelezwa kutaka kumsaidia mwandishi huyo ambaye alikua akipigwa na polisi wenzake.
Marehemu Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika kijijini cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika tukio ambalo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakifungua tawi la chama chao, huku Polisi wakitumia nguvu kubwa kuzuia uzinduzi wa tawi hilo.

Source: Fikra Pevu | Kisima cha busara!
Mkuu Fikkra Pevu ahsante kwa taarifa hii ya kuhuzunisha, cha msingi Polisi wamkamate huyo mkuu wa Polisi aliyetoa amri ya kuchukua silaha na magari kwenda kuzuia CHADEMA isifungue matawi vijijini!!! Maana chanzo cah mauwaji ni Polisi kuzuia shughuli za chama cha CDM kwa amri ya chama tawala cha CCM!!! Hakuna haja ya kuunda tume viongozi waliohusika wakamatwe wakajitetee mahakamani kwa mauwaji!!!!

Kama huo ndio mpango wao basi wamechemsha kabla ya utekelezaji wa mpango huo.
Pressure imekuwa kubwa kwa serikali hadi inaamua kujichanganya, kitendo cha kumshitaki muuaji tayari ni ushahidi tosha kwamba wahusika wakuu wa vurugu pamoja na mauaji ni jeshi la polisin likishirikiana na ccm na serikali yake.
Mkuu Mwita kwani huyo polisi akishitakiwa si atatoa ushahidi kuonyesha waliomtuma??? Mbona safari hii jamaa wanababaika saana wanajifunga kamba wenyewe!!!!
 
jina la huyi askari pamoja na cheo chake bila kusahau namba yake vipo wazi au ndio changa la macho?

Tuwe makini kwenye hili maana ni kama wanajihukumu wenyewe!Hawashindwi kuchukua mhalifu wa siku nyingi gerezani akalipwa apandishwe kizimbani na kutudanganya wamemshtaki polisi!!!Shame Tanzania!
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.

kama kawaida kitendo cha kupelekwa mahakamani .hatutaruhusiwa kuzungumzia tena .kwakuwa kesi hiko mahakamani .na mnavyojua tena kesi ya murder tz inawezachukua ata miaka 3 .ndio imeshatoka hiyo ikirudi ina pancha .muhanda ,mwema ,nchimbi wameshastaafu.
 
Na hii yaweza ikawa janja nyingine ya polisi kuja na tamko:"Suala hili liko mahakamani.Halipaswi kuzungumzwa nje ya mahaka kuanzia sasa..."
 
Haya, yaleyale ya Dr. Ulimboka ya kupeleka mtu mahakamani kuzuia majadiliano yasiendelee. SHAME ON THEM,GOD WILL EXPOSE EVERYTHING ONE DAY.
 
.
Afadhali wewe umeliona mkuu. Mabadiliko ya nchi yetu Mungu anasimamia kipengele hichi kwa wasio haki dhidi ya wenye haki Isaya 54:17.
Hakika yake ndimi za hawa wadhalimu katika vyomba vyao vya siri, zitageuzwa kuwa hatia kwa hukumu yao.
.

Hii ni Amina na Kweli, Mh. Mbowe aliwahi kusema akihutubia Arusha kuhitimisha kampeni za 2010, kuwa Mabadiliko yanayojitokeza sasa kwenye nchi yetu si ujanja wa Chadema, Mbowe wala Slaa, ni matokeo ya maombi na vilio vya watanzania wanaotaka haki itendeke katika taifa lao!Nilimkubalia Mh. Mbowe bila wasiwasi. Chadema hawakuwa na ujanja wa kukwepa huu mtego muovu wa serikali ya CCM! Ni Mungu Mwenye amewanasua!
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.
Tume kazi yake itakuwa ni kuongeza eneo la uchunguzi, kwa sababu yenyewe itafanya kazi kutokana na hadidu za rejea ikiwa ni pamoja na kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya waandishi wa habari na jeshi la polisi mkoani Iringa, kwa nn mahali pote ambapo Kamanda Kamuhanda amekuwa akifanya kazi kumekuwa na mauwaji yanayosababishwa na polisi na vitu vingine ambavyo vitahusisha kundi kubwa zaidi kuliko mtu mmoja.
 
Kumshitaki mtu mmoja kwenye issue kama hii ni kama kukata majani ya magugu (badala ya kungoa gugu lote) ukidhani utamaliza magugu..

What about kiongozi wa huyo mtu.., what about mtu aliyemtuma.., what about mtu aliye-issue hayo mabomu akijua fika ni ya kutumia kwenye umbali mrefu wakati akijua watu watakuwa karibu ?

Issue kama hii inabidi hadi watu wa juu kuwajibika (after all an innocent person life has been lost).., hapa haki inabidi isitendeke peke yake bali ionekane kwamba imetendeka...,
 
Back
Top Bottom