Shukurani
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 251
- 11
Tunasubiri kuona utekelezaji wa hiliJK: Fedha zote zilizoibwa BoT zitarejeshwa
2008-02-01 08:50:57
Na Joseph Mwendapole
Rais Jakaya Kikwete, amewahakikishia Watanzania kuwa, fedha zote zilizoibwa (BoT) kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), zitarejeshwa serikalini na amewaomba wananchi kuwa na subira.
Aliyasema hayo katika hotuba yake ya kila mwezi kabla ya kwenda Addis Ababa kuhudhuria kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika.
``Napenda kuwahakikishia kuwa, Serikali inayo dhamira ya dhati ya kulifuatilia suala hili mpaka mwisho wake ujulikane. Mwisho ambao utakuwa na maslahi kwa taifa letu,`` alisema.
Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, wameanza kuchukua hatua.
Aidha, alisema amewaagiza watoe taarifa kwa wananchi mara kwa mara kadri inavyowezekana pamoja na haja ya kuwa waangalifu kutokutoa mengi yahusuyo uchunguzi wanaoufanya ili ushahidi usiharibike.
Alisema anaamini kuwa, kazi hiyo itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita waliyopewa na aliwataka wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hilo waisaidie kamati hiyo.
Rais Kikwete aliwapongeza wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa kazi nzuri waliyoifanya na kutoa taarifa ya kina kuhusu matatizo yahusuyo matumizi ya fedha za Akaunti hiyo.
Kuhusu suala la mafuta, Rais Kikwete alisema bado bei ya nishati hiyo iko juu sana na kuathiri uchumi wa nchi zote duniani tajiri na maskini ingawa nchi maskini zinaathirika zaidi.
``Hili si jambo geni kwetu Napenda kurudia kauli zangu za siku za nyuma kwamba, hatuna uwezo mkubwa wa kujikinga na athari za bei za mafuta tunapaswa kuendelea kuwa waangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta na tuepuke matumizi yasiyo ya lazima,`` alisema.
Alisema wakati huo huo serikali itaendelea na juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha) na kwamba juhudi hizo zikifanikiwa zitasaidia kupunguza mzigo wa mafuta yanayoagizwa kutoka nje.
Alisema ana furahi kuona juhudi hizo zina mwelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo Tanzania itaanza kunufaika na matunda yake.
Akizungumzia ujio wa Rais George Busha wa Marekani, Rais Kikwete aliwaomba watanzania wampokee mgeni huyo kwa mujibu wa mazoea na desturi za ukarimu wa Kitanzania.
``Huu ni ugeni mkubwa na wa heshima kubwa kwa nchi yetu. Rais George Bush ameipa heshima kubwa nchi yetu kwa kuamua kutumia sehemu kubwa ya ziara yake ya Bara la Afrika hapa kwetu. Ameonyesha upendo mkubwa kwetu nasi tumuonyeshe hivyo hivyo,`` alisema.
Aliomba pia Watanzania wajitokeze kwa wingi siku hiyo kumpokea mgeni huyo mashuhuri.
SOURCE: Nipashe