Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 332
- 702
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limesitisha kuiondolea uanachama Israeli na badala yake imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ubaguzi yaliyotolewa dhidi ya maofisa wa Soka wa Palestina.
Jopo kuu la FIFA linalosimamia utawala litachunguza “ushiriki wa timu za Israeli zinazodaiwa kuwa katika eneo la Palestina,” bodi ya FIFA ilisema.
Maamuzi hayo yanakuja zaidi ya miezi minne baada ya maafisa wa Palestina kuitaka FIFA kuisimamisha uanachama Israeli, wakiweka bayana “ukiukwaji wa sheria za kimataifa” uliofanywa na Israeli huko Gaza.
Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, Shirikisho la soka la Palestina limekuwa likiiomba FIFA kuchukua hatua dhidi ya shirikisho la kandanda la Israeli kwa kujumuisha katika ligi yake, timu zinazotoka Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Kulingana na jopo la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa, klabu zipatazo nne zinacheza katika makazi ya Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, huku tisa zikicheza mechi zake za nyumbani kwenye makazi hayo.
Wataalamu hao wanadai kuwa, kitendo hicho kinahalalisha uwepo haramu wa Israeli katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu.