FIFA Confederations Cup Brazil 2013

FIFA Confederations Cup Brazil 2013

JUVE2012 kishakuja kujitetea kwa sauti ya upole kabisa akiwa na majeraha yake moyoni, GANG CHOMBA uko wapi uje na misemo yako???????????????

Usigeuze sikio kusikiliza ya wenzio...
 
Mkuu EMT,
Kwa upande wa maandalizi hakuna shaka kwasababu kwa Brazil hata i''kibidi watu wale'' nyasi yatafanikiwa tu.
Kitu kilichonifurahisha ni kupata ile ladha kamili ya kuangalia na kusikiliza soka kama lilivyo na ilivyozoeleka.

Tofauti na South Afrika hapa unasikia ile mandhari ya uwanja kwa ushangiliaji au hata kuzomea ili mradi shamra shamra.
Hakuna kelele za kipuuzi kama za vuvuzela.

Vuvu zela ilikuwa kero sana si kwa wenzetu hata mimi niliichukia sana. Of course haikuandikwa sana kwasababu ya kuogopa mambo ya race, ukweli utabaki pale pale Vuvu zela ilikuwa nuisance and primitive way ya shamra shamra na ilifanya mashindano yapoteze ladha.

Kuhusu goal-line technology hiyo nimeikaribisha sana lakini FIFA wangekuwa na utaratibu wa 'review' pale penye utata.
Lile goli la Brazili lililopatikana kwa mkwaju wa adhabu ukiangalia vizuri sana utagundua kuwa beki wa Italy hakufanya rafu.

Kilichotokea ni mchezaji wa Brazil kupoteza mpira na haraka akachomeka mkuu wake katikati ya yule beki kutafuta penalty.

Waamuzi hawajagundua mbinu ya Brazil ya kujiangusha na wakati mwingine kulazimisha adhabu kwa ''exaggeration''
Pamoja na umahiri wao wa soka hili ni jambo linalotia maudhi sana. Kwamba wakiwa na mpira basi wasinyang'anywe hadi wafunge. Unakumbuka last world cup kuna refa aliwakalia kidete hadi wakaacha ujinga huo wa kujiangausha.
 
Nini wewe?
Unachuma dhambi kwa kumzihaki Gianluigi Gigi Buffon.
Buffon ni numero uno hapa Duniani.
Hana wa kufanana nae wala wa kumkaribia.
Ni kipa ambaye akifungwa basi mabeki wanakwenda kuokota mpira na kuurusha kati ili watu wauanzishe...

Tell em!
 
Mkuu EMT,
Kwa upande wa maandalizi hakuna shaka kwasababu kwa Brazil hata i''kibidi watu wale'' nyasi yatafanikiwa tu.
Kitu kilichonifurahisha ni kupata ile ladha kamili ya kuangalia na kusikiliza soka kama lilivyo na ilivyozoeleka.

Tofauti na South Afrika hapa unasikia ile mandhari ya uwanja kwa ushangiliaji au hata kuzomea ili mradi shamra shamra.
Hakuna kelele za kipuuzi kama za vuvuzela.

Vuvu zela ilikuwa kero sana si kwa wenzetu hata mimi niliichukia sana. Of course haikuandikwa sana kwasababu ya kuogopa mambo ya race, ukweli utabaki pale pale Vuvu zela ilikuwa nuisance and primitive way ya shamra shamra na ilifanya mashindano yapoteze ladha.

Kuhusu goal-line technology hiyo nimeikaribisha sana lakini FIFA wangekuwa na utaratibu wa 'review' pale penye utata.
Lile goli la Brazili lililopatikana kwa mkwaju wa adhabu ukiangalia vizuri sana utagundua kuwa beki wa Italy hakufanya rafu.

Kilichotokea ni mchezaji wa Brazil kupoteza mpira na haraka akachomeka mkuu wake katikati ya yule beki kutafuta penalty.

Waamuzi hawajagundua mbinu ya Brazil ya kujiangusha na wakati mwingine kulazimisha adhabu kwa ''exaggeration''
Pamoja na umahiri wao wa soka hili ni jambo linalotia maudhi sana. Kwamba wakiwa na mpira basi wasinyang'anywe hadi wafunge. Unakumbuka last world cup kuna refa aliwakalia kidete hadi wakaacha ujinga huo wa kujiangausha.

na la pili kuna mtu alikuwa offside upande wa Dante na mpira ulikwenda uelekeo ule ule na Dante mwenyewe alizidi mkono.frankly speaking,yule refa atakuwa Mtahiti maana na lile goli letu la pili vichekesho tupu!
 
Kabisa Mkuu, mimi nilikuwa upande wa Brazil jana ila ukweli lazima tuongee, lile goli la Dante ule mpira ulivopigwa ndani ya 18 mtu wa kwanza kabisa kuupga ambae aliluka juu alikuwa Offside kabisa. Ninaweza kubdili mtazamo wangu kama nitaangalie tena ile video lakini mpaka sasa nafahamu ni Offside ile.
 
goli la kwanza la Dante he made the same mistake....naona anazeeka vibaya. Italy should look for new number one.!

The guy is only 35 years old for God sake. Tena ni kipa. Angekuwa striker sawa.

Nilimsikia commentator akisema hivyo hivyo, lakini alishambuliwa sana twitter.

The players are tired kwa kucheza mechi nyingi mno bila break.

Umeangalia form ya Oscar mwenye miaka 21 ilivyoshuka?

Nasikia kacheza mechi zaidi ya 80 msimu huu.
 
weupe wote maneno yapo Spain timu bora duniani,1st na 2nd eleven muziki ule ule sio timu kikosi kimoja kila mechi hadi unakariri.
 
Sunday Mba ana rekodi ya kufunga kila j2,sijui labda na leo atafunga vs Spain,Spain vs Nigeria usikose saa 4 usiku TZ
 
Kuhusu goal-line technology hiyo nimeikaribisha sana lakini FIFA wangekuwa na utaratibu wa 'review' pale penye utata. Lile goli la Brazili lililopatikana kwa mkwaju wa adhabu ukiangalia vizuri sana utagundua kuwa beki wa Italy hakufanya rafu.

Hata mie sikuelewa maana pale beki alikuwa hana hana cha kufanya. Nafikiri the most controversial decisions kwenye soka siyo kama mpira umevuka mstari bali, whether mfungaji alikuwa off side. Whether the ball crossed the line, inatokea mara chache sana.

On one hand, kama soka itatawaliwa na technology kunaweza kupunguza excitement ya soka. What makes football interesting siyo tuu skills za wachezaji bali pia pia some controversial decisions made by referees. Mara nyingi baada ya mechi discussions zinajikita zaidi kwenye maamuzi yaliyofanywa na refa. Hii ni tofauti na rugby ambapo baada ya mechi kuisha, there is no further interesting discussions (sorry afrodenzi 🙂).

On the other hand, siku hizi watu wame-invest sana kwenye soka to the extent that kuna financial costs associated with the decisions made by referees. Kuna mechi moja nadhani ni Wigan walifungwa goli ambalo lilionekana na wrong decision kama ile ya Neymar jana, na kocha wao kudai kuwa that the referee's decision to award their opponent a free kick, which they scored, cost them £30 million!

Kitu kilichonifurahisha ni kupata ile ladha kamili ya kuangalia na kusikiliza soka kama lilivyo na ilivyozoeleka.

Tofauti na South Afrika hapa unasikia ile mandhari ya uwanja kwa ushangiliaji au hata kuzomea ili mradi shamra shamra. Hakuna kelele za kipuuzi kama za vuvuzela.

Vuvu zela ilikuwa kero sana si kwa wenzetu hata mimi niliichukia sana. Of course haikuandikwa sana kwasababu ya kuogopa mambo ya race, ukweli utabaki pale pale Vuvu zela ilikuwa nuisance and primitive way ya shamra shamra na ilifanya mashindano yapoteze ladha.

Yea, kwa upande wa mashabiki they have been fun, japokuwa mitaani wengi bado wana protest kwa kiingilio kuwa juu mno. Nimependa ushiriki wa Tahiti na hasa wachezaji wao wa kuokoteza mitaani kama yule mwotesha nazi. Wako baadhi wanadai kuwa they are making football to look ridiculous, but they they qualified to paly in the Confederation Cup baada ya kushinda Oceania Cup of Nations against the "might" of Australia and New Zealand.

Imagine mkwea nazi kutoka Mbagala Kizuiani, anakabana na Torres wa mambigwa wa dunia kwenye international competitive match, tena kwenye uwanja ulioko Brazil na pamoja na kufungwa bao 10, mashabiki 99.99 wanamshangilia na baada ya mechi wanapewa a standing ovation and a lap of honour kutoka kwa mabingwa hao wa dunia.

That is inspiring na inaonyesha respect ambayo inapoteka kwenye soka aka the "beautifull game". Mafanikio yoyote yanatokana na respect unayotoa kwa wapinzania wako, regardless of their capacity. Lakini huyu pundit ana-question the professionalism ya wachezaji wa Tahit ku-smile baada ya mechi baada kufungwa bao 10

[video=youtube_share;myF44FsME80]http://youtu.be/myF44FsME80[/video]
 
Last edited by a moderator:
afrodenzi umepokea kigongo hicho, ha ha ha ha

Nadhani Tahit wana haki kabisa kwasababu walishindana''si viti maalum''. Tunakumbuka kuwa miaka iliyopita Ziare iliwahi kuchapwa 9. Kwahiyo hoja ya kuwa Tahiti inakera haina maana. Hivi leo Nigeria akilambwa 6 tutasemaje? maana leo lazima alambwe tu sioni mahali pa kutokea.

Mkuu, hebu rudia ile faulu iliyoleta goli, ni wazi kabisa mchezaji wa Brazili aliingiza mguu makusudi na kujirusha.

Kwakweli mimi siyo mshabiki wa Brazil kwasababu ya kujiangusha, ku-exaggerate n.k.

Ndio maana siku zote EPL ni bora duniani kwasababu kama unakunywa chai na kitumbua na lunch ya mlenda au mgagani ukianguka no one cares soka linakwenda mbele.

Nawapenda German maana wao ni kazi tu kuanguka ni dhalili, nawapenda Netherland kwakutandaza bila kujiangusha hovyo.

Spain na Portugal mhhh aa wanajaribu kuiga latin America kwa kiasi fulani.
 
  • Thanks
Reactions: EMT

Dividing inaboa sometimes, hasa ile ya ku-exagerate kama Dani Alves.

Kitu kinachonishanga ni kuwa wanao-dive ni professional footballers.

Sijaona mchezaji wa Tahiti aki-dive au akijaribu kufanya exaggeration.

Ila kwa Netherlands, yule Arjen Robben kaacha ku-dive?

soc_g_robben_gb1_640.jpg
 
Huwa sishabikii timu za kiafrika sababu hii.watacheza mpira sana,watawatieni matumaini lakini kupeleka mpira wavuni hamna kitu,wenzao wakirudi hawakosi.hivi waafrika tuna laana na timu za taifa?hebu angalia Nigeria walivyoibana timu ngumu kama Spain kwa dk karibu 60 huku wakikosa magoli kipuuzi.sasa wamechoka,Torres kaanza kuwatundika misumari,bulshit!
 
Tempo ya kawaida ya Spain leo haipo. Naona midfield ya NG inaendana sambamba na akina Iniesta, Xavi & Silva. NG wanazidiwa kwenye 'precision' maeneo ya 18 yrd
 
Spain 3

Nigeria wancheza kama wamechoka sana sijui hawajapewa fedha! yaani ni horrible tu

Siyo ile ya akina Olisei, JJ.

Shame on you nigeria
 
Spain 3

Nigeria wancheza kama wamechoka sana sijui hawajapewa fedha! yaani ni horrible tu

Siyo ile ya akina Olisei, JJ.

Shame on you nigeria
Hawa wanaijeria hawana uzalendo kabisa, nahisi huenda hawakupewa posho......!!
 
Spain fainali hiyo,naiona

wadau nimeshanunua kopo la panadol.nilianza dozi jana baada ya kusikia Ballotelli na Pirlo wameumia.Ballo ndio leo kapanda ndege kurudi Milan.De Rossi ana kadi dah,poa lakini ntakufa na Italia yangu hata akipangwa Iaquinta poa tu,ntafanyaje sasa!
 
Back
Top Bottom