Huwa napenda kusikiliza watu wazima from time to time ili kupata picha time yao walikuwa wanafikiria nini. Juzi ilikuwa zamu ya Babu KRS One. Kwenye album yake 'I Got Next' ana track inaitwa 'A friend', dope track si uongo. Nimeiskiliza kama mara 3/4/5 hivi, nikakumbuka our very own..Fid Q ana track inaitwa 'sihitaji marafiki', kwa bahati mbaya sijawahi kuiskiliza mpaka sasa, ila nilishawahi kuona episode moja ya Mkasi Jamaa akiielezea. Knowing Fid Q, nikaingia Tzhiphop na kucheki lyrics, na kulinganisha na track ya Teacha. Nimegundua Jamaa ka-copy concept, baadhi ya mistari na maneno pia, japo kayafanyia sanaa kidogo.
'True friends are quick to sit
in the beginning of all trouble, and when your bankroll doubles/ - Teacha
Vs
Kupata washkaji ukiwa na pesa ni rahisi, Kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi/ -
Fid
'Cause don't nobody care about us, all they do is doubt us/ Until we blow the spot then they all wanna crowd us, and wanna shout us/
but you my man from way back' - Teacha vs 'sihitaji urafiki na usupastaa / ukihit ndo unang'aa..
upishwe useat kwenye bar,upewe beat na Jr../ kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground' - Fid
'/I'm not a yes man and none of my friends are yes men or women/' - Teacha Vs 'sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man/'- Fid
'Whether at the bar with superstars'- Teacha Vs
'sihitaji urafiki na usupastaa / ukihit ndo unang'aa..
upishwe useat kwenye bar,' - Fid
Kuna lines kadhaa pia za Rappers wengine humo ndani, mojawapo ni ya Biggie Smallz
'Girls used to diss me, now they write letters coz they miss me' Vs 'Siku hizi mademu wanaoni-miss ni walioni-diss'
Fid Q, Fraud Q or Fake Q??
Teacha Huyu hapa, msikilize mwenyewe halafu linganisha na ngoma ya Fid hapa chini.
bado hauja nishawishi katika hili,what i know you just a hater not annalist..!!!
"what doesnt kill me makes me strnger"kanye west pia hii tuiite copycat kutoka katika line za 2pac sindio mzee??
"anamiaka chini ya kumi na nane"Sugu na "baby don't cry(keep ya head up"II) 2pac nayo ni copycat??
They shot i mad em look, .....hii ikitoka kwenye Ngoma moja ya NAS. Utaikuta kwenye Danger ya Fid q.
Bt nikujuze hivi. Sanaa ni fasihi, na fasihi hutokana na kuona, kusikia, kutunga, n.k ili kujenga maudhui ya nyimbo na kazi ya fasihi. Pia jua, hakuna ambacho ni kipya vyote , so mtu akisoma vitabu, kusikia, na kuweza kufanya mseto wa hoja hizo kwa misemo, vina kwa Lugha yake nayo ni sanaaaa.
Big up fid, umeanz kitambo ku make hits na stil unatengeneza hits.
Jamaa anachosema ni kweli.. Kiukwel katika hiphop sana sana rap kwa fid mi naeka kando.. Sawa jamaana ana flow ana mpangilio ila ile art of HIPHOP yenyewe ni ndogo sana.. Mtu haezi copy mistari mingi kwa mwingine tukamuita hiphop artist kucopy kupo ila si design ya jamaa.. Mcheki mtu kama MBWAA MZEE (chindo) ana art yenyewe mtu ujiskiza lyrics zake unakubali kweli amekaa na akaandaa uhalisia wa jambo.
Unless sielewi lugha au concept ya a friend in Need alikuja nayo KRS One ebu niambie kuna usawa upi katika hizi verse mbili....
True friends are quick to sit
in the beginning of all trouble, and when your bankroll doubles/ - Teacha
Vs
Kupata washkaji ukiwa na pesa ni rahisi, Kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi/ -
Fid
By the way ingawa haijafanyika hapa nadhani nyie wadau hamjui kitu kinaitwa Sampling (done all over the world) na hapa cha maana ni mtu kutoa kazi inayoendana na concept ikapendeza ikaeleweka na ika-flow, ukizingatia hawa Artist wote ma Role Models wao ni hao hao hardcore rappers wa enzi hizo..,