John John Msakuzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 279
- 99
==
Katika sekta ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Sita imetoa miongozo ya kuyawezesha makundi mbalimbali ya jamii kuimarisha uwezo wao wa kushiriki shughuli za maendeleo na kuleta usawa wa kiuchumi. Katika kipindi hiki, kumekuwa na ongezeko la vikundi vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri za Mkoa wa Mara kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kutoka vikundi 187 mwezi Novemba 2020 hadi vikundi 324 Aprili 2025. Fedha zinazotolewa kama mikopo kwa vikundi hivyo zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.63 Novemba 2020 hadi shilingi bilioni 5.88 mwaka 2025.
Idadi ya vikundi vya wanawake imeongezeka kutoka vikundi 92 Novemba 2020 hadi vikundi 99 Aprili 2025, vikundi vya vijana kutoka 53 hadi 139, na vikundi vya watu wenye ulemavu kutoka 42 hadi 86. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na vikundi hivi ni pamoja na kuongezeka kwa ajira, kuimarika kwa uchumi wa vikundi na mtu mmoja mmoja, pamoja na kupungua kwa utegemezi wa makundi haya katika jamii. Kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mkoa wa Mara una jumla ya wanufaika 50,934 hadi Juni 2025, ambapo wananchi hao wameweza kuboresha maisha yao kwa kujifunza na kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Aidha, Mkoa kwa kushirikiana na Tume ya Madini na Mgodi wa Barrick North Mara umewawezesha upatikanaji wa leseni 104 kwa vikundi 48 vyenye jumla ya vijana 1,836 kutoka vijiji 13 katika eneo la Nyamongo, Wilaya ya Tarime. Uwezeshaji wa makundi hayo ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT) yenye lengo la kutoa fursa kwa vijana kushiriki katika mnyororo wa thamani wa madini. Vijana hao wanapatiwa elimu kuhusu uchimbaji wa madini chini ya uangalizi wa Mgodi wa Barrick North Mara, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Ofisi ya Madini Mkoa.
Hata hivyo fedha zote zilizotamkwa katika utekelezaji wa miradi ya uwezeshaji ni shilingi bilioni 5.88, huku jumla ya wanufaika wote wakiwa watu 52,770.

| Miradi | 2020 | 2025 | Ongezeko |
|---|---|---|---|
| Idadi ya vikundi vyote | 187 | 324 | 137 |
| Vikundi vya wanawake | 92 | 99 | 7 |
| Vikundi vya vijana | 53 | 139 | 86 |
| Vikundi vya wenye ulemavu | 42 | 86 | 44 |
| Thamani ya mikopo (TSh Bil.) | 1.63 | 5.88 | 4.25 |
| Wanufaika TASAF | - | 50,934 | - |
| Wanufaika leseni za madini | - | 1,836 | - |
| Jumla ya wanufaika wote | - | 52,770 | - |
| Jumla ya fedha zote (TSh Bil.) | - | 5.88 | - |