WanaJf,
Mshkaji wangu anaomba ushauri kwenu wa dhati juu ya tatizo lake hili
Ana mchumba ambaye hawajaanza kuishi bado pamoja sasa shida inakuja wapi huyo mchumba wake wa kike ana rafiki yake mwingine wa kike pia na hata kazi wanafanya jirani pamoja mchumba wake na rafiki yake huyo.
Sasa kuna kijitabia ambacho wamekianzisha hawa watu namaanisha mchumba ake na huyo best ake
yani wanaweza panga ndani ya week hii wanaenda kulala kwa rafiki yake halafu week ijayo wanaenda kulala kwa mchumba wake na sababu ya maana haijulikani yani wanaenda kulala tu.
Na wakati mshkaji ananambia kama kodi analipa fresh ili mchumba ake apate mahali pa kulala salama kabisa. Sasa ndo anajiuliza ni kwanini kitabia hiko hakikuonekana mwanzoni mpaka kije kionekane sasa hivi na wao wanaenjoy kabisa na timetable wamejipangia kabisa kuwa week hii kwenu week hii kwetu.
Ndo mshkaji anawaza au wanapolala pamoja kuna kitu watakuwa wanakifanya n wanaenjoy (usagaji). Maana hawaelewi kwanini wafanye hivyo wakati kila mtu ana kwake na maisha yake.Kingine ni kwamba kila mchumba wake anapoenda kulala kwa best ake huyo ni lazima amtaarifu mshkaji wangu kuwa Leo akalala kwa Fulani.
Anaomba ushauri wenu wa dhati wa kuu kama ni namna ya kufanya uchunguzi, msaidie maana anawaza sana kuwa yawezekana wameanzisha kautaratibu ka kusagana na kameshawakolea.
Ikumbukwe kuwa huyo best ake pia ana mchumba wake
Karibuni kwa ushauri