Feki 9932 ni kufeli kwa taasisi zetu za ajira?

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
300
423
Baada ya Necta kutoa idadi ya waliothibitika kufoji vyeti ambao ni 9932 kwa Tanzania nzima imeonyesha wanastahili pongezi kwa kuwabaini.

Ingawaje imechukua muda mrefu sana kuwabaini maana wengine ndio wakuu Wa vitengo kwenye Taasisi zao na wengine ndio wanaenda kustaafu Mwezi huu .

Mfano kuna mmoja ambaye anastaafu tarehe 17 /5/2017 nae ameshajua angetakiwa kulipwa kiasi cha milioni mia thelasini na NNE na laki saba ,ila kwa kuwa alifoji cheti basi imetokea hayo.

Jinai ni jinai makosa ya uvunjifu Wa sheria hayana expire date tunajua watu wengi wataadhirika na hili sakata la vyeti feki sio tu hao 9932 ila hamna jinsi pia ambayo itatoa funzo kwa wahalifu Wa namba hii.

Mh.Magufuli amefanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika katika Nchi yetu na anastahili pongezi za dhati bila kumungu'nya maneno. Tunatumia gharama Kubwa kwenye Elimu ila tunakua wazembe kusimamia mambo yetu yaende kama inavyotakiwa .

Wimbi hili la waathirika Wa vyeti feki kwa kiasi Fulani linatuvua ngua kama Taifa na kutuacha watupu .Ni aibu kwa kiasi kikubwa wafanyakazi feki 9932 sio idadi ndogo hii INA madhara makubwa kwa Taifa yumkini ndio maana kunakuwa na ubadhirifu mkubwa Wa fedha za uma na matumizi mabaya ya madaraka katika taasisi zetu. Hii inaweza kuwa inachangiwa pakubwa na kuwepo kwa watumishi wasiostahili kama hawa waliobainika kwa haya makosa ya kuvunja sheria kwa kufoji vyeti.

Ikumbukwe kwamba hatuwezi kuendelea kama taifa kwa kuwa na Rais imara peke yake .Atafanya atakaloweza kwa muda kama haya anayoyafanya sasa Mh. Ila baada ya muda yanaweza yakarudi tena upya kwa kasi isiyomithilika.

Masuala haya tumekua tukiyazungumzia kila uchao hapa jukwaani kwamba badala ya haya mambo yanayoendelea ya kuwa na Rais imara anayefanya kila kitu tunahitaji taasisi imara .

Taasisi ya kuajiri ingekua imara haya yote yasingetikea aibu hii kwa taifa isingetufika .Idadi ya 9932 ni Kubwa mno INA maana basi vitu vingi bado vina shida kwani wasimamizi Wa mambo ndio hao waliokua na vyeti feki.

Tuangalie upya hizi taasisi zetu tuhakikishe zinakua imara ili kuepisha pia usumbufu Wa wananchi wetu .Kwenye hili sakata kuna watu 9932 ukijumlisha na wategemezi wao wanane wanne utajikuta unakua na watu wengi wanaoadhirika na maamuzi yetu yanayotokana na kutokuwa na taasisi imara za kudahili na kuajiri watu wanaostahili .

Maendeleo ya taifa letu yanahitaji kuwatumia watu wanaohusika kwenye sehemu husika na sio vinginevyo .Kama tutashindwa kufanya hivyo maana yaje maendeleo yatachukua muda mrefu kitufikia.

Nawasilisha......
 
Mtaani ni kilio na Kusaga meno wengine wamechanganyikiwa.
Hoja yako ni ya muhimu sana maana haya mazuri yanayofanyika bila taasisi imara yatakosa muendelezo
 
Ni kufeli Mfumo wa utawala wa CCM. Wafanyakazi wengi waliofukuzwa waliajiriwa wakati CCM ikiwa madarakani na wamefukuzwa wakati CCM ikiwa madarakani. Na bado CCM hiyo hiyo imeacha viongozi wengine kuendelea kutumia vyeti hivyo feki
Hapa bila kupata katiba mpya hakuna kitakachoendelea. CCM inatumia kila mbinu ku brainwashed watanzania wakati CCM ni ile ile na watu ni wale wale.
 
Taasisi za ajira zilijaa rushwa, kujuana yaani bosi akiwa na mchepuko mtaani usio na elimu anatafutiwa cheti na kupewa ajira, bosi akiwa na mtoto kilaza ananunua cheti na kupewa kazi ndio maana haya majanga yamezalishwa, na ndio maana utendaji kwenye sekta nyingi ulikuwa wa hovyo maana kila mtu alikuwa kambale hakuna wa kumgusa atakusemea nawe utafukuzwa ukileta kiherehere, JPM kwa kili amerudisha heshima kwa kiwango kikubwa sana.
 
kutokuchukua hatua kwa awamu iliyo pita ilikuwa tatizo kuu, kumbuka sakata la kuajili watoto wao uhamiaji na ikabainika ila mamlaka zikakaa kimya

walio saidia kutoa ajira za kufoji, upendeleo pale inapo bainika hatua kali zingechukuliwa ingepunguza hili.

hatuja chelewa bado, tuanze sasa pale itakapo bainika mamlaka kutoa ajira kwa upendeleo, rushwa ama naona yoyote kumbeba mtu hatua zichukuliwe.
 
Back
Top Bottom