Fikra Pevu: Hatutaki Tena Hekaya za Alinacha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fikra Pevu: Hatutaki Tena Hekaya za Alinacha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, May 8, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  May 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hatutaki Tena Hekaya za Alinacha

  Mwezi wa kumi (10) Watanzania wenye umri usiopungua miaka kumi na nane (18) watapiga kura kuchaguwa Rais na wabunge kupitia vyama vyao wanavyo viamini kuwa vikichukuwa madaraka vitawakomboa kutoka kwenye makucha ya ufukara na umasikini.

  Kupiga kura kuna umuhimu wake mkubwa, kwa sababu ni siku ambayo utakayo wapa wanasiasa maisha yako ya miaka mitano ijayoÂ…

  Wapo watu wanasema kwamba walionewa, kupuuzwa na kunyonywa kwa sababu ya unyonge wao. Kwahiyo, ili kujikomboa ni lazima kwanza waondokane na unyonge huo.

  Kwa wale wenye kuamini Mwenyezi Mungu, watakubaliana nami kuwa Binadamu kabla hata hajaumbwa ameambiwa kwamba yeye anakuja kuwa Khalifa. Msimamizi wa dunia kwa niaba ya Mwenyezi Mungu. Na ili alitekeleze jukumu hilo, vitu vyote vikadhalilishwa kwake. Avitumie kwa manufaa yake.

  Kwahiyo, kwa asili yake Binadamu si mnyonge wala Mwenyezi Mungu hajampa sifa ya unyonge. Kule kuikubali kwako kupiga kura ndio ukombozi wenyewe.

  Tusikubali kupigiwa magoti tena na wale ambao tunajuwa kabisa kwa miaka mitano iliyopita hawakuweza kutufanyia lolote la kimaendeleo zaidi ya wao kulala bungeni na kupitisha miswada ya kikandamizaji.

  Dalili ya watawala walioshindwa kutawala lakini bado wapo madarakani ili kusogeza siku na kuingoja rasmi siku ya kuondoka kwao, ni "uwongo". Ukiona wameanza kusema uwongo mweupe na hawawaambii watawaliwa ukweli, elewa wazi kuwa si kwamba ukweli haupo bali ukweli wa kuwaambia wananchi upo isipokuwa kinachokosekana hapo ni ile Moral authority au sheria ya rohoni, kitu ambacho ni muhimu sana kwa utawala na uendeshaji wa nchi.

  Tanzania ni nchi ya amani, wanachi wake wengi ni wenye kuamini imani tofauti tofauti na wameishi kwa miaka mingi kwa maelewano makubwa. Tanzania ni nchi katika nchi chache duniani iliyoweka msingi madhubuti wa kuishi pamoja watu wa dini, makabila mbalimbali katika hali ya kukubali kutokubaliana.

  Lakini vyote hivyo havizuii wala havita himili wimbi la mabadiliko kutoka kwa wananchi hasa wazalendo, hapo watakapo sema "utawala huu sasa basi", kweli itakuwa basi. Makaburu walipiga, waliua, walitesa na kufunga watu kwenye jela zao lakini wapi, hakuna kilichowazuia wananchi wasiusukumie kaburini utawala waliouchukia na kuchoka nao.

  Mtawala akishachokwa njia pekee iliyo bora ni kutoka madarakani kwa amani badala ya kungoja kusukmwa na hasira za wataliwa hadi mtu ang'ang'anie kubaki madarakani kwa gharama zozote.

  Hatutegemei tena hao watakao kuja kuomba kura wakisaidiwa na Masheikh na maaskofu uchwara watuletee ngonjera, visa vya Abunu wasi, mashairi na ngonjera za kusifiana n.k.

  Huu ni wakati wenye matukio na masuala maalum na muhimu kwa Watanzania na mustakbali wao katika nchi hii ya Tanzania.

  Dalili ya kwanza ya utawala ulioanguka hali ungali madarakani, ni dalili za "ukatili" dhidi ya wananchi wake inaowatawala ni wazi kwamba tunaweza kuutafsiri ukatili huo kama hatua ya mwisho ya kutapatapa ya mtawala mfanya maji ambaye analazimika kushika maji hayo hayo yanayomuua.

  Sasa hivi mtu anayeijia Tanzania kwa nguvu ya fedha ni sawa na ajaye na nguvu ya Mungu ambayo mambo yote yawezekana na hakuna lisilowezekana. Kwa nguvu ya fedha mtu anaweza kumnunua Afisa yeyote. Nguvu ya fedha inawezesha lolote hata kama litakuwa tendo la uhaini wa hali ya juu wa kuangamiza nchi.

  Hii ni kwa sababu watu sasa wanajali maslahi ya muda mfupi na faida za papo kwa papo. Hali hii imetokana na watu kukata tamaa ya maisha na kuamua kubangaiza na neno ambalo kwa lugha nyingine linatiwa "survaival".

  "Survival" ni maisha yaliyokusudiwa wanyama siyo watu. Sisi wanadamu tulikusudiwa "tuishi" yaani "life" na siyo "Survival". Serikali ndiyo iliyopindua maisha ya Mtanzania na kuyateremsha chini hadi kuwa sawa na maisha ya Sungura aliyeko mbuga za wanyama ambaye kuishi kwake kunategemea ujanja wake wa porini na chenga nyingi.

  Tunataka uchaguzi huu huwe wa amani na salama kama vile Watanzania wenyewe walivyo watu wa amani na salama, hatutategea tena kuyarejea yale ya miaka ilopita ya kusimamiwa na askari wenye silaha za kivita.

  Kwenye uchaguzi huu hakuna kusikiliza kasisi, askofu wala sheikh, tunataka kila mgombea kuhojiwa kwenye hadhira iliyo wazi. Na atufahamishe kwanini anataka kugombea na kama anakuja tena kwa mara nyingine basi ni wajibu wetu kumuhoji ametufanyia nini mpaka aje tena kutuomba kurejea kwenye madara tulompa miaka mitano ilopita. Na yule ambaye tunajuwa wazi kabisa akujishughulisha na masuala ya walalahoi basi huyo ni wa kupuuzwa tu bila kujali jina, cheo na nasaba yake.

  Watanzania tayari tuwamoja, Kuwepo kwa Jumuiya, vyama na Taasisi nyingi sio alama ya kukosa umoja au ugomvi. Ni vituo vya kazi, lengo letu likiwa moja, kuendeleza nchi yetu.

  Tusingependa kusikia katika chaguzi hii zile kampeni za chuki na majigambo kwamba eti hatuna umoja, hatuna uongozi, tusigombane, tutumie hekima kwani ardhi yenye rutuba tunayo, watu wa kuendeleza nchi tunao na pia naamini kuwa viongozi wazuri tunao, kilicho baki ni jukumu letu sisi Watanzania kuchaguwa wale ambao watatuvusha kwenye janga ili la kiuchumi bila kuangalia Dini, Kabila au chama cha siasa.

  Tutegemee vile vile kwamba katika chaguzi hizi, Watanzania watachagua viongozi wao kwa amani, bila ya kutiana majeraha tena kwa kukejeliwa, kukashifiwa, au kusababishiwa vilema vya maisha na mama zao kudhalilishwa.

  Chaguzi zilizopita tulikuwa tunaulizwa shida yenu nini, matatizo yenu nini. Sasa baada ya yote haya, Watanzania hawategemei kuulizwa tena "shida yenu nini".

  Shida yetu dhulma iondoke. Shida yetu mafisadi wakamatwe... wafikishwe mahakamani... Shida yetu... !

  Kusiwepo na hila za kumtangaza mshindwa badala ya mshindi au kutoa fursa kwa chama fulani kujipigia kura kinyume na utaratibu na kura hizo zikajumuishwa na zile za halali, kuwepo na uwazi katika kupiga na kuhesabu na kutoa matokeo, pia kuwepo uhakiki wa idadi ya waliojiandikisha utakaosaidia kuwajua vyema wapiga kura wote.

  kwani zoezi hilo litaondoa wasi wasi walionao baadhi ya watu kuhusiana na idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura. Kufanya hivyo kutaondoa dhana kwamba huenda kulikuwa na ongezeko la kimya kimya la idadi ya waliojiandikisha kupiga kura katika idadi iliyotangazwa na Tume...

  Katika kipindi hiki kilichobakia Tume iwaagize watendaji wake kwa kuvishirikisha vyama husika kuhakiki idadi, gharama si kitu mbele ya suala nyeti kama hilo ambalo pindi ikijitokeza dosari hugharimu maisha ya watu na kusambaratisha nchi.

  Tume itakuwa imetimiza wajibu ambao historia ya nchi hii itaurekodi iwapo itajiepusha na harakati za wachache wanaotaka kujitwalia nyadhifa kinyume na ridhaa ya walio wengi.

  Ni jambo la kushangaza kumuamuru mtu atumie dakika moja kujiamulia namna atakavyoishi kipindi cha miaka mitano, huyu ndiye atakaevuna matunda ya uamuzi wake wa kura kwa miaka hiyo kama ni matatizo atakumbana nayo yeye na kama kinyume chake ni yeye kwa nini asitumie siku nzima au hata mbili kwa ajili ya hiyo",

  Aidha tunavitaka vyombo vingine vinavyolinda usalama wa nchi kutotumika kufanya hila kukisaidia chama fulani kishinde badala yake isiwe tu viseme viko pembeni na vitakuwa tayari kumtii mshindi atakayetangazwa bali vihakikishe uadilifu unakuwepo katika kupiga kura na kutangazwa matokeo.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,525
  Trophy Points: 280
  Hekaya ni za Abunuwas ama Alfu Lela Ulela, cha Alinacha ni Kisa tuu, ambacho ndicho kitakachotokea October!.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  May 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nimekusoma mkuu Pasco!
   
 4. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kaka summary, asante
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  May 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni kitu gani ambacho ujakielewa mkuu, mpaka utake summary!?
   
 6. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  You guys prepare for a surprise coming from the 20million voters and thereafter democracy will have spoken tusianze kuremba kwa sababu watu milioni 20 siyo wajinga
   
Loading...