Fikiri kabla ya kuchukua hatua!!

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Baba ameamka Asubuh akijiandaa kwenda kukutana na mfanyabiashara mkubwa ili kufanya mikataba ya Kibiashara.Akiwa kashavaa
nadhifu kabisa mkewe akamuomba wanywe chai kabla ya kuondoka japo alikuwa ni haraka lakin kwa Shingo upande kakubali.

Wakiwa Mezani Baba, Mama,na mtoto wao mdogo ghafla mtoto akagonga kikombe na chai ikamwagikia kwenye Shati nadhifu ya Baba. Baba kwa hasira akaamka akamshika mtoto na kuanza kumpiga Mama kuona vile akaingilia kati ogomvi ukawa mkubwa wakatukanana namwisho wa siku Kila mtu akaondoka kivyake huku Baba akibadilisha shati na kuvaa lingine.

Kuja kutaamaki mda umeenda inabidi aiwahi appointment yake na mfanya biashara,ikabidi atoke na gari kwa kasi sana kufuatia Hasira alizokuwa nazo na stress za kuwahi mwisho wa siku akajikuta anamgonga mtembea kwa miguu na kumuua hapo hapo.Baada ya kumalizana na trafick anafika ofisin kampun inamfukuza kazi kwa kusababisha kukosa dili ya Mamilioni.

Sasa angalia jinsi maamuzi ya dakika kadhaa yanavyoweza kukuharibia Maisha yako,jamaa kazi kapoteza, mtoto anamchukia, Mke wapo kwenye ugomvi na kesi ya mauaji juu. Angetumia busara ya kumwambia mkewe njoo ufute hapa mezani na yeye kwenda kutafuta shati kabatini bila malumbano haya yote yasingetokea.

Please kabla Hujaamua kufanya jambo lolote jaribu kufikiria matokeo yake kwanza, siku zote maamuzi yetu kimaisha ndio yanayokuja Kuturudisha nyuma na kutufanya tujutie Baadae.
 
nimeipenda mkuu ni fundisho pia thnx


Unaona hiyo kali kuhusu uamuzi wa haraka haraka? Fikiria hii, tena fupi tu;

Baba anaamua kutembea na changudoa
Anajiuliza kama atumie kinga au la
Anaona asitumie ili apate hisia zote
Siku mbili baadaye anajituliza tena kwa mke wake mja mzito
Baada ya wiki anaambiwa yule changudoa ni muathirika
 
:shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth:
 
Unaona hiyo kali kuhusu uamuzi wa haraka haraka? Fikiria hii, tena fupi tu;

Baba anaamua kutembea na changudoa
Anajiuliza kama atumie kinga au la
Anaona asitumie ili apate hisia zote
Siku mbili baadaye anajituliza tena kwa mke wake mja mzito
Baada ya wiki anaambiwa yule changudoa ni muathirika

Dayuuuuum! hii kali kuliko...:tape2:
 
khaaaaaaaaa!! Yani! Mh ! So sad mskin mumy na mwanae tumbon lol!
 
Baraka za familia zinasaidia sana katika kuongeza mafanikio nyumbani.
 
Unaona hiyo kali kuhusu uamuzi wa haraka haraka? Fikiria hii, tena fupi tu;

Baba anaamua kutembea na changudoa
Anajiuliza kama atumie kinga au la
Anaona asitumie ili apate hisia zote
Siku mbili baadaye anajituliza tena kwa mke wake mja mzito
Baada ya wiki anaambiwa yule changudoa ni muathirika

dah! Hii nayo... Tamaa mbele mauti nyuma.
 
Kweli hasira hasara. Tunapaswa kuishinda hasira , watu wengi wamekosana kwa vitu vidogo tu . Ukiishinda hasira utapunguza ugomvi , heri kua mpole na kukubali nafasi ya unyonge mara nyingi inalipa lkn hapa inategemea ni ktk nini. Kabla ya kuchukua hatua daima hakikisha unajua potive na negative effects ya hicho kinachokukabili.
 
Back
Top Bottom