Fernando Torez katika vivuli vya kiafrika

Rockcity native

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
2,176
Reaction score
1,475
Katika watu ambao career yao ya soka haitawasahau waafrika ni huyu torez. Kila kukicha ndani ya stanford bridge lazima apambane na ushindani wa namba na mwafrika. Ikumbukwe jamaa alisajiliwa kwa pesa ndefu sana kuja kuchukua nafasi ya drogba lakini kilichomtokea anakijua mwenyewe. Drogba akaondoka torez akawa free hajakaa sawa akaletewa victor moses japo hakutoa challenge kubwa kwa torez, january akaletwa demba ba, licha ya kubebwa sana na kocha mhispania mwenzake benitez kwa kupewa nafasi kubwa lakini bado Torez akili yake ilikua ishakua na figisu figisu juu ya waafrika. Na sasa Eto'o japo ni veterani lakini bado anazidi kugongelea msumari wa moto katika donda na jinamizi la Torez juu ya fowad za Kiafrika.. Kwa wazee wenzangu wa uswazi wanasema jamaa anapigwa sana misumari sa sijui ni kweli au?
 
Ni kwel kaka lkn moses co mshambuliaj wa kat au nakosea wajama
 
Back
Top Bottom