babilas25
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 483
- 361
Heshima kwenu wanabodi.
Kuna wakati maneno ya wahenga huwa yanatimia katika maisha yetu ya kila siku, Msemo wa "Fikiri kabla ya kutenda" kwangu umetimia,
Nilikua nikifanya kazi katika kampuni X kwa zaidi ya mwaka1 na nusu kama msimamizi wa mradi wa ufugaji samaki. Wakati nikiwa kazini nilitembelewa na mgeni alikuja kuona mradi ule na kutaka kujifunza, alivutiwa na mradi ule akaomba nikutane nae nje ya eneo la kazi ili nimshauri zaidi, tukapanga siku tukakutana nikamshauri, akasema analo eneo lake kanda ya ziwa anataka kuwekeza huko hivyo anahitaji mtu committed anaeweza kujisimamia na akafanya kazi kwa ufanisi, akasema itachukua kama mwaka 1 zaidi kutengeneza miundo mbinu kwenye eneo hilo ili kazi ianze, akaniuliza kuhusu elimu yangu, nikamwambia nina Diploma, akasema kwanini hujaendelea na Degree? Nilimwambia niliwahi kuomba na nikachaguliwa kujiunga na chuo lakini sikufanikiwa kupata mkopo hivyo nikashindwa kuendelea na masomo.
Hapo ndipo akapata mwanya wa kunirubuni, aliniambia kama nipo tayari yeye anifadhili niendelee na masomo wakati huo yeye anaendelea kutengeneza miundo mbinu ili nikimaliza chuo tuanze kazi, atanipa mkataba wa miaka 5 ili awe anakata hela yake,
Kwangu niliiona kama fursa ya kufikia ndoto zangu nilikubali, na ilipofika August niliandika barua ya kuomba kuacha kazi kwa mwajiri wangu, aliipokea kwa masikitiko makubwa na akaniomba walau ikwezekana shule niende mwakani lakini sikukubali akajaribu pia kutumia watu wa karibu wajaribu kunishawishi ila haikusaidia kubadili msimamo wangu, mwajiri alijibu barua yangu akaniruhusu kuacha, mda ulipofika nikaacha kazi, ili nikafanye maandalizi ya kurudi chuo.
Baada ya kua nimeacha nilimjurisha mfadhili wangu kua tayari kazi nimeacha tena mapema ili nifanye mandalizi ya kutosha alinijibu kua tungeonana baada ya wiki 1 maana alikua na safari ya kwenda ughaibuni, wiki 1 baadae nikamtafuta kwa njia ya simu hakua anapatikana wiki ya 3 vivyo hivyo, nikamtafuta kwa njia ya WhatsApp akawa hapokei nikituma SMS hazijibiwi, mwisho akaniblock mpaka mda huu nipo njia panda kazi nimepoteza kwa tamaa ya chuo, chuo nacho sijaenda mfadhili kayeyuka
Nashindwa tena kurudi kwa mwajiri wangu wa zamani nawaza nitakwenda kumwambia nini tena ili anielewe na aweze kunilejesha kazini, hapo ndipo nakumbuka "Tamaa mbele mauti nyuma"
"Unataka kupata ushauri juu ya ufugaji samaki hatua kwa hatua au partnership kwenye project ya ufugaji Samaki"
+255764123459/+255783686643.
Sent using Jamii Forums mobile app