Fidel Castro hakuwahi kutabiri Papa wa Kilatini na Rais mweusi USA

Dotto C. Rangimoto

Verified Member
Nov 22, 2012
1,993
2,000
1458819116644.jpg

"The US will come talk to us when it has a black president and the world has a Latin American Pope.”

Picha ya Fidel Castro ilo andikwa maneno hayo imekuwa ikisimbaa duniani kupitia mitandao ya kijamii, hasa hasa baada Katoliki kupata Papa wa Kilatin.

Pia nimeona rafiki zangu humu facebook wakiendelea kusambaza hiyo picha, leo hii nimeona nizame na kuchimbua ukweli wa utabiri huo, naam, nimelazimika kutafuta ukweli wa hiki kinaochoitwa unabii au uchawi wa Fidel Castro wa kuweza kuona mambo yajayo kabla hayajatukia.

Awali ya yote hakuna ukweli wowote juu ya kauli hii, huu ni uzushi kama uzushi mwingine wa mtandaoni na wa kwenye magazeti na majarida ambayo naweza kusema ya UDAKU. Ambayo siku zote hujitafutia umaarufu kwa kuwalisha maneno wasanii na wanasiasa maarufu.

Nukuu hiyo kumhusu Fidel Castro iliandikwa kwa mara ya kwanza na mwaandishi wa Kiagertina Bwa Pedro Jorge Silans katika jarida la "The Journal Of Carlos Paz" tarehe 10/03/2015.

Uzushi huu wa Bw Solans juu ya Fidel Castro ulimaanisha dhihaka ama istizai lakini katu hauwezi kuuita unabii sababu wakati unaandikwa kwa mara ya kwanza tayari Obama yuko ndani ya White House na Papa Fransis yuko Vatican akihudumu upapa. Nasema ni dhihaka na si unabii kutokana na sababu zifuatazo.

Mosi: Kwanini haya yajulikane baada ya miaka 40?

Tangu mwaka 1973 unaosemekana hayo maneno katamka Fidel Castro hayakujulikana au kuandikwa popote hadi miaka 40 baadae tena ikiwa tayari Marekani ikiwa na rais mweusi na Katoliki kuwa na Papa wa kilatini? Kwanini mitandao au hilo jarida lilo andika kwa mara ya kwanza lilisubiri Whit house kuwa na rais mweusi na katoliki kuwa na papa wa kilatini?

Pili kwanini mwaka tu?

Solans anasema Mwaka ambao Fidel Castro amesema maneno hayo ni 1973, lakini hataji tarehe na mwezi. Maneno kama haya na tena utabiri mzito na hasahasa ukizingatia kupamba moto kwa vita baridi, iweje tarehe na mwezi wake usijulikane? Hiki ni kiashiria cha urongo na uzushi.

Tatu, Chanzo Cha Habari
Tarehe 10/03/2015 jarida la El Diario de Carlos Paz( The Journal Of Carlos Paz) liliandika makala yenye kichwa kisemacho " Cuba through changing times: The End Of the blockade?"

Mwandishi wa makala hiyo anaitwa Pedro Jorge Solans, pamoja na mambo mengine alo yaandika juu ya USA na CUBA, lakini pia alizungumzia huo utabiri wa Fidel Castro.

Solans amesema mwaka 1973 Kamanda Fidel Castro akiwa ndio kwanza akiwasili Havana akitokea Vietnam alizungumza na wanahabari wa kimataifa. Kipindi hicho vita baridi ilikuwa ndio imepamba moto, mwanahabari kiingereza aitwaye Bryan Davis akamuuliza Castro.

"Unafikiri ni lini hasa mahusiano kati ya Cuba na USA yatarejea tena?"

Fidel Castro akamkazia macho Davis kisha akamjibu.

"Marekani itakuja kukiri kwetu pindi wakiwa na rais Mweusi na Dunia ikwa na Papa wa kilatini" Hiyo nukuu iko kwa kiingereza ila nimeitafasiri hivyo.

Kwa mujibu wa Clarin gazeti maarufu la Argentina, wakati Solan akigundua kauli hiyo ya Caatro alikuwa Havana akifuatilia habari za mahusiano kati ya USA na Cuba.

Solan anasema alipokuwa Cuba alifanya mazungumzo na Dereva wa Tax Eduardo de la Torre aliyemhudumia , na katika mazungumzo hayo ndipo Solan akasikia kwa mara ya kwanza nukuu hiyo ya Castro kutoka kwa Eduardo. Eduard de laTorre ambaye kwa sasa ni Dereva Tax mwaka 1973 alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

Eduardo ni shabiki mkubwa wa Fidel Castro, yeye alimuona Castro kama nabii na alifananisha na Yesu Kristu pale alipomwambia Bw Solan

"Fidel Castro alifufuka mara nyingi kuliko hata Yesu Kristu, hivi unafikiri mara ngapi vyombo habari vya kimataifa viliripoti kuwa kamanda kafa lakini inatokea mzima?" Eduardo alisema kwa mtindo wa kutupia swali kwa Solans. Kwa ushabiki huu na utungaji huu wa hekaya Bwa Eduardo hafai kuwa chanzo cha habari cha kuaminiwa sana hususani habari hiyo ikimuhusu Castro.

Sasa ni ajabu sana maneno ya Dereva wa Tax katika mitaa kubebwa na mwandishi huyu mazimamazima ikiwa jiji la Havana linasifika kwa nukuu za kuwalisha maneno watu maarufu. Bw Solan hakutakiwa kumtegemea Eduardo pekee kama chanzo sahihi cha habari yake ikiwa mwandishi anayeaminiwa kumuuliza swali Castro yuko katika jijini London na sasa hiv mlevi mbwa, namaanisha angejiridhisha japo kwa kumuuliza Bryn Davis pia.

Nne: Kwanini vyombo vya habari vya Cuba na kimataifa havijaripoti?

Huenda nukuu hiyo ya Fidel Castro ni sahihi, lakini naingiwa na shaka kwasababu hakuna kumbukumbu rasmi ya kiserikali ikionesha kuwa Fidel Castro aliwahi kuzungumza na wanahabari kisha akatamka maneno hayo, lakini pia hakuna chombo chochote kilicho ripoti mkutano huo na maneno hayo hadi pale yalipokuja kuandikwa kwa mara ya Kwanza na Bw Solan.

Tumeona Whitehouse kuna rais mweusi na dunia ina papa wa kilatini, na hivi majuzi tu tumeona Obama akizulu Cuba, hivi kwanini vyombo vya kimataifa havijarejea maneno haya ya Castro wakati vikiripoti ziara ya Obama Cuba? Hiki ni kiashiria tosha kuwa Bw Solan aliamua tu kudanganya ulimwengu.

Hata hivyo, Bw Solans hakujishughulisha kuthibitisha maneno ya Eduardo kwa kutumia kumbukumbu za kihistoria au huenda alifanya hivyo lakini akawa amekosa kumbukumbu hizo, na kubwa zaidi hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha madai yake.

Rafael Rojas, author of A Brief of tha Cuban Revolution aliliambia gazeti la Mexico El Universal kuwa "Siamini hata kidogo kuwa Fidel Castro aliwahi kuzungumza maneno haya ya kinabii"

Rojas anasema iwe Castro au mtu yeyote lakini maneno hayo yamezushwa kama masihara mengine tu, kuonesha jambo fulani ni muhari kutokea, mathalani Cuba kuna msemo maarufu "it will happen when a frog grows hair"

Tano: Fidel Castro ni mbovu katika utabiri.

Wengine wanasema maneno hayo ya uzushi yanauhusishwa na mahojiano kati ya Fidel Castro na Barbara Walter yalofanyika mwaka 1977. Katika mahojiano hayo Feidel Castro alimwambia Barbara huenda USA na Cuba zitarudisha mahusiano kati ya mwaka 1980 na 1984 kipindi ambacho Jimmy Carter akihudumu awamu yake pili Whitehouse.

Mahojiano ambayo yalibatilisha unabii wowote wa fidel Castro alio wahi kuutoa sababu mwaka 1980 Ronald Reagan alimuondoa Carter Whitehouse kwa ushindi wa kishindo. Kwa hivyo ingekuwa ni jambo la kushangaza kwa Castro kuwa na utabiri huu ikiwa utabiri kama huo alio uhusisha na Jimmy Carter ulifeli.

Bofya link hiyo kuona video ya mahojiano kati ya Castro na Barbara ya mwaka 1977.

Video: Fidel Castro's Prediction for 'Normal Relations' With US

Mwisho.

Ni aibu sana kwa mtu yeyote, kuokota kitu katika mtandao na kisha ukakisambaza bila kukifanyia utafiti, inakuwa aibu kubwa sana jambo hili likifanywa na masomi, lakini fedheha likifanywa na anayetegemewa na anayeigizwa.

Njano5
0622845394
 
moghasa

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,017
2,000
View attachment 332281

umemaliza mkuu
 
dist111

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
3,278
2,000
Sina hakika kama alitamka,

ila hivi ni vitu vya mzaha, hata kama alitamka haviwez kuwa couted kwa kipindi hiko! mpaka pale mambo yanapoelekea kutimia ndo watu watakumbuka semi hizo, so kutafuta ushahidi wake ni ngumu manake hata yeye castrol anaweza akawa amesahau!

ila inaleta ujumbe ni namna gani mzungu alivombishi! Kwamba only mpaka discrimination itakapoisha ndo mambo yataenda sawia duniani
 
dre4691

JF-Expert Member
Feb 22, 2016
499
500
Kwanza upo nyuma kwenye ufuatiliaji pili vyombo vyote vya hbr vikubwa vinamilikiwa na kundi LA maalum wenye nia yao wenyewe tatu Albert pike alitabiri vita ya 1na 2 kabla haijatokeA hivyo ni kawaida kbs kwataarifa yako watu wana mipango hadi ya miaka Mia mbele na itatimia km ilivyopangwa..
 
Dotto C. Rangimoto

Verified Member
Nov 22, 2012
1,993
2,000
Kwanza upo nyuma kwenye ufuatiliaji pili vyombo vyote vya hbr vikubwa vinamilikiwa na kundi LA maalum wenye nia yao wenyewe tatu Albert pike alitabiri vita ya 1na 2 kabla haijatokeA hivyo ni kawaida kbs kwataarifa yako watu wana mipango hadi ya miaka Mia mbele na itatimia km ilivyopangwa..
mpangaji nani??
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,642
2,000
Yale yale kama ya Donald Trump kuwasema Waafrika na Wakenya!

Habari ambayo haipo hata huko Marekani kwenyewe lakini imeenea kwenye mitandao ya Waafrika na akili zao!
 
MNFUMAKOLE

JF-Expert Member
Nov 14, 2014
565
1,000
Hivi mleta mada unakumbuka kuwa. kuzaliwa kwa Yesu kulitabiliwa kabla? lakini hakuna anaekumbuka tar wala mwaka! lakini tunaamini kuwa ndie Masihi! pili lini Wamarekani walisifia vitu vya wengine? wao wanaamini vizuri vyote vinatoka kwao! usishangae wakwambia Magufuli babu yake alikuwa Mmarekani! siku zote unabii ukumbukwa siku ukitimia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom