Mjusi Sharobalo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2025
- 7,442
- 12,710
Siku zote kabla ya kujifunza kuheshimu watu, jifunze kuheshimu maneno yanayotoka kinywani mwako. Manano yetu yanabeba hatima na msingi mkubwa wa maisha yetu.
Watu wengi hufikiria kumchukiza mtu ni hadi utende kwa vitendo, husahau hata maneno madogo yanaweza kuwa na madhara makubwa katika maisha yao. Mfano mzuri ninaoweza kukupatia hapa, chukulia neno "Utanifanya nini?
Ni neno jepesi lakini lina uzito ndani yake na hatima kubwa. Neno kama hilo unapomwambia mtu, hatakama hakuwa na nia ya kufanya jambo lolote baya kwako, lakini atatafuta sababu ya kufanya hivyo, kukujibu anao uwezo wa kukufanya chochote.
Siku zote jifunze kumheshimu kila mtu na ujiwekee mipaka ya maneno yako. Kumbuka neno UTANIFANYA NINI, limeondoka na uhai wa watu wengi au kuachiwa maumivu ya kudumu maishani mwao. Asante...