hapo umeongea mazee,
hawa jamaa wakishakaa kwenye 'system' wanasahau walikotoka. Wanasahau kwamba na wao walipitia elimu ya juu. tena enzi zao walikua wanagomea msosi.
Kama inawezekana kuwapa wafanyabiashara mikopo nchi nzima kwa nini wasiweze kuwapa hao watoto wa maskini. inashangaza kuona Serikali ya Tanzania haioni umuhimu wa kuwekeza katika elimu. Hivi do they know kwamba the next Tanzania will lie on the hands of the current higher education students/ au wanataka waharibu mfumo mzima wa elimu ya Tanzania, ili watoto wao na ndugu zao ambao wamesoma 'majuu' wathaminike hata kama wamesoma vyuo batili.
Inasikitisha kuona ni jinsi gani serikali yetu isivyojali kuboresha sekta ya Elimu. Ni vyema watoe mikopo ya ada 100% alaf hizo fedha za matumizi wazigawe kwa 'grades'.
Unaposhindwa kutoa fedha za Ada unategemea chuo kitajiendeshaje? Chuo kinategemea serikali, serikali inatupia mzigo kwa wananchi. Mboa mizigo yao inawatosha tayari. Imagine mtu wa kipato cha chini "Tsh. 80,000" anayeishi hapa dar es Salaam. Igawe hiyo hela yake kwa ajili ya Nauli, Chakula, Malazi, Matibabu alafu ubakishe 20% ya ada ya mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu.
Mimi ninaamii kwa MIPANGO thabiti, serikali kutoa 100% kwa wanafunzi wote inawezekana.
kama wanashindwa sasa hivi basi watambue hawatokaa waweze kulipia hata 20% ifikapo 2015. kwa mtu wa kawaida anaweza akaona nchi inapoelekea. kama Elimu ya Msingi ni bure sasa hivi, Elimu ya sekondari na yenyewe ni 'Kama bure'. Shule za msingi na sekondari zinaongezeka kila kukicha. kizazi kijacho kitakua kimezoea 'Elimu ya bure' na hawatokua na 'MAADILI'.
MIPANGO thabiti inahitajika ili kuikomboa sekta ya Elimu, La sivyo Tanzania itaangukia kwenye mikono ya wasomi wasio na akili (EDUCATED FOOLS) ambao wanajali maslahi binafsi tu.