sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,695
- 9,908
Mkuu inaonekana unachanganya rapper mkali na mwanamalenga mzuri. Fid ni rapper anaetegemea zaidi ushairi wa kimapoke pia anatohoa sana hafanyi creation from the scratch. Ila ukija kwenye flow, content, one two one two, ideas bado amuwezi Ngwea. Ngwea anaweza fanya hardcore na commercial ukafurahi. Ila Fid ni underground rap mwanzo mwisho.Kupiga freestyle kali haikufanyi kuwa mc mkali mbele ya ma'mc ambao hawapingi freestyle, hip hop ni zaidi ya freestyle!!
Ngwair alikuwa mkali Tena Sana ila naona anakuwa overhyped Sana! Alikuwa na flow kali, alikuwa na uwezo wa Kuimba juu ya beat na kuitembelea kama hataki kama Ngoma she got gwan, pia alikuwa ana content Kali zinazoigusa jamii kama a.k.a Mimi au kama ni binti sikiliza ft Jaydee! So ana maunyama yake yaani sio kinyonge! Pamoja na hayo still kulikuwa MC's kibao ambao kiuwezo walikuwa juu ya Ngwair katika namna mbali mbali!!
Mfano huwezi kumuweka Ngwair na Fid kwenye stage Moja halafu ukasema Ngwair mkali kuliko Fid! Tuzungumzie uandishi, matumizi ya lugha, tamadhali za semi, ufundi katika relate na jamii, content zilizoshiba! Watu wanasema Fid anacopy kwenye vitabu, yes hiyo pia ni sehemu pia ya Sanaa na ndio maana MC's wengine hawawezi hiyo! Fid ni knowledgeable! Maarifa mengi! So kete yangu inaenda kwa Fareed Kubanda!
Yeah hawezi ndio maana anayo moja tu. MC bila storytelling hujawa MC mkali.Fid hawezi storytelling? Report za mtaani ft Zahir Ally Zorro ilikuwa nini? Kwa upande wangu Ile Ngoma ni miongoni mwa Ngoma kali za muda wote as far as storytelling is concerned!
Uzito wa mashairi unamaanisha misamiati, misemo na quotes za kwenye vitabu?
Unaweza nitajia wimbo wa Fid Q wenye mashairi mazito kushinda walau jina langu ya Prof Jay?
Tatizo wabongo wengi wanajifanya wanajua Sana lakini hakuna wanachojua zaidi ya porojo za vijiweni.Wasambaa wanasema “hard work beat talent”
Ngwea anakipaji cha kuweza kutunga wimbo kwa freestyle lakini mashairi yake yatakua mepesi ila yatabebwa na swaga na beat kali anazotumia Ngwea
Fid Q ni aina ya waandishi wanatumia effort kubwa kutunga mashairi na mpangilio
Uandishi huu unahitaji knowledge, ndio maana mnasema ana quote vitabu
Fid Q ana mistari ukiusikia wewe mwenyewe unahisi hajatunga yeye ka copy mahali
Lakink Ngwea anaimba vitu vyepesi kueleweka
Kwa mbele Ngwea ni kama Lil Wyne
Na Fid Q ni kama NAS
Tatizo wabongo wengi wanajifanya wanajua Sana lakini hakuna wanachojua zaidi ya porojo za vijiweni.
Bahati nzuri Fid na Ngwair wote nimewasikiliza since day one wanaanza kutoa Ngoma na kutambulika kwenye game lakini niseme tu hata kumlinganisha Ngwair na Fid NI dhambi kubwa Sana tena Sana.
Binafsi mi ni shabiki mkubwa wa Ngwair Hadi kuna member mmoja hapa JF alizani mi Nina undugu na Ngwair maana hua napenda sana kuchangia Sana nyuzi zinazomhusu Hadi kuandika pia lyrics maana sizani kama kuna Ngoma ya Ngwair sikukalili... Hadi huyo jamaa kwenye simu yake nazani kanisave Ngwair, maana ikifika mahali tukawa marafiki.
Lakini tukirudi kwenye kulinganisha sijajua labda alimaanisha Ngoma zilizobamba club labda kwenye hiyo angle Ila Kama ni swala la Hip-hop basi hapa bongo hakuna msanii anayeweza kumzidi Fid Q labda kidogo kitambo kile Langa Alikua na uandishi mkali tatizo hakua na Ngoma nyingi (consistency) kama Farid.
Kusema anakopi kwenye vitabu huu ni utani Fid anamisemo mingi Sana hata akiwa anazungumza unaweza elewa ni mtu wa namna gani?
"Akikupiga ngumi ya jicho na we mpige ngumi ya sikio akiuuliza unaonaje na we muulize unajisikiaje!?" Sijui huu mstari upo kwenye kitabu gani??
Umefunga mjadalaTatizo wabongo wengi wanajifanya wanajua Sana lakini hakuna wanachojua zaidi ya porojo za vijiweni.
Bahati nzuri Fid na Ngwair wote nimewasikiliza since day one wanaanza kutoa Ngoma na kutambulika kwenye game lakini niseme tu hata kumlinganisha Ngwair na Fid NI dhambi kubwa Sana tena Sana.
Binafsi mi ni shabiki mkubwa wa Ngwair Hadi kuna member mmoja hapa JF alizani mi Nina undugu na Ngwair maana hua napenda sana kuchangia Sana nyuzi zinazomhusu Hadi kuandika pia lyrics maana sizani kama kuna Ngoma ya Ngwair sikukalili... Hadi huyo jamaa kwenye simu yake nazani kanisave Ngwair, maana ikifika mahali tukawa marafiki.
Lakini tukirudi kwenye kulinganisha sijajua labda alimaanisha Ngoma zilizobamba club labda kwenye hiyo angle Ila Kama ni swala la Hip-hop basi hapa bongo hakuna msanii anayeweza kumzidi Fid Q labda kidogo kitambo kile Langa Alikua na uandishi mkali tatizo hakua na Ngoma nyingi (consistency) kama Farid.
Kusema anakopi kwenye vitabu huu ni utani Fid anamisemo mingi Sana hata akiwa anazungumza unaweza elewa ni mtu wa namna gani?
"Akikupiga ngumi ya jicho na we mpige ngumi ya sikio akiuuliza unaonaje na we muulize unajisikiaje!?" Sijui huu mstari upo kwenye kitabu gani??
Professor jay ndo alinifanya nikaipenda hip-hop "chemsha bongo"Ila prof j wengi wataanza kumzungumzia pindi akiwa kasha kuwa marehemu kwasasa design kama wanampotezea hivi. Ila ukizungumzia msaani mwenye uwandishi wa ajabu ambaye hatoki nje ya mada katika kile anachokiimba hakika ni prof j.
Huyu jamaa hakika kujiita prof katika industry ya muziki wa bongo hakukosea, kweli tuwaongelee wakina farid na gwea lakini hawa baba yao ni prof j . Hebu kaa sikiliza hivi vinu vya huyu mwamba
- usinetenge ft q chifu
- siyo & ndyo mzee
- joseph
- nang'tuka
Afu uje unipinge nikisemacho
Nakubal fid q ndo mfalme wa hiphop
Wadau me Naleta hoja kwenu, kuna watu naona wanaleta list tofauti za wana hiphop kila mtu na mtazamo wake anavyoona yeye, lakini kinachonichanganya kuna baadhi ya watu wanasema kuwa Ngwair alikuwa ni zaidi ya Fid Q kitu ambacho kwangu sijawahi kukubaliana nacho. Maana kwa mtazamo wangu sidhani kama kuna rapa kweli anamuweza Farid kwa uandishi.
Jamaa anayo IQ kubwa sana, mimi nataka mnifundishe hiphop, kama nakosea nataka mnielekeze Ngwair alikuwa anamzidi Fid katika category gani?
Hatutaki story telling huwa nasikiliza ngoma za Jay z Hana kitu inaitwa story telling ...Ila ni namna mtu anaghani na mashairi fid q is the bestNamkubali Farid ila Ngwea ni mkali kuliko Farid. Unapozungumzia IQ Ngwea yupo mbele ya Fid Q. Ukimsikiliza Ngwea ngoma zake anaandika flows yani bar after bar zinatililika. Fid hawezi kufanya hata storytelling.
Afande sele aliwahi fanya wapi freestyleKutokujua freestyle Wala sio udhaifu
Fareed,Langa, MwanaFa hata Prof Jay sio wazuri kwenye freestyle.
Wasanii wachache wanaweza kufreestyle na kubandika bars za kueleweka,Ngwair na Afande sele wamo kwenye Hilo kundi.
Ngwea zaidNgwair and Fid Q wote wazuri
Kinachokuchanganya ww ni kuchanganyikiwa na mitazamo ya watu wakati ww una mitazamo yako sahihi kabisa alafu kwa kutojiamini unabaki kuuliza ilikuaje.
Wadau me Naleta hoja kwenu, kuna watu naona wanaleta list tofauti za wana hiphop kila mtu na mtazamo wake anavyoona yeye, lakini kinachonichanganya kuna baadhi ya watu wanasema kuwa Ngwair alikuwa ni zaidi ya Fid Q kitu ambacho kwangu sijawahi kukubaliana nacho.