Fichua mashimo

Fichua mashimo

Joined
Mar 27, 2024
Posts
42
Reaction score
179
Napenda kufichua shimo ninalo lifahamu kwa takribani miezi miwili sasa, nikiwa na lengo la kuwapa taarifa wahusika wa kurekebisha miundombinu...pili kwa watumiaji wa vyombo vya moto.

Kuna shimo lipo nyuma ya chuo cha ustawi wa jamii Sinza...ukiwa unatokea Makumbusho unaelekea Mwenge Kuna barabara inachepuka kushoto nyuma ya kaijage road na mbele Kuna Shekilango road Sasa yenyewe inachepuka kushoto ili ikakutane na ya Shekilango road kupitia nyuma ya chuo cha ustawi....

wakuu ukiwa umejisahau kidogo hasa nyakati za usiku utaweza ukapiga chini na boda ukavunja hadi meno..naomba wahusika wakalishuhulikie hilo tuta ni hatari Sana mara mana linazidi kutanuka ...ewe mwana jf nakuomba uchukue tahadhari...

Kama unalijua shimo lolote embu lifichue wahusika wanaweza kuwa humu wakatatua kwa haraka

Ahsanteni Sana!
 
Back
Top Bottom