M.E.M.A
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 1,373
- 472
Miaka ya nyuma nilikuwa napenda kucheza soka (japo sasa nimelihamishia kwenye playstation). Naenda kazini na kabag kangu ka vifaa vya kuchezea. Natoka kazini napita uwanjani kisha ndio nielekea nyumbani.
Kipindi hicho pia nilikuwa na mpenzi. Tulipendana sana, na mbali ya kuwa mpz akawa rafiki yangu mkubwa. Na hata nikiwa kiwanjani alikuwa anakaa pembeni anaangalia mazoezi au mechi.
Siku zilivyozidi kwenda akaanza kuniambia hapendi kuniona nacheza mpira na hapendi kabisa mpira. Hii ilinishangaza kidogo na nikakosa cha kumwambia. Nikajua labda anatania...ila aliendelea kusisitiza. Mi nikamuambia mbona ni kitu ninachokipenda sana. Na hata hivyo huwa nacheza kwa kupenda na pia kwa ajili ya mazoezi. Akaniambia nitafute tu mazoezi mengine kwa sababu katika hili hatakuwa tayari kuendelea na mimi. Basi nikamuambia nitaacha, japo siku moja moja nilikuwa nachepuka. Siku moja nikiwa nimechepuka akanipigia simu. Na kama ujuavyo huwezi kucheza na simu mfukoni..kwa hiyo haikujibiwa. Baada ya mazoezi nikaona missed calls kibao. Nilivyompigia ikawa ugomvi..na mimi kwa hasira nikamuambia 'i need a woman mature enough to know, one can not have a cellphone in playground'. Akakata simu..ila baadae tukawekana sawa.
Basi kwa kumpenda nikaweka habari za mpira pembeni..nikanunua playstation. Hapa nako ikawa tabu..malalamiko kibao kwamba simpi muda wa kutosha. Basi nikahamishia game kwenye computer ya ofisi. Hapo sasa nikawa na kigezo cha kwamba kazi nyingi..ili tu nipate muda wa mimi kufanya nikipendacho.
Kukata story ni kwamba mwisho wa siku tuliachana kwa kigezo tu kwamba simjali. Siku za karibuni hapa amekuwa akinipigia pigia kuniuliza...niko wapi?, nafanya nini?, nitapata muda wa kumtembelea au yeye aje kwangu?..na nimekuwa namkwepa kadri ya uwezo wangu.
Ninachojiuliza ni
1. nimeacha kucheza hadi sasa nimekuwa manyama uzembe, nikiruka tu hata kamba misuli inabana. Nimeacha na vingine vingine ili tu nimpendeze ila mwisho wa siku nikaachwa.
2. Ukiwa na mpenzi ina maana hutakiwi kuwa na muda wako mwenyewe wa kufanya yako?